Maziko ya mastaa,watangazaji,wanasiasa na wanajeshi yanapewa kipaumbele

Mar 1, 2012
29
10
Maziko ya mastaa,watangazaji,wanasiasa na wanajeshi yanapewa kipaumbele kwenye vyombo vya habari na wanasiasa wanahudhuria kwa wingi lakini ikiwa ni mwalimu,mkulima,mvuvi,mfugaji au bwana shamba, daktari hakuna msisitizo kama huo.je hao si watu watz wenzangu?mbona twabaguana?nilishalifuatilia hili kwa muda nikagundua tofauti hiyo tubadilike tutende haki kwa wote.
 
Duh basi mzee amekusikia, msh2e tu misiba ya walimu madaktari na wakulima atahudhuria mradi taarifa tu. Si unajua ni full kamanda so ananguvu za kutosha hofu ondoa. Nchi ya malalamiko!!!!!!!!
 
Maziko ya mastaa,watangazaji,wanasiasa na wanajeshi yanapewa kipaumbele kwenye vyombo vya habari na wanasiasa wanahudhuria kwa wingi lakini ikiwa ni mwalimu,mkulima,mvuvi,mfugaji au bwana shamba, daktari hakuna msisitizo kama huo.je hao si watu watz wenzangu?mbona twabaguana?nilishalifuatilia hili kwa muda nikagundua tofauti hiyo tubadilike tutende haki kwa wote.

Mkuu haya mambo ya Mastaa maziko yao kutangazwa au kuudhuliwa na watu wengi sio Tanzania tu dunia nzima ipo hivyo..

Mfano tumeona mazishi ya Michael Jackson, Whitney Houston huku Marekani.

Mfano mwingine mazishi ya Rais wa zamani wa Zaire, Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa Za Banga.

Huyu alizikwa na watu 8.
 
Mimi nashangaa ni kwa nini serikali inatumia fedha za walipa kodi kugharimia shughuli za mazishi za marehemu ambao si viongozi wala watendaji wa serikali. Hii tabia ya kuchota fedha zetu kugharimia mazishi ya Super Stars ni kielelezo cha ubaguzi wa serikali kati ya Super Stars na Non Super Stars. Binafsi sijaona sababu ya msingi ya serikali kubeba gharama za mazishi ya Kanumba wakati masters wengi tu mfano Mr Ebo, Pwagu, Remmy Ongala, nk wamekufa na serikali haikugharimia chochote.

Vinginevyo serikali ianze kugharimia mazishi ya Watanzania wote maana wote ni muhimu.
 
Mkuu haya mambo ya Mastaa maziko yao kutangazwa au kuudhuliwa na watu wengi sio Tanzania tu dunia nzima ipo hivyo..

Mfano tumeona mazishi ya Michael Jackson, Whitney Houston huku Marekani.

Mfano mwingine mazishi ya Rais wa zamani wa Zaire, Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa Za Banga.

Huyu alizikwa na watu 8.

pole na msiba mkuu
 
Nchi isiyothamini wanajeshi wake ni sawa na mtu aliyeradhi kutembea uchi wa mnyama mchana kweupe bila hofu.
 
Back
Top Bottom