Maziwa fresh, Kiswahili chake ni nini?

Maziwa fresh, Kiswahili chake ni nini?

Mleta mada umekosea kuandika sentens yako embu tuambie maziwa fresh IPO katika lugha gani?
 
Maziwa fresh ni maziwa tu. Ila katika kutofautisha na aina nyingine mf maziwa mgando yanaitwa mtindi au maziwa lala. Maziwa ya unga
 
maziwa ni maziwa. ila mtindi ndio maziwa yaliyoganda. fresh milk and milk

Kweli mkuu maziwa ni maziwa na ya kiganda yanaitwa mtindi hatuna haja tena ya kusema maziwa yaliyoganda (hii inakuwa tafsiri ya mtindi)
 
wewe umeandika maziwa fresh ila unataka neno moja. kwa nini? kwa maneno mawili ni maziwa yasiyohoshiwa

Haya ndio yale yanayopatikana kwenye Biblia au pale dukani kwa Mangi Ndorobo?
 
Hiyo "fresh" ni mbwewe tu kwani neno "maziwa fresh" tayari linashida si kiswahili wala sio kiingereza, kwa kiswahili kuna MAZIWA na ukiomba maziwa utapewa hayo maziwa ambayo wengi wameongeza neno fresh lakini kimsingi ni MAZIWA

Hii definition naona inakaribiana na uhalisia wa ukweli.
 
Back
Top Bottom