Mazingira yamechangia kudumaza ufahamu wa Mwafrika

Andrew Tate

JF-Expert Member
Jun 28, 2020
3,824
5,812
Straight to the point.

Africa ni bara lililosheheni vitu vingi vya asili vyenye thamani.

Vitu ambavyo kama vingetumiwa ipasavyo na inavyotakiwa basi africa ingekuwa moja kati ya mabara yenye nguvu duniani.

Africa ni moja ya bara lenye mazingira mazuri ya kuishi binadamu na asilimia kubwa ya viumbe vingine.

Pamoja na yote hayo ambayo Africa inavyo, Africa ndio bara masikini na la mwisho kwenye almost kila kitu. Sababu ni Africa imeteleza kwenye kitu kimoja ambacho ni ufahamu/akili kwa watu wake.

Ufahamu/akili ndio kitu pekee duniani chenye mchango mkubwa kwenye kila kitu kilichopo duniani leo hii na moja ya vitu hivyo ni technology iliyopo leo hii duniani.

Na ufahamu/akili hicho kitu kama kitapungua au kutokuwepo kabisa basi ni tatizo kubwa. Mfano wa tatizo hilo kubwa ni kilichoitokea africa na kinachoendelea kuitokea africa sasa hivi.

Kumbuka binadamu wote kwa asilimia kubwa tuna ufahamu ulio sawa. Hivyo simaanishi kwamba mwafrika ufahamu wake ni duni! Hapana. Bali namaanisha ufahamu wa mwafrika umedumaa.

Na hicho kitu mojawapo vilivyochangia kudumaza ufahamu wa mwafrika ni "MAZINGIRA".

Binadamu anaweza kufanya chochote na kubobea kwenye hicho akifanyacho kama ameamua na kama anakifanya hicho kitu mara kwa mara hivyo binadamu atabadirika ili kuendana na kinachoendelea kufanyika au kutokea.

Hivyo ukifanya hicho kitu mara kwa mara basi utakuwa mzoefu na utabobea zaidi kwenye hicho unachokifanya.

Ila kama hutoamua basi mazingira ndio yatakayokuendesha na kukubadilisha.

Mfano mdogo ni kama msuli wa binadamu ambao ni moja ya sehemu za mwili wa binadamu ambapo ukinyanyua chuma kila siku basi msuli utazoea na kutanuka ili uweze kunyanyua hicho chuma vizuri zaidi. Kama wale watu wanaokwenda "gym" (kama sijakosea) ili kutengeneza misuli mikubwa na matumbo sita au wanaita wenyewe six-packs.

Na mfano mwingine ni mtu anayeshinda kwenye sofa akiangalia tv na kula bila mpangilio basi lazima huyo mtu mwili wake utakuwa wa hovyo na dhoofu.

Ila hapa sizungumzii six-packs bali hapa nazungumzia "Ubongo" ambayo ni sehemu moja wapo ya mwili wa binadamu na ndio sehemu akili/ufahamu ulipo.

Pia kila mnyama/kiumbe anabadirika ili kuendana na hali halisi ya mazingira yanayomzunguka huyo kiumbe. Ni sawasawa unaposema umtoe simba msituni umpeleke Antarctica basi huyo simba lazima apate tabu sababu ya baridi hadi kufa au umtoe penguin Antarctica umpeleke msituni lazima apate tabu hadi kufa.

Hiyo sababu mazingira hayato-support hao viumbe na pia wao si binadamu viumbe ambao nilishataja sifa zao. Kwamba binadamu anaweza kufanya chochote na kubobea kwenye hicho akifanyacho kama akiamua na kufanya mara kwa mara hivyo atabadirika ili kuendana na anachokifanya.

Wazungu kilichowabadilisha ni mazingira yao
  • Ardhi isiyo na rutuba hivyo ngumu kupata chakula
  • Vipindi virefu vya baridi
  • Ardhi iliyobana
  • Mvua chache nk
Mazingira ya aina hiyo ni ngumu kwa binadamu kuishi.

Hiyo ikampelekea mzungu awe mtu wa kusolve matatizo ili aendelee kuishi na kumbuka nilisema juu kwamba binadamu anaweza kufanya chochote kama akiamua na kama akifanya hicho kitu mara kwa mara basi atakuwa mzoefu na atabobea zaidi kwenye hicho anachokifanya.

Wazungu hawakuamua wenyewe kuwa walivyo bali mazingira yao ndio yamewafanya wawe vile walivyo.

Hivyo mzungu kutokana na kusolve matatizo mara kwa mara ili aendelee kuishi hiyo ikapelekea ubongo wake kubobea kwenye kusolve matatizo na unavyozidi kusolve matatizo unatengeneza curiosity ambapo utakuwa unagundua matatizo mengi zaidi yanayohitaji ufafanuzi na kutatuliwa.

Hiyo imepelekea ubongo wa mzungu kubobea huko na kuwa mzoefu hali inayopelekea kuwa kuwa kawaida kwa ubongo wa mzungu
kuona tatizo au changamoto kila sehemu ambayo Mwafrika kwa asilimia 80% hatodhania kama kuna tatizo au changamoto sehemu hiyo.

