Mazishi ya Fr Evaristus Mushi: Dr. Slaa na Mtikila wanena

Mazishi ya Fr Evaristus Mushi: Dr. Slaa na Mtikila wanena

segwanga

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
2,788
Reaction score
731
attachment.php


Leo ndo mazishi ya Padri Evaristus Mushi aliyepigwa risasi akiwa katika utekelezaji wa majukumu yake na hivi sasa ndo kuaga na kufanya misa ya marehemu. Watu wengi mno na viongozi wa serikali,siasa na dini ya kikristo wamehudhuria. Baadhi ni rais wa zanzibar Dr. Shein, Dr. Slaa,mchungaji Mtikila. Walipotakiwa kueleza wameguswa vipi na kifo cha padri.

Dr slaa amesema ni tukio la kusikitisha kutokea zanzibar kwani znz ndo chimbuko la ukristo kwa Tz. Wamisionari wa kwanza walianzia znz. Ameshangaa haya matukio yanajitokeza siku hizi. Tukio hili halina maelezo ya kina kuhusu chanzo chake. Amesisitiza kuwa tusingependa kifo cha aina hii kitokee kwa mtu yeyote na akasema muda umefika sasa tujadili mizizi ya tatizo na si matawi na matunda ya tatizo.

Naye Mchungaji Mtikila amesema ni muda wa kutafakari,kuonyesha uvumilivu kwa watanzania wote bara na visiwani. Amesema ni kipindi cha kutafakari vitabu vitakatifu vinasema nini. Kwa waislam,amesema korani inasema adui wao si wakristo bali ni mayahudi na makafiri.
Source: Radio Maria
 
Roho wa Bwana yu juu yenu

Luka 18:31-33
Akawachukua wale Thenashara, akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote yatatimizwa, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii. Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa Mataifa, atafanyanyiwa dhihaka; atatendewa jeuri, na kutemewa mate; nao watampiga mijeledi, kisha watamwua; na siku ya tatu atafufuka.
 
Adui wa wanadamu na viumbe wote ni shetani, yeye ana tabia ya kujificha katika maumbo tofauti ambayo wanadamu tunayafahamu na kuyavisha hadhi.

Zamani sana alijificha kwa nyoka ambaye alijulika zama hizo kuwa mwerevu, akaendesha mazungumzo na Hawa mpaka uharibifu ukapatikana. Kwa ulimwengu wa sasa anapoingia kwa wanadamu tunaowajua vizuri usomi na weredi wao anafaulu kutudanganya.

Tumtizame Muumba wetu na tuwasamehe na kuwaonea huruma wanadamu wenzetu ambao shetani anaingia ndani yao na kujitokeza kwa hali ambayo haimupendezi mtu huku yeye akishangilia.
 
DR SLAA Anamaanisha nini kusema Zanzibar ndio Chimbuko la Ukirsto Tanzania?
 
muda umefika sasa tujadili mizizi ya tatizo na si matawi na matunda ya tatizo
hili ndo neno nani chanzo cha udini
 
Back
Top Bottom