Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
dole gumba.jpg

Alama ya dole gumba au utambulisho wa mboni yako ni utambuzi wa kibaiolojia ambao hutumika kama njia ya kumtambua mtu na kuruhusu kufikia au kufungua vitu fulani.

Ikiwa mtu au kampuni yenye nia mbaya inapata nafasi ya kufikia alama zako za utambulisho, taarifa zako binafasi kama miamala ya kibenki, picha, video, anuani, jumbe na kadhalika zinaweza kufikiwa kirahisi na kutumiwa dhidi yako kwa kukutisha ili utoe hela au hata kufanyia uhalifu. Lakini pia madhara hayo yanaweza yasiishie kwako tu, yakahusisha na watu wengine na hivyo kusababisha hasara kubwa.

jichoo.png

Tunatumiwa jumbe kila kukicha “Ile hela tuma kwa namba hii” au “Umeshinda bahati nasibu piga huku kuchua hela yako” au “Kujiunga na Freemason, kurudisha mpenzi aliyekuacha mjukuu wa babu anasuluhisho lako” lakini wahusika wakitafutwa hawajui kinachoendelea. Hii ni kwa sababu wahalifu hao wanakuwa wametumia alama ya kidole cha mtu kusajlia line zao.

Hivyo ni muhimu sana kujiridhisha kwanza kabla hujatoa utambulisho wako sehemu kuwa, taarifa zako zitakuwa salama na hazitatumiwa vibaya na kama zikitumika vibaya vipi unaweza kuwawajibisha. Vivyo hivyo, pia ni muhimu kwa kampuni na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali kuhakikisha mifumo yao ya utambuzi ni thabiti na ina viwango vya juu vya usalama katika kulinda taarifa binafsi na faragha za watu ili zisiweze kutumiwa vibaya.
 
Back
Top Bottom