Msukuma_De_Great
JF-Expert Member
- Nov 26, 2016
- 1,185
- 975
Amen
asante ndugu yangu wapo wajinga humu wanatamani hata mabaya yatokee ili wapate nafuu,lakini unajiuliza ni nafuu gani hii wanayoitafuta hawa wenzetu?Nakumbuka ambavyo mwaka 2008 nilipokamatwa ikidaiwa mimi ni GAIDI ulijitoa na kuja kuwa wakili wangu bila kuombwa na hata hukuniomba senti. Wakati huo hukuwa katika "active politics".
Maisha yakaenda mbele, ukawa mwanachama wa JamiiForums kwa jina halisi (verified Tundu Lissu) na kuniambia unataka kuonesha support kwa huduma tunayoitoa.
Disemba 2016 nilipokamatwa kwa madai ya kutotoa 'ushirikiano' kwa vyombo vya dola, hukuniacha ukaja hata bila kuitwa. Ulinisisitiza "Max, tumetoka mbali hata kabla sijaingia kwenye siasa, leo unanikimbia? Sikuachi uumie, nitakutetea bure na hata kufunga safari toka Dodoma kila kesi yako itakapotajwa." Tukacheka na kutiana moyo!
View attachment 583487
Ni wiki mbili zilizopita tulipopiga picha hii, hapa ulikuwa unarekebisha kalenda yako kuhakikisha tarehe ya kesi yangu unakuwepo ili kuhakikisha sizamishwi na walionipania (na nakumbuka ulithubutu kuwaambia usoni mbele zangu).
Habari ya wewe kushambuliwa kwa risasi (ni wazi waliutaka uhai wako) imeniumiza sana, imenitia simanzi kuu na kunifanya nikose la kufanya zaidi ya kupata japo dakika kadhaa kukuombea (the best I could do).
I happen to know you Tundu, nje ya siasa wanazoona walio wengi! Mungu akusaidie upone haraka na kukurejeshea afya yako hata kuyaponya majeraha yako.
Mungu wetu ni mwingi wa huruma; kama amekuepusha na kifo leo - atakuponya!
Get well soon brother...
Tafakari. Lissu ni mwanasheria anaendesha kesi nyingi na kesi zina pande mbili. Wanaoshindwa wnaweza kutengeneza visasi. Tusikimbilie siasa tuangalie pia nature ya kazi yake.Lisu kafanya kosa gani hadi watake kumuua kama jambazi??
we ulishaona wapi mtu anashindwa kesi harafu unaenda kumuua wakili?Tafakari. Lissu ni mwanasheria anaendesha kesi nyingi na kesi zina pande mbili. Wanaoshindwa wnaweza kutengeneza visasi. Tusikimbilie siasa tuangalie pia nature ya kazi yake.
Sent using Jamii Forums mobile app