Mawazo ya kuibadilisha TANESCO

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
4,818
2,000
Kuhusu Bwawa la Nyerere: Ukweli ni kwamba Umeme wa Bwawa la Nyerere utatutosheleza lakini sio mwingi kiasi cha kuuza nje. Kuna umeme sasa umefika vijijini, joto la dunia linaongezeka, treni ya umeme, matumizi ya Air condition kuongezeka, viwanda vipya. Mfano viwanda vya chuma na cement vinatumia umeme sana.

TANESCO
  1. Utengenezaji wa umeme (Generation) ambapo umeme unaotokana na joto (Themal) kwa kutumia gas 63.36% na umeme wa maji 36.64%
  2. Usambazaji wa umeme
  3. Customer Service lakini wenyewe wanasema Distribution
Kwanza nisema kwanini kuna tatizo la umeme kwa sasa.

  1. Ukweli ni kwamba jitahada za kusambaza umeme nchi nzima hazijaendana na ongezeko la utengenezaji wa umeme.
  2. Kwenye kusambaza umeme vijijini umeme mwingi unapotea. Kwasasa 16% ya umeme wa Tanesco unapotea lakini hii asilimia inaongezeka zaidi umeme unavyozidi kusambazwa
Je, nina mawazo gani kuhusu kubadilisha hii kampuni?
  1. Tanesco iwe na wakurugenzi watatu wa kila idara na mmoja wa kampuni yote. Hivyo kila kitengo kiendeshwe kama kampuni. Hii inasadia kujua ni sehemu ganio hasa ina yumba na inahitaji msaada mfano kuna fungu maalamu kwenye malipo ya bill za umeme abayo ni usambazaji tu. Hivyo usambazaji wa umeme ukiwa kama kampuni tutajua kwa undani kama pesa zinatosha au bunge litafute njia nyingine ya kuongeza pesa. Lakini kama kweli tupo 80% ya vijiji au zaidi basi gharama zinatakiwa zianze kupungua baada ya muda maana kusambaza ni mara moja na baada ya hapo ni kutengeneza maharibiko madogomadogo kwa pesa ambayo itaongezeka na wateja wapya. Hiyo ingekuwa kampuni inajitegemea ingeweza hata kukupa maana unamwekea mtu umeme halafu gharama zinarudi polepole lakini mwanzo kuna pesa zinahitajika nyingi zaidi.
  2. Ukweli ni kwamba umeme wetu ni wa gas 63.36%. Wasiwasi wangu ni kwamba serikali inawezekana kabisa inanunua umeme huu kwa bei ya kimataifa ingawa gas hii inatoka Tanzania. Hii ni kwasababu wauza gas ni songas, TPDC na makapuni mengine ya nje lakini kuna gharama za pipeline ziko hapo. Bwawa na maji tunalojenga litasaidia sana kwenye hili. Lakini vilevile serikali inatakiwa itumie njia ya hedge ambayo unanunua gas nyingi wakati bei ipo chini halafu unaomba hiyo gas iletwe baadae
  3. Manunuzi yote ya umeme yahamie kwenye mitandao na kutumia simu. Hii itapunguza gharama za madalali na utengenezaji wa kadi za namba kwa Tanesco bila kupunguza kipato
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom