Mawaziri wapimwe kwa kuleta sera mpya au kuhuisha sera

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Nipende kutoa wito, maoni na ushauri adhimu na wa kipekee.

Kama nchi lazima tubuni mikakati mipya ya kukabiliana na maadui watatu muhimu waliotajwa hapo awali yaani umasikini, ujinga na maradhi.

Bado kama Taifa hatujafikia kiwango tulichohitaji kufikia katika kukabiliana na maadui tajwa. Hivyo bado sera, katiba, miongozo na mipango yetu inaendelea kulenga maadui hao watatu.

Dunia imeenda kasi sana na Tanzania imejaribu kukimbizana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia, kitamaduni na kiuchumi, hata hivyo ukichambua bado tunahitaji kama taifa kuendelea kusimamia misingi ya malengo tuliyojiwekea kama Taifa wakati tunapata uhuru.

Observation
Bado tuna watu walioprofile/waliopata vyeo ambao hawajatenda ilivyopaswa hususani katika ngazi ya kisera, kimkakati, kimipango na kiutekelezaji.

Leo najikita kwenye ngazi ya juu yaani Uwaziri
Uwaziri sio jambo dogo, Uwaziri ni Sera mujarabu zinazotakiwa kutuvusha kutoka hatua moja hadi nyingine ndani ya muda mfupi na mrefu.

Mawaziri wetu
Wengi wa Mawaziri wetu hawatambui kwanini wamepewa fursa hiyo kutuvusha, wengi wao wanadhani uchawa na kusifu kwao ndio role yao. Wengi wao wanadhani wapo hapo kusimamia na kumantain status quo.

Leo niwaase kuwa mawaziri wana kazi kubwa sana inayotakiwa kufanyika, kupimwa na kukumbukwa, yaani kubadili namna ya fikra, perception, utendaji n.k, watoto wa pwani tunasema lazima waziri ajue namna ya kutweka (kuelekeza jahazi kwenye uelekeo fulani).

Hapo nyuma kabla ya Magufuli, mawaziri wetu walikuwa ni wazee wa copy and paste, yaani kila upuuzi ulioamuliwa kwenye conference fulani wao wanauleta nchini.

Kipindi cha mzee baba JPM Mawaziri walijikita kwenye u-manager, yaani hili halijafanyika basi inabidi lifanyike, waliiga style bila kipaji.

Nishauri; sasa ni nyakati mpya, ni nyakati za ubunifu na ni nyakati za ku-take risk. Hii inamaanisha kuwa tuje na sera mbadala, tuzipeleke bungeni, tuwaelimishe wabunge na tuzifanyie utekelezaji.

Kamwe, kipimo cha waziri kisiwe ni kutumbua bali ni kwa sera ipi mpya anayokujanayo kuimarisha sekta fulani.

kwa leo ni hayo tu.

Kwa hisani ya mtu wa Tanzania.
 
Huu Uzi, ni Uzi Bora sana

Ukweli ni kwamba Tuna mawaziri ambao kwao Raha ni Ile wanavyopigiwa saluti , magari na misafara , yaan Waziri anafeel proud tu kuonekana ni "Waziri".


Ukiwauliza, wao wanasema Sisi ni wasimamiz8 Yu wa sera !!.

Hili pia linaweza kua ni kweli, Mwenye tatizo ni yule anayechagua mtu alisema Sheria, kwenda kua Waziri wa Afya.

Alafu hapohapo anachagua Alisomea Uchumi kwenda kua Waziri wa Uchumi .


Hapohapo anamchagua Makambaz kwenda kua Waziri wa Nishati , Sasa Makamba bichwa lake lenye upaa, na Nishati wapi na wapi?.




Matokeo yake, wanakaa kwenye Wizara ,huoni mambo mapya, hawana ubunifu kabisaaaa .


Ifike Mahali, Wizara Husika, kuanzia Waziri wake mpaka naibu katibu, na watendaji wake, wawe ni watu wenye taaluma inayohusian na Wizara hiyohiyo.


Natumia sana , mtu kasoma Arts anaenda kuongoza Wizara ya Afya??? Kwann asidanganywe ?. Chagua mtu ambaye angalau hata aliwah kukesha Hosp usiku na mchana akipambana na Wagonjwa !!.
 
Jingalao akili zimeanza kukurudia, badilisha jina sasa.
 
Kwa Tanzania wanapimwa kwa idadi ya Safari za kushitukiza walizo fanya waliwa na Ma Camera
 
Back
Top Bottom