Mazingaombwe ya kutoroka kwa mshukiwa wa mauaji ya msikitini Mwanza

hahahaha nikikumbuka polisi walivyo na mabavu kwa ukawa naishia kucheka tu, waweza sema intelejensia zao na madishi yote ya rada yameelekezwa Ufipa!
 
Hivi hawa majambazi walioua Mwanza wapo wangapi Dar walimua aliye waua watu msikitini mwanza na Tanga hizii sinema zitaisha lini.
Ya kweli na mimi nilisikia hii habari. Sasa huyu aliyetoroka ni nani? Au labda walioua Msikitini MZA walikuwa kadhaa na na aliyeuwawa Dar ni mmoja wa kadhaa!
 
Hawa jamaa ni wasanii sanaa, mbona kuzuia mikutano ya kisiasa huwa hawapelekwi na MTU na hufika eneo la tukio kwa wakati.
 
Lolote baya linapotokea mbio mtandaoni,jema hutalisikia...tutafika kweli endapo kila mtu akikazania kuangalia na kukosoa udhaifu wa mwingine bila kutoa suluhisho mbadala!

Hii inatokea kwa kuwa hata wao hukesha mitandaon kusifiana tu hata katika yale wanayokosea
 
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limesema mtuhumiwa wa ujambazi waliyemkamata kwa matukio ya uhalifu yakiwamo ya uporaji maduka ya miamala ya kifedha na mauaji ya watu watatu msikitini, Hamis Juma, ametoroka chini ya ulinzi wa polisi wakati akiwapeleka mlimani kuwaonyesha wahalifu wenzake. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema mtuhumiwa huyo alikuwa mikononi mwa polisi akiwapeleka mahali walipojificha wenzake katika mlima Kiloleli, baada ya polisi na mtuhumiwa huyo kufika eneo la tukio saa 8:00 usiku, ghafla majambazi waliokuwa wamejificha katika mlima huo walianza kurusha risasi kwa askari ambao walitaharuki na kujibu mashambulizi huku wakimsahau mtuhumiwa aliyewapeleka. ‪#‎Akasepa‬!

MY TAKE;
1. Hii milima si tuliambiwa sasa imesafishwa na majeshi yetu?
2. Polisi waliendaje na mhalifu sugu milimani usiku wa manane?
3. Mhalifu alikuwa anakwenda kuwaonesha polisi wahalifu wenzake, sasa ilikuwaje Polisi hawakutegemea kuwa lazima mapambano yatatokea, unawezaje kwenda kukamata genge la wahalifu kama vile unakamata mbuzi zizini?
4. Kwa hiyo polisi wamempoteza jambazi mkuu na majambazi wasaidizi wote usiku huo!

Enzi za mazingaombwe zimerudi, sasa naanza kumkumbuka pawa Mabula, Pawa Gronda na mapawa wengine waliokuwa wanaambatana na wanamazingaombwe mashuhuri kufanya miujiza mijini na vijijini. Kwamba huyu jambazi ni sawa na yule muuza madawa ya kulevya wa kimataifa, ‪#‎Tuwe_Kizazi_Cha_Kuhoji_Daima‬.

Mtatiro J
Hapo ndiyo baadhi ya makabila usema maweeeee!
 
Abrakadabra nyingine. Nakumbuka abrakadabra sijui ilikuwa ya nani ile tukaletewa jambazi Mkenya. Mnikumbushe.
 
Lolote baya linapotokea mbio mtandaoni,jema hutalisikia...tutafika kweli endapo kila mtu akikazania kuangalia na kukosoa udhaifu wa mwingine bila kutoa suluhisho mbadala!
Kama mema yanavyo pewa kipaumbele na madhaifu ni muhimu kupewa kipaumbele
 
polisi wa kileo ni majanga matupu, Enzi zile askari kunyang'anywa silaha ilikuw ni kigezo tosha cha kufukuzwa kazi, Leo mtuhumiwa aliyefungwa pingu mkononi eti kawakimbia!!!!!!!!!!! Ama kweli Tanzania INA kila sababu za kuingizwa kwenye vitabu vya kumbukumbu vya Dunia
 
Sikutegemea kusikia habari kama hiyo kwa watu ambao ni trained police officers!
 
