Hala halaaa halaaa nyie wanaume wa Kitanzania msidhani tunafurahia sana hii tabia yenu mbaya,mmetugezua sisi uwanja wa mazoezi kila siku mwacheza viwanja vyetu vya nyumbani lakini Mechi mwaenda nchi za jirani,hamjielewi mwadhani sisi tutaolewa na nani kama nyie mwaoa Rwanda,Kenya,Uganda sijui wapi mwafikiri kuwa wanawake wa huko wazuri kuzidi nyumbani kwenu,ama kweli nabii hakubaliki kwao,kwa taarifa yenu tulifanya jitihada zote tukamtoa nduli zari wa Uganda.
Wanawake wa Tanzania tupo kwenye maombi mazito hizo ndoa zenu ziwe majanga muachane mrudi nyumbani kuoa Ally kiba tunaokumbea uachane na huyo mwanamke waty wa Mombasa wakusaidie weee urudi nyumbani uoe umezalisha huku kama kuku halaf unaenda kuoa jirani hii dharau tukiwaroga mnalalamika,tunawaambieni dawa zenu zinachemka ,mbona mimi nilimuacha msomali nimekuwa na Mngoni wangu G kwa sababu mim ni mzalendo ila na mapigo yalichangia tu kiukweli ndio maana G akafanya mapinduzi makubwa akachukua mzigo jumla ni uzalendo tu pia (Mngoni Nakupendaaaaaaa balaaa)
Tunaomba Mheshimiwa Makonda najua unapita pita humu naomba utusaidie wanawake wa Tanzania mwishowe wote watakuwa wasagaji sasa ,maana wanaume wanakimbilia jirani tu,ingilia kati hili swala hakuna mwanaume kuoa nje ,mazoezi nyumbani mechi ziwe nyumbani pia alaaa, hapa mtakuja na visingizio hakuna cha visingizio sijui oooh tupoje hamridhiki nyinyii
Mnakimbilia kwa watu wa Rwanda wenye visimi virefu kama ile dawa ya mbu ya zamani ile ilikuwa ya duara nimeisahau jina,watu wana maji kama mito,mnaacha wanawake wa kitanzania wazuri,waaminifu,hawapendi pesa ,wanajua kupika,wanajua mapenzi mnataka laana nyie wanaume wetu,mnatukosea sana.
Tupo kwenye maombi mazito yeyote anaethubutu kuoa nje au kufikiria tunaomba aache mara moja,na ndoa zenu zitakuwa majanga mrudi nyumbani mtakuwa mnadanganywaa ooh huyu mgeni kaka yangu kumbe bwana ake,tena wanawake wa kitusi ndio tabia zao umemuoa wewe lakin akienda salimia kwao anarudi na ujauzito maana wanajionaga wale nao utafikiri wazungu
Kuweni wazalendo pendeni vya kwenu
Povu ruhusa maana hampendi kuambiwa ukweli
Wanawake wa Tanzania Tuseme Ameeeen
Mama Sabrina nishamaliza ukipenda niite mama G