Na mpaka leo mzungu anaendelea hivyohivyo na kuendelea kulithishana vizazi kwa vizazi hiyo hali ya bongo zao.

Na ndio maana mzungu anajiuliza kwanini Apple linidondokee tu bila kuguswa na aina yoyote ya kitu kinachoonekana.

Hivyo mazingira ndiyo yamembadirisha mzungu awe hivyo alivyo na sio yeye ameamua yeye kuwa vile alivyo.

Kama ilivyo kwa mzungu Afrika ni kinyume chake. Mwafrika mazingira yake ni mepesi kwa asilimia kadhaa kulinganisha na ya mzungu.
  • Misitu mingi mikubwa na minene
  • Hali nzuri ya hewa
  • Ardhi yenye rutuba
  • Mvua za kutosha na jua la kutosha
  • Chakula cha kutosha nk
Hayo mazingira ni rahisi kwa binadamu kuishi na kuendelea ku-survive.

Hivyo Mwafrika hakuweza kuona au kupata changamoto wala tatizo kubwa sababu mazingira yalimrahisishia kwa asilimia karibu 80% ya maisha yake kuendelea kuwepo. hivyo kuendelea kuishi bila ugumu wala changamoto kubwa zisizoonekana kirahisi.

Hiyo imepelekea ubongo wa mwafrika kudumaa na kulala sababu haujishuhurishi kufanya chochote kigumu wala kutatua chochote kile ambacho kitahitaji nguvu kubwa ya ubongo.

Hivyo ubongo wa mwafrika umekosa uwezo wa kuona changamoto au tatizo na umekosa curiosity sababu ya mazingira. Mwafrika akawa anaishi tu ili mradi ana-exist na kufuata nature kama ilivyo kwa mzungu na sio kwamba alipenda kuwa vile au hivi tulivyo.

(Wewe ujiulizi miembe yote iliyoko afrika lakini hakuwahi kutokea mwafrika hata mmoja kujiuliza kwanini Embe linadondoka lenyewe tu bila kuguswa? Au kujiuliza chochote kuhusu chochote kwanini kinafanyika na kwanini kitokee? Alafu akakiandika ili kila mtu aone?
Sababu ubongo wa Mwafrika umedumaa kwa kukosa changamoto za kutaua na kukosa curiosity.

Na mpaka leo bado wanaendeleza hiyo legacy kwa asilimia karibu 95%.

Hivyo mazingira ndiyo yaliyodumaza ubongo wa mwafrika na si kingine.

Hata hivyo mwanzo kule juu nilisema binadamu anaweza kufanya chochote kama akiamua na kama akifanya hicho kitu mara kwa mara basi atakuwa mzoefu na atabobea zaidi kwenye hicho anachokifanya.

Ila kwakua sasa tumejua nini chanzo au vyanzo vya sisi kuwa nyuma au tatizo ni nini basi tuanze kubadilika. Na kujua chanzo cha tatizo ndio mwanzo wa kutatua tatizo.

Hivyo bado tunaweza kubadilika na kuwafikia wazungu au kuwa zaidi ya wao kwa kuamua na kufanya vitu ambavyo vitaongeza kitu chanya kwenye ubongo wako na kwa taifa kwa ujumla hivyo na sisi Africans tulithishe vizazi vyetu vijavyo hicho kitu. Na hapo tutakuwa tumeipinga nature.

Waafrika amkeni na mbadilike.
 
Waafrika hawa hawa ninaowajua mimi?

Waafrika wameendekeza uchawi mnoo
 
Kingine ni udumavu wa akili unaotokana na lishe duni kuanzia mama akiwa mjamzito, kujifungua na huduma za afya kwa mtoto mpaka kufikia miaka 5 au 7. Akili ikidumaa uwezo wa mwenye hiyo akili kutafakari, kujiendeleza kielimu, kuelimika na pia kukabiliana na changamoto za maisha ya kila siku unapungua sanaa.
 
Ni ukweli na pia ni sababu moja wapo kwakuwa nikiangalia industrial revolution ili anza baada ya kutaka kutengeneza nguo kwa efficiency kubwa ili kujiKinga na baridi hapo ndipo water power na steam engine zilipo anza kugunduliwa. Then machine tools zikafwata
 
Ingekuwa ni hivyo basis sasahivi tungekuwa vizuri kuliko wao maana tunachangamoto kubwa kuliko wao kwa sasa. Kama malaria ni tatizo kubwa kwetu kuliko kwao Ila dawa wanatoa wao tutasemaje mazingira yanafunza? Kama usafiri tu kwetu ni tatizo kuliki kwao na hatujatengeneza hata lingi ya baiskel tutasemaje mazingira ni mwalimu.
 
Ingekuwa ni hivyo basis sasahivi tungekuwa vizuri kuliko wao maana tunachangamoto kubwa kuliko wao kwa sasa.
Hizo changamoto tunazoziona sasa wao walishaziona miaka mingi nyuma na washazimaliza pia.
Ila sisi ndio kwanza tunaanza kuziona leo na misaada wanayotupa inazidi kutudumaza.

Hizo changamoto tunazoziona sasa zilikuwepo miaka mingi nyuma kwanini hatujaziona?
Hatujaziona sababu kulikuwa na asilimia kubwa ya uwezekano wa kuendelea kuishi kutokana na mazingira.
Tumeweza kuziona hizo changamoto baada bongo za waafrika kuanza kua
advance taratibu.
Ndio maana nikasema mzungu anaweza kuona changamoto sehemu ambayo mwafrika hawezi dhania.

Kama sasa hivi jamii ina changamoto nyingi na serikali wala watu wake hawazioni.
Kama malaria ni tatizo kubwa kwetu kuliko kwao Ila dawa wanatoa wao tutasemaje mazingira yanafunza? Kama usafiri tu kwetu ni tatizo kuliki kwao na hatujatengeneza hata lingi ya baiskel
Now unanielewa.

Dawa wanatoa wao sababu mazingira yao yaliwawezesha kuwa wadadisi na kuweza kutatua changamoto nyingi pia kuweza kuona changamoto sehemu ambayo mwafrika ni ngumu kuona kama kuna changamoto.

Malaria ni hatari kwa mzungu kuliko mwafrika.
Hivyo mzungu alishatengenza dawa tangu zamani ili asiendekee kufa.

Mwafrika ana kinga imara juu ya magonjwa kuliko mzungu.

Wewe umeona corona ilivyoshindwa kuvunja kinga zetu za mwili lakini wazungu wanapukutika hivyo wakaanza kuhaha kutafuta kinga na dawa na chanzo cha ugonjwa huku sisi tunasema mungu atatusaidia?

Jiulize Malariaa tumeanza kuijua mwaka gani? Bila shaka miaka 200 150 nyuma.
sasa kwani Malaria haikuwepo hapo kabla?
Hapana ilikuwepo.
sasa kwanini hatukutengeneza dawa zetu zenyewe na kuziendeleza?
Sababu hatukuwa na wazo hilo.

ila sasa hivi ndio tunagundua Malaria ni tatizo wakati Malaria ilikuwepo miaka mingi nyuma.

alafu mkuu ngoja nikupe mfano mdogo wa changamoto lakini mpaka leo mwafrika hajaona kama ni changamoto sababu kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kuishi na hizo changamoto bila ya yeye kuathirika hivyo ubongo wake umelala na kushindwa kung'amua kama ni changamoto hata kama anajua ni changamoto lakini hawezi au kashindwa kusolve.

•Nyumba zilizojengwa bila mpangilio.
•Mfumo mbovu wa elimu.
•Umasikini.
•Mazingira mabovu na miundombinu mibovu
•Uchafu
•Uwezo mdogo wa kufikiri (nadhani mimi pekee ndio nimeliona hilo)
•Kutumia lugha mbili tofauti kufundisha wanafunzi na kuswitch ghafla kuelekea lugha ya pili.
•Bara lenye utajiri mkubwa wa asili lakini hapohapo ni bara masikini kuliko yote

Hizo ni changamoto chache kati ya nyingi ambazo mwafrika hazioni hivyo yeye anaona kawaida kikubwa yeye ataendelea kuishi sababu mazingira yanamsupport asilimia nyingi za kuwa hai.
Na ubongo wake umekosa curiosity na uwezo wa kutatua na kuona changamoto.

Wazungu wamejiuliza kwanini baadhi ya waafrika wanajisaidia nje badala ya chooni.
Wakaja najibu kwamba itakuwa vyoo vinatoa harufu mbaya iliyopitilza hivyo mwafrika anaona bora ajisaidie nje na wakati hiyo ni hatari sababu kunaweza kulipuka kipindupindu na millions kufa.

Hivyo mzungu ametengeneza dawa ambayo unamwaga chooni hivyo binadamu akifika chooni na kuanza kuhisi ile harufu mbaya basi ubongo wake utablock ile harufu ili binadamu aliyeingia hicho choo asiisikie.

Sasa umejiuliza kwanini mzungu aone hiyo ni changamoto na kutafuta solution huku waafrika wenyewe akijisaidia nje ili kukimbia hiyo harufu badala ya kutafuta powerful solution ambayo itasaidia kwa kiwango kikubwa baada ya hata kushindwa kusafisha hicho choo au kujenga vyoo vingi zaidi na sio kujisaidia nje.

Now umeona jinsi gani mazingira yamecheza party kubwa kwenye kudumaza ufahamu wa mwafrika.
 
mt
Kingine ni udumavu wa akili unaotokana na lishe duni kuanzia mama akiwa mjamzito, kujifungua na huduma za afya kwa mtoto mpaka kufikia miaka 5 au 7. Akili ikidumaa uwezo wa mwenye hiyo akili kutafakari, kujiendeleza kielimu, kuelimika na pia kukabiliana na changamoto za maisha ya kila siku unapungua sanaa.
mtu anakula ugali tangu kuzaliwa kwake hawezi kuwa na akili za maana zaidi ya akili za kwenda chooni na kivukia barabara
 
Back
Top Bottom