Sikumbuki mazuri yake ila ntasema "Mazuri tunayomfanyia sisi wananchi na kodi zetu"
a) Anapata kiinua mgongo (pension) kama "retired PM ambayo ni amount nzuri kwelikweli! japo ni mwizi na mhalifu
b) Bado ni MP japo hajatutendea vema wananchi wa TZ kama PM kashfa kibao
c) Hajapelekwa mahakamani kama Mramba, Yona, Mgonja etc kwanini? I can't wait that happening.
a) Yes ni yeye pekee ndio amedhihirisha bila hofu kwamba ni mchafu -soma ripoti ya Mwakyembe hakuna PM mwingine -kimsingi kuendelea kumlipa mafao kutokana na kodi zetu ni favour au huruma tu ya wabongoa]ni ishu ya katiba hiyo hata waliopita wanapata hiyo kiinua mgongo,umemuona huyu tu ndio mchafu?
b]ni jambo ambalo ni la wananchi wa monduli kuamua kumuondoa au kumwacha mwakani,kama nawe ni mmoja wao hamasisha mmpinge asirudi mjengoni.
c]uchunguzi[kama upo]unaendelea
mbona nchi ingeendeea, jamaa alikuwa mtenda kazi mzuri sana, aneweza kuwafunika kikwete na kina pinda wote, na alikuwa anamsaidia sana jk kwenye urais wake na kama lowasa bado angekuwepo madarakani, nakwambia kungekuwa na badiliko fulani....achana na richmond, ktk hao wote uongozini hakuna mtakatifu. walimtoa muhanga tu ila wengi wapo na hatuna proof kwamba alikula rushwa so hatuna la kusema. ninamshukuru sana kwa kuhamasisha ujengaji wa shule za kata ambazo watoto wengi wamesoma hadi sasa hata kama walimu wachache, at least we have school buildings, angeendelea hata hao walimu wangekuwepo tu...pinda hafanyi lolote, ukimjumlisha na kikwete ndo hamna kitu kabisa...bora lowasa pengine angekuwa anawaficha kidogo.
M
Hata hizo shule mnazosema alijenga, alitumia mabavu zaidi ya kutumia akili. Utajengaje shule bila kuwa na uhakika wa walimu watakaofundisha kwenye shule hizo. Tulipopata Uhuru viongozi makini na waliokuwa na akili vichwani mwao walianza kwa kufundisha wananchi. Mara baada ya Uhuru vyuo vilivyokuwepo vilipanuliwa na vingine kujengwa ili watakaohitimu waweze kufundisha wengine. Lakini nyie wenzetu mnashabikia shule ambazo hazina walimu wala madawati! Ama kweli akili ni nywele kila mtu ana zake!
Namkubali sana mzee pinda, namkubali sana huyu kiongozi wangu wa nchi kwa kuwa ni mchapakazi.lkn ningalitamani waziri mkuu mstaafu El kurudi tena bungeni na kuwa waziri mkuu , kwani licha ya kuwa mkali kwa watumishi wabovu, lkn pia utendaji kazi wake hasa pale alipoamuru bandari ya dsm kufanya kazi masaa 24 pale nimemkubali na matunda yake tumeyaona
ndo we wakuuliza utajenga nyumba kama hauna uhakika wa mtu kuja kukaa? ndiyo, jenga kuna siku tu mtu mhitaji atajitokeza kuja kukaa kwenye hiyo nyumba, so are for schools, kama alijenga bila kuwa na uhakika na waalimu mbona walimu wanazaliwa kila siku, si bora hata hizo zipo? na kama unasema alitumia mabavu, bora anayetumia mabavu kufany akitu kinachoonekana kuliko anayetumia maneno laini halafu hakuna chochote kinatendeka. haujui kama udictator wakati mwingine ni bora kuliko demoncracia?
huyu jamaa ni mtenda kazi safi, tz hatuhitaji watu waliozubaa, wenye maneno malaini vitendo vichache...kitendo chake cha kushabikia matumizi ya maji ya victoria kilimfanya mkuuu wa nchi kumchukua kwasababu jk ana interest na waarabu wa kaskazini....hatujui waliongea nini na waarabu na alipewa nini hata akamtosa rafiki yake kipendi aliyemsaidia sana kuupat ahata huo urais.....unafikiri ulikuwa ni uaminifu wa jk au usafi wake? nooooo, bora lowasa kuliko kikwete na pinda. mara mia.