Kama ni kweli basi kuanzia huyu kamanda na team yake yote ilibidi wafukuzwe kazi mara moja. Haiingii akililini hata mara moja jambazi anatoroka mbele ya ulinzi mkali. Je ailikuwa amefungwa pingu ama la? Kama ndiyo inamaanana amekimbia na mali ya serikali ambaye tunataka kujua nani atalipia kupata pingu nyingine.
 
Hakuna jambazi yeyote aliyepotea

Hata hiyo Jana kamanda msangi alikuwa akizungumza kwa wasiwasi sana hata alikuwa anaogopa kuangalia kamera

Waseme kama mtuhumiwa kafa kutokana na mateso waliyokuwa wakimpa
Au wameamua kummaliza kwa manufaa ya watu fulani

AU
...............
Agizo bado halijatenguliwa
 
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limesema mtuhumiwa wa ujambazi waliyemkamata kwa matukio ya uhalifu yakiwamo ya uporaji maduka ya miamala ya kifedha na mauaji ya watu watatu msikitini, Hamis Juma, ametoroka chini ya ulinzi wa polisi wakati akiwapeleka mlimani kuwaonyesha wahalifu wenzake. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema mtuhumiwa huyo alikuwa mikononi mwa polisi akiwapeleka mahali walipojificha wenzake katika mlima Kiloleli, baada ya polisi na mtuhumiwa huyo kufika eneo la tukio saa 8:00 usiku, ghafla majambazi waliokuwa wamejificha katika mlima huo walianza kurusha risasi kwa askari ambao walitaharuki na kujibu mashambulizi huku wakimsahau mtuhumiwa aliyewapeleka. ‪#‎Akasepa‬!

MY TAKE;
1. Hii milima si tuliambiwa sasa imesafishwa na majeshi yetu?
2. Polisi waliendaje na mhalifu sugu milimani usiku wa manane?
3. Mhalifu alikuwa anakwenda kuwaonesha polisi wahalifu wenzake, sasa ilikuwaje Polisi hawakutegemea kuwa lazima mapambano yatatokea, unawezaje kwenda kukamata genge la wahalifu kama vile unakamata mbuzi zizini?
4. Kwa hiyo polisi wamempoteza jambazi mkuu na majambazi wasaidizi wote usiku huo!

Enzi za mazingaombwe zimerudi, sasa naanza kumkumbuka pawa Mabula, Pawa Gronda na mapawa wengine waliokuwa wanaambatana na wanamazingaombwe mashuhuri kufanya miujiza mijini na vijijini. Kwamba huyu jambazi ni sawa na yule muuza madawa ya kulevya wa kimataifa, ‪#‎Tuwe_Kizazi_Cha_Kuhoji_Daima‬.

Mtatiro J
Kazi ilikuwa hivi:
hh.jpg

majambazi.jpg
 
Hahahahaha hahahaaa Askari waoga hawa! Ubabe wao kwa vijana WA Chadema tu wakikutana na nanihii wanaufyata
 
Hata kama Polisi wamewaua hao watuhumiwa lakini kusema ati walimpoteza mtu hatari namna hiyo bila hata majeruhi yeyote wa Polisi au jambazi, hakika haipendezi. Haiingii akilini kabisa!!!!
Mtuhumiwa alikuwa ameachwa peke yake kwani alikuwa askari mwenzao?? Sijawahi kuwa Polisi lakini kama uzembe huu upo huko kwao, siutaki Upolisi.
 
Lolote baya linapotokea mbio mtandaoni,jema hutalisikia...tutafika kweli endapo kila mtu akikazania kuangalia na kukosoa udhaifu wa mwingine bila kutoa suluhisho mbadala!
Unafamilia wewe?kama unayo mambo yanapofanywa hovyo hovyo nyumbani kwako huwa unaangalia tu bila hata kukemea? Sasa hebu toa suluhisho kwenye Hilo jambo tuone
 
Hiyo ni zuga tu. Wanajua walikompeleka huyo gaidi.
Ila nimtakie RIP Juma otherwise wasambaze picha yake kwenye mitandao ya kijamii tuwasaidie kumkamata.
 
Lolote baya linapotokea mbio mtandaoni,jema hutalisikia...tutafika kweli endapo kila mtu akikazania kuangalia na kukosoa udhaifu wa mwingine bila kutoa suluhisho mbadala!

Ukiona wenzio wanakimbilia mtandaoni kupost habari mbaya tu na wewe uwe unakimbilia kupost mazuri unayoyaona, sidhani kama umekatazwa.
 
Back
Top Bottom