Ninaomba uanzishe Thread yako inayosema mabaya ya EL.Heri ya mchawi, kuliko mnafiki kama lowasa, kwanini mpaka leo amekaa kimya juu ya ukweli wa richmond.. Hana lolote ni mwizi tu huyo, kama si mwizi kwanini alikubali kujiuzuru.... Hujajifunza tu kilicho mpata arumeru yeye na mkwe wake, endeleeni kujidanganya na lichama lenu la wezi, wazinzi, na wachawi kila siku kwa waganga, mnadhani ikulu ni mahali pa kuchezea tu mpaka waganga wa kienyeji mnawaweka katika payrol ya kila mwisho wa mwezi kwa sababu ya kumganga dhaifu wenu na mavirus yake... Pole zenu, mungu wetu si kiziwi. Lowassa hana tofauti, mwakyembe au, mwandosya... Ni wanafiki watupu.
Mkuu Annael, nisaidie katika haya;
1. Kwanini Tuseme aliyoyafanya Mh. Edward Lowassa(MB), vipi kwa wabunge, au wengine wastaafu?
2. Tutaje akiwa kama mbunge(MB) au na nyadhifa zingine?
3. Kwanini tuseme "mazuri" aliyoyafanya Mh EL tu, yale mabaya?
4. Tukishayataja, iweje?
Naomba hapa wana JF tuseme Mazuri ya EL aliyoyafanya katika nchi yetu.
MODs kwa sababu mimi nimeanzisha uzi huu atakayeleta matusi futeni comment yake.
Yafuatayo ni baadhi ya mazuri.
1. Bomba la maji toka ziwa victoria: Viongozi wote wa Tanzania waliogopa kuchuka maji kutoka ziwa victoria eti kwamba makubaliano ya nchi kandokando ya mto nile. Lakini kwa ushupavu wa EL leo hii watu wa mkoa wa Shunyanga wanafurahia maji toka ziwa victoria.
2. Misimamo yake na nia thabiti: EL anamisimamo iliyo thabiti na yenye kuleta maendeleo katika nchi, EL haogopi yuko tayari kufanya maamuzi magumu kwa faida ya nchi.
haya ni baadhi tu ta mazuri kama unajua na wewe basi tupia.
1. Wabunge wengine siku nyingine tutawataja na kueleza mazuri yao, Ngoja leo tuongelee EL.
2. Nadhani A na B sawa.
3. Kwasababu leo tunataka tueleze mazuri tu siku nyingine tutaongelea mabaya yake.
4.Tukishataja kuna watu walikuwa hawajui mazuri yake basi watajifunza kutokana na uaminifu wetu wa kutaja mazuri ya EL.
NB: Kuna watu watakuja kutumia hizi comment zetu kwaajiri ya kujibia mitihani, kufanyia reseach nk.
Kama haujui mazuri ya EL wapo watakujuza poa rafiki?Sasa mkuu, yaani hao watu(ambao umesema hawajui) washindwe kujua "MAZURI" aliyoyafanya muda wote wa uongozi ( nyadhifa zote alizowahi kushika hadi sasa) na waweze kuutambua kwa thread hii?!
Hapo sehemu ya nne umesema watu walikuwa hawajui mazuri yake, inawezekana hakuna "mazuri" kwao na ndio maana hawasemi na kama hawajui hayo mazuri inawezekana wanajua mabaya...Then kwa nini tusianze na hayo mabaya watu wanayoyajua?
Sijui kwa wengine ila kwangu mimi naona kama unataka kumsafisha, na kama sivyo(yaani kamauna nia nzuri) then this is a wrong approach.
Ninaomba uanzishe Thread yako inayosema mabaya ya EL.
Ninaomba muitoe.
Kama haujui mazuri ya EL wapo watakujuza poa rafiki?