Mawifi inakuwaje? Kunakuwa na kutokuelewana na mke wa kaka yao

Wakikutana wanawake wajinga ni shida.

Hapo mmoja ni mjinga na sio wifi tu anaweza kuwa hata mkeo ndo mjinga
 
Mawifi wakishajua kama kaka amenasa na wameshindwa kupambana na mke wa kaka yao, shida sasa huangukia kwa kaka ,
utawasikia madada ...kalogwa..amekuloga huyo kwao washilikina sana... ...kaka amelishwa kitu sio kawaida yake... ,kaka unaosha vyombo na nguo huyo mkeo anafanya kazi gani ?? Yaani inakuwa ni balaa ,kiukweli nimesoma hii mada tokea page 1 hadi hii ,nazidi kuvurugika.

Inaweza ikawa mnazungumza na dada zako bila kutegemea ukasikia dongo linalushwa, undani sijaufahamu wananiona kama zezeta,sina akili ,sasa mapenzi kwa mke wangu wanataka yaweje ? Unawakuta hawana jibu zaidi utawasikia ,....nawe umezidi ..!
 
Duuh dada mtu anaingiaje chumba cha kaka yake na mkewe?😳😳 ajabu hii na uswahili kiwango cha lami
Sio anaingia mwenyewe ni ile mke wa kaka yao kujipendekeza kwao na kuona furaha anamkaribisha chumbani ili aone anavyotunza nyumba na usafi na mpangilio ni katika kujiweka karibu na kuonyesha upendo wa dhati kwa ndugu wa mume ,ila nalo hilo si ajabu likajenga shari ...umekiona chumba mavumbi kila kona sijui kaka anaishi vipi mle ndani ndio maana kila siku ana mafua.., Yaani we wacha tu , sasa najifanya na mimi hamnazo ,huwa na cheka na kuwaponda wote wawili ....wanawake ndivyo mlivyo.... ,basi akiondoka wifi inakuwa balaa jingine ,mke anaanza yake .....naona unamsapoti yule dadako ... ,inakuwa hata huelewi ni suali au ni mazungumzo.
 
Kuna wengine wanatenganisha familia kwakuwa na wivu wa kupitiliza na hawako tayari ndugu wapate mapenzi ya mumewe hata kama alikuwa anajua waliyapata!

Kuna wengine wanakwenda kwenye ndoa kwa lengo la kuwakomoa ndugu kwa hiyo hapo panakuwa hapatoshi!
Yaan nasemaje? Mimi ndo mama msaidizi, sina dhiki ila upendo wangu na wadogo zangu kima ajitokeze atajua vyema. Nami nikaenda miji ya watu nitakua na adabu hivyo2. Wanataka tuwapende kina nani kama sio uzao wa mama zetu.

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Nampenda sana wifi yangu mke wa kaka yangu. She is my best friend.
Umefanya nimkumbukuke wifi yangu anayetimiza miaka 5 leo tangu atutoke ghafla, alikuwa ni zaidi ya wifi yangu, kaka yangu alikuwa kama ndiye shemeji, ila upande wangu duu balaa
 
Yaan nasemaje? Mimi ndo mama msaidizi, sina dhiki ila upendo wangu na wadogo zangu kima ajitokeze atajua vyema. Nami nikaenda miji ya watu nitakua na adabu hivyo2. Wanataka tuwapende kina nani kama sio uzao wa mama zetu.

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
Kijana akioa kuna vitu huwa vinapungua hata kama hajashauriwa na mtu inakuwa automatically labda kama hajampenda kutoka moyoni.
 
Wapo ndugu yangu! Yaani hadi unajiuliza hawa watu,mbona wanakua hivi?? Dada mtu,anajua hadi boxer za kaka yake
Boxer ya kaka iliotoboka toboka kama chujio la nazi duu , uswahili huo! Hao wanaweza kuwa hata wote wanamirupo na inakuwa siri yao.
 
Dada wa wanaume wanasahau kuwa mwanaume akishaoa wao si kipaumbele tena, kipaumbele na jukumu lake ni kuhusu mkewe.

Wao inabaki kuwa msaada na msaada si lazima.
Hapo ndipo tatizo huwa linaanzia, wadada hutaka kaka aanze na wao, na hicho kitu hakiwezekani labda kwa mwanaume asiyejielewa mbulula wa malezi, nenda hata kwenye kufungishwa ndoa hawaambiwi uanaze na familia ya kwenu ila unaanza kwa mke/Mme .
 
Kijana akioa kuna vitu huwa vinapungua hata kama hajashauriwa na mtu inakuwa automatically labda kama hajampenda kutoka moyoni.
Sisi tunaingelea mambo ya familia mkuu. Wanasema ukienda Roma jifunze kuabudu kama wanavyoabudu. Mengine ni kuleta mashindano yasiyo na tija

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom