Mazingaombwe ya kutoroka kwa mshukiwa wa mauaji ya msikitini Mwanza

Kazi ilikuwa hivi:
hh.jpg

majambazi.jpg
Wanashambulia kwa mstari.
 
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limesema mtuhumiwa wa ujambazi waliyemkamata kwa matukio ya uhalifu yakiwamo ya uporaji maduka ya miamala ya kifedha na mauaji ya watu watatu msikitini, Hamis Juma, ametoroka chini ya ulinzi wa polisi wakati akiwapeleka mlimani kuwaonyesha wahalifu wenzake. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema mtuhumiwa huyo alikuwa mikononi mwa polisi akiwapeleka mahali walipojificha wenzake katika mlima Kiloleli, baada ya polisi na mtuhumiwa huyo kufika eneo la tukio saa 8:00 usiku, ghafla majambazi waliokuwa wamejificha katika mlima huo walianza kurusha risasi kwa askari ambao walitaharuki na kujibu mashambulizi huku wakimsahau mtuhumiwa aliyewapeleka. ‪#‎Akasepa‬!

MY TAKE;
1. Hii milima si tuliambiwa sasa imesafishwa na majeshi yetu?
2. Polisi waliendaje na mhalifu sugu milimani usiku wa manane?
3. Mhalifu alikuwa anakwenda kuwaonesha polisi wahalifu wenzake, sasa ilikuwaje Polisi hawakutegemea kuwa lazima mapambano yatatokea, unawezaje kwenda kukamata genge la wahalifu kama vile unakamata mbuzi zizini?
4. Kwa hiyo polisi wamempoteza jambazi mkuu na majambazi wasaidizi wote usiku huo!

Enzi za mazingaombwe zimerudi, sasa naanza kumkumbuka pawa Mabula, Pawa Gronda na mapawa wengine waliokuwa wanaambatana na wanamazingaombwe mashuhuri kufanya miujiza mijini na vijijini. Kwamba huyu jambazi ni sawa na yule muuza madawa ya kulevya wa kimataifa, ‪#‎Tuwe_Kizazi_Cha_Kuhoji_Daima‬.

Mtatiro J
Nashindwa kuamini eti ametoroka akiwa mikononi mwa polisi. Serious!!!!!! Halafu kamanda mzima anasimama na kuuambia umma hivyo. Aibu.
 
Si ndiyo maboresho aliyoalikwa rais ayabariki nasema huwezi kuboresha kitu bila kukivunja kwanza tangia Uhuru ni JWTZ pekee ndiyo iliboreshwa baada ya maasi kwa Polisi hawataweza kwa vile ndani take washirika na uhalifu wapo ndani yake
 
Lolote baya linapotokea mbio mtandaoni,jema hutalisikia...tutafika kweli endapo kila mtu akikazania kuangalia na kukosoa udhaifu wa mwingine bila kutoa suluhisho mbadala!
Kama kweli wewe huoni mapungufu katika operation hiyo ya Msangi, basi ulikuwa mshirika! Mhalifu wala hajafungwa leg chains na pingu za mikono pamoja na askari! Bila mbwa! Usiku wa manane bila miwani ya night vision! Ha ha ha ha Msangi asitudanganye!!
 
Hivi hawa majambazi walioua Mwanza wapo wangapi Dar walimua aliye waua watu msikitini mwanza na Tanga hizii sinema zitaisha lini.
Vyema umetaja matukio ya mwanza, Tanga. Lazima ujue hayo sio mapambano dhidi ya jambazi mmoja bali ni mtandao mzima. Mambo ya kusema sinema yanatoka wap?. Liache jeshi la polisi lifanye kaz yake, usianze siasa
 
Nimeanza kumkumbuka Chagonja na wale magaidi kule kwenye mapango ya Amboni huko Tanga. Hivi kweli polisi wanaweza kudhibiti mikutano ya Upinzani lakini wanashindwa kumdhibiti mtu mmoja acheni kujishushia heshima
 
kesho tusishangae kumuona waziri wa mambo ya ndani akienda hapo mlimani kusimamia utafutaji wa huyo jambazi.jishi lenye weledi hua hali ruhusu siasa katika shughuli zake
 
Hapa naona kuna mambo mawili kwa Mtazamo wangu. Huyu jambazi alitumia elimu na ujanja wake kuchezea akili na ujanja mdogo wa polisi. Haiwezekani jambazi ana negotiate na polisi msimfunge pingu wala kumwekea kuzuizi chochote ili asitoroke. Usiku huu wa manane kuambatana na jambaz pasipo kuzuizi ni ukweli unaojionesha hapa kulikuwa na mawasiliano Kati ya jambaz na wenzake. Polisi kwa akili na ujanja mdogo kweli jambazi anacheza na akili zenu na mnaingia kwenye mtego wake. Suala la pili inaonesha huu ulikuwa mpango wa hao wahusika Yaani mapolisi na hawa majambazi, Haiwezekani Usiku huu wa manane askari waliokula kodi za wananchi pale ccp moshi mnapigwa changa la macho Hii inaonesha maboresho yaliofanywa bado sana maana Huyu mkuu wa kituo kutoa oda ya kuondoka kwa jambazi na mapolisi ktk milima hiyo kwa style na mipango hiyo ya kipuuzi, basi mkuu huyo na polisi waliohusika wachukuliwe hatua Kama sheria na utaratibu wa jeshi la polisi linavyosema.
 
Nimeanza kumkumbuka Chagonja na wale magaidi kule kwenye mapango ya Amboni huko Tanga. Hivi kweli polisi wanaweza kudhibiti mikutano ya Upinzani lakini wanashindwa kumdhibiti mtu mmoja acheni kujishushia heshima
Hiyo inatwa kampa kampa tena, kwenye mikutano ukawa wanakuja kama manyumbu so ni easy kuwadhibiti tofauti na kaka jambazi
 
Nahisi huyo alikuwa mshukiwa hewa maana nchi yetu haikomi vitu kama hvo
 
Hivi naomba kuhuliza police Tanzania wanafanya maigizo habari za kuua majambazi mwanza na tanga zinachanganya.
 
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limesema mtuhumiwa wa ujambazi waliyemkamata kwa matukio ya uhalifu yakiwamo ya uporaji maduka ya miamala ya kifedha na mauaji ya watu watatu msikitini, Hamis Juma, ametoroka chini ya ulinzi wa polisi wakati akiwapeleka mlimani kuwaonyesha wahalifu wenzake. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema mtuhumiwa huyo alikuwa mikononi mwa polisi akiwapeleka mahali walipojificha wenzake katika mlima Kiloleli, baada ya polisi na mtuhumiwa huyo kufika eneo la tukio saa 8:00 usiku, ghafla majambazi waliokuwa wamejificha katika mlima huo walianza kurusha risasi kwa askari ambao walitaharuki na kujibu mashambulizi huku wakimsahau mtuhumiwa aliyewapeleka. ‪#‎Akasepa‬!

MY TAKE;
1. Hii milima si tuliambiwa sasa imesafishwa na majeshi yetu?
2. Polisi waliendaje na mhalifu sugu milimani usiku wa manane?
3. Mhalifu alikuwa anakwenda kuwaonesha polisi wahalifu wenzake, sasa ilikuwaje Polisi hawakutegemea kuwa lazima mapambano yatatokea, unawezaje kwenda kukamata genge la wahalifu kama vile unakamata mbuzi zizini?
4. Kwa hiyo polisi wamempoteza jambazi mkuu na majambazi wasaidizi wote usiku huo!

Enzi za mazingaombwe zimerudi, sasa naanza kumkumbuka pawa Mabula, Pawa Gronda na mapawa wengine waliokuwa wanaambatana na wanamazingaombwe mashuhuri kufanya miujiza mijini na vijijini. Kwamba huyu jambazi ni sawa na yule muuza madawa ya kulevya wa kimataifa, ‪#‎Tuwe_Kizazi_Cha_Kuhoji_Daima‬.

Mtatiro J
Kijeshehi hiyo ni negligence!you can not let your captive unwatched before you get your targeted culprits, kijeshi hapo kuna shida
 
Yaani nchini ina full comedy. Vitumbi kuanzia juu hadi chini. Eti kubwa la majambazi na wasaidizi wake limetoroka.
 
Back
Top Bottom