Maxence (baada ya ajali ya gari): Ahsante Mungu, ahsante watanzania!

Status
Not open for further replies.
Pole sana. ushauri wako kwa madereva/abiria ni sahihi na ya kuzingatiwa. mimi pia mkanda ulishaniokoa katika ajali mbaya.
 
Lakini hapo unaposema Mungu kakupeni second chance sijapaelewa vizuri.ina maana ndo mmeanza maisha upya kabisa?
 
Nimependa ushauri wako lakini zaidi hili lako ni ushuhuda mkubwa wa ukuu wa Mungu,ukimtegemea hawezi kukuacha. Ashukuriwe yeye aliye mtakatifu na mwenye haki na anayehukumu kwa haki!
 
Pole sana Mpwa, juzi ijumaa nilikua nasafiri kwa gari yangu kwenda Tanga, nadhani tulikua tunakaribia Mbwewe basi kwenye down moja nzuri nimeshuka na spidi zaidi au kama Mia moja hivi kwenda kuibuka Tu ni mpuuzi sijui ni basi gani but nakumbuka Lina za njano akawa Ana overtake gari ndogo.

Kila nikikumbuka nataka kulia maana ilikua tukavaane uso kwa uso. Nikafunga break na Yule mpuuzi akapita kwa bahati sana maana nshamuona alitaka aingie porini but akakomaa akajitahidi kurudi upande wake.

Mimi sasa ndio nikawa naenda kuigonga huku ubavuni karibia na mwisho. Ghafla tukawa tumepishana salama.

Thank you God it was horrible, pole Mpwa wangu
 
Dah! Pole sana mdau.....!
Tushukuru Mungu amekuponya, hata kama ilikuwa bahati mbaya mkuu tahadhari muhimu!!
Nchi imechafuka sana hii!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom