Maziwa fresh, Kiswahili chake ni nini?

Maziwa fresh, Kiswahili chake ni nini?

Hii definition naona inakaribiana na uhalisia wa ukweli.

Mie nadhani ni hivyo na ukiomba aina nyingine ya maziwa labda utasema naomba Mtindi (ukimaanisha maziwa mgando), shida inaanza pale tunapoacha kutumia neno moja kama MTINDI na badala yake tunatumia maziwa mgando na hapo ndio chanzo cha MAZIWA FRESH na MAZIWA MGANDO
 
Nimekupata sawia mdau wa madhiwa
 
Naomba kwa mwenye kujua, anisaidie. Maziwa fresh kwa neno moja la kiswahili huitwaje? Mfano, maziwa ya mgando ni mtindi. Je yale ambayo hayajagandishwa je?

Maziwa mabichi.
 
Jamanieee,kukata mziz wa fitna tena kwa nianjema tuyaite MAZIWA MABICHI au ukipenda uyaite MAZIWA YASIYOCHACHU(yasiyochachuka)
Hapo vipi wadau?
 
Naomba kwa mwenye kujua, anisaidie. Maziwa fresh kwa neno moja la kiswahili huitwaje? Mfano, maziwa ya mgando ni mtindi. Je yale ambayo hayajagandishwa je?

Tanzania tumejaaliwa kuwa na hazina ya lugha za makabila mengi lakini hatuzitumii kukikuza Kiswahili.

Sisi kwa Kirangi maziwa ambayo hayajaganda tunayaita "Jororo" na maziwa yaliyogandishwa tunayaita "Mpototo".

Kama hakuna neon la Kiswahili nashauri tukope maneno haya ya Kirangi kama Nyerere alivyotukopesha neno la Kizanaki la "Kung'atuka"
 
Yah, Jororo nitaanza kulitumia neno hilo kuanzia sasa. Na nina imani, baadhi ya watu watalizoea na kulisambaza neno hilo
 
Back
Top Bottom