Mazishi ya mtu hai kishirikina

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
888895-IMG_3878.jpg

Wengi wetu wamefanyiwa mazishi wangali hai. Wapo hai lakini kiroho wamezikwa na wanateseka sana. Unapozikwa hai kishirikina unapoozwa na kufifishwa nyota yako. Unapozikwa hai kishikirina kinga zako za kiroho zinapungua nguvu hivyo hakuna rangi utaacha kuona.

Vitu vyenye vinasaba nawe ni muhimu sana kuvitunza na kuvilinda.. Vitu kama nguo hasa za ndani, kuchwa zako, nywele zako zozote, damu yako, picha yako nk. Imethibitika hata kwenye sayansi ya macho kuwa chochote unachogusa unaacha alama yako hapo, alama za vidole ama kinasaba chochote.. Watu waliosoma forensic wanalijua hili vema.

Hivyo basi hata kwenye ushirikina huwa wanatumia kitu chenye kinasaba nawe kukutengeneza. Sasa basi katika vyote hivyo picha ndio huwa rahisi kupatikana kwakuwa ni ngumu kumtaimu mtu mpaka umkate kucha yake au umnyoe nywele zake, ama umtaimu saluni akinyoa au kusuka. Lakini picha tu..unaeza ipata hata mtandaoni

Picha kiroho imebeba maisha yako. Kuna connection kubwa sana kati yako na picha yako kiroho. Kumbuka ile mada ya Tafsiri ya picha katika ulimwengu wa roho. Maranyingi tunapiga picha na watu wetu wa karibu au wa mbali tunaowajua na tusiowajua, na baada ya picha tunadhani tumemaliza. Kwenye kila picha upigayo kuna alama muhimu unaacha

Ukiwa mbabe picha yako inaweza kutumika kukumaliza. Chukulia tu mfano wa kidunia fanya tukio baya kwenye jamii, kazini kwako nk. Picha yako ndio itatumika kukutafuta na ndio itasaidia kupatikana kwako na kupelekwa kwenye sheria

Sasa unawezaje kuzikwa ukiwa hai? Nikipata picha yako, maji ya mochwari, jeneza dogo, sanda nk. Naweza kukufanyia mazishi kamili kisha nikakuzika na kuanua tanga siku ya tatu. Nikiamua kukumaliza kabisa siku ya 40 (siku ya kukatika kichwa) ninafanya kafara la kuchinja mnyama

Ishi tu vizuri na watu, tenda yaliyo mema. Usiwaumize wengine kwakuwa tu hawana ulichonacho wewe, usiringe, usikashifu wengine, jali hisia za wengine, ziheshimu. Ukijifanya mjuaji sana utazikwa ungali hai halafu utaona yajayo yanavyofurahisha. Ukijitahidi kuishi maisha ya ukamilifu hata tufani na mapigo ya kishirikina yatakupitia mbali kwakuwa utakuwa na kinga imara za kiroho.

NB: Usijaribu kufanya hii michezo kama na wewe una mapungufu yako! Hapo kuna mawili kufeli ama yakurudi!
 
Usemacho ni kweli, mimi ni mfano ambao niliwahi kuzikwa kishirikina, lakini Yesu akanitoa kwenye hilo kaburi au gereza.

Masikitiko yangu ni kwamba mtoa mada hujaelezea jinsi ya kufufuka kutoka kwenye hilo kaburi, na dalili zipi utazijua kama wewe binafsi umeshazikwa.
 
Usemacho ni kweli, mimi ni mfano ambao niliwahi kuzikwa kishirikina, lakini Yesu akanitoa kwenye hilo kaburi au gereza.
Masikitiko yangu ni kwamba mtoa mada hujaelezea jinsi ya kufufuka kutoka kwenye hilo kaburi, na dalili zipi utazijua kama wewe binafsi umeshazikwa
Wewe umesema ni mfano wa aliyekumbwa na madhila hayo. Mbona unauliza tena mtu atajuaje kuwa amezikwa? Kwani wewe ulijuaje?
 
Usemacho ni kweli, mimi ni mfano ambao niliwahi kuzikwa kishirikina, lakini Yesu akanitoa kwenye hilo kaburi au gereza.
Masikitiko yangu ni kwamba mtoa mada hujaelezea jinsi ya kufufuka kutoka kwenye hilo kaburi, na dalili zipi utazijua kama wewe binafsi umeshazikwa
Pole sana sana.. Nadhani hujanisoma vema nimeongea vyote mkuu
 
Back
Top Bottom