Singida: Wananchi walalamika mauaji ya watu mfululizo, ufukuaji makaburi na kuchukua nguo za ndani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Singida.jpeg
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Manyoni imetakiwa kuchunguza mauaji ambayo yamekuwa yakiripotiwa kutokea mfululizo pamoja na vitendo vya ushirikiana vinavyohusisha kufukua maiti na kuchukua nguo za ndani na baadhi ya vitu vya thamani.

Maagizo hayo yametolewa Januari 20, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba wakati wa kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Manyoni na Itigi ambapo wananchi hao walilalamikia mauaji yanayotokea karibu kila wiki huku marehemu wakiwa wanakutwa hawana nguo za ndani.

"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa hapa Manyoni vifo vimekithiri sana kila wiki lazima tuokote maiti mahala fulani lakini sio kwamba wananchi wa Manyoni hawawafahamu wahalifu bali wanawafahamu ," alisema Prisca Maleta.

Aidha Katika hali ya kushangaza,wananchi hao wamedai kuwa mauji hayo ambayo yanadaiwa kuibua hofu kubwa kwa jamii baadhi ya pikipiki zinazomilikiwa na askari polisi wa Manyoni kwa ajili kuendesha biashara zao ndizo zinahusika kutumika kwenye mauaji hayo.

"Kuna baadhi ya askari kwa sura na majina ila siwezi kuwataja hapa ila ukihitaji nitakutajia wana pikipiki zao ambazo ndizo zinashiriki kwenye uhalifu," alisema.

Mwananchi huyo alieleza kuwa wananchi wanashindwa kutoa taarifa polisi kutaja wanaohusika na uhalifu huo kwasababu baadhi ya polisi sio waaminifu katika kutunza siri za waleta taarifa.

"Tatizo linakuja kwa Jeshi la Polisi mimi kama Prisca ninapokwenda kutoa taarifa polisi kabla mtuhumiwa hajaenda kukamatwa wanampa taarifa kuwa fulani amekuja kukuripoti huku,vitentldo hivi ndio vinasababisha vifo kuongezeka kwasababu kunakuwa na visa na visa," alisema Maleta mbele ya Mkuu wa Mkoa, Serukamba.

Aidha alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa mauji hayo OCD Mratibu wa Polisi Ahmad Makele alikiri uwepo wa mauaji hayo ambapo alisema tayari walishaanza uchunguzi na kuwakamata baadhi ya watuhumiwa kwa ajili ya upelelezi huku akidai kuwa vifo hivyo havitokani na visasi.

"Vifo vinavyotokea sio vya kisasi wala kuwania mali sababu mtu akiuawa vinachukuliwa viungo vya mwili wake kama vile sehemu za siri,"alisema Makele.

Kutokana na malalamiko hayo ya wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Serukamba amemwagiza Afisa wa Usalama wa Taifa wa Wilaya ya Manyoni (DSO), kuunda kamati itakayoshirikisha vyombo vyote vya usalama kuchunguza mauaji hayo.

"Haiwezekani watu wanauawa kirahisi rahisi na serikali ipo, vinginevyo tumwambie IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini) awaondoe Manyoni,pia hatuwezi kuwazuia na polisi wanaoshirikiana na wahalifu, hatuwezi kuwafukuza kazi lakini tunaomba wapelekwe mikoa mingine hapa tunahitaji kuona polisi wema ambao wanalinda wananchi na mali zao," alisema.

Mkuu wa Mkoa huyo alisisitiza kuwa Jeshi la Polisi linao uwezo wa kuwatambua wahalifu,washirikina na wanaofukua makaburi ili wabainike na kuweza kuchukuliwa hatua kali za kisheria
 
"pia hatuwezi kuwazuia na polisi wanaoshirikiana na wahalifu, hatuwezi kuwafukuza kazi lakini tunaomba wapelekwe mikoa mingine hapa tunahitaji kuona polisi wema ambao wanalinda wananchi na mali zao," alisema."

Polisi wanaoshirikiana na wahalifu wapelekwe mikoa mingine?ili wakaendelee na uhalifu si ndio?

Tulishasema humu U-DC,U-RC ufutwe hawa watu hawana kazi wala hawana tija zaidi kuongeza matumizi,ni chawa waliochangamka.
 
Back
Top Bottom