..Mawaziri saba watoswa.....

Njaa tu zinakusumbua! By the way, kwenye picha hii ya vibaka wenzako wa buku 7 uko wapi?

attachment.php

Hii Kali,buku 7 at work!!
 
Hata hii Mkuu wanatudanganya tu!

JK hawezi mtosa Dr Kawamba na Adam Malima!

Nape anajifurahisha tu
Hizi ni siasa za NAPE za maji taka. Katika utawala, CCM ina uwezo wa kuwaita na kuwaonya au kuwatimua. Hii ni Cheap popularity ya NAPE na Boss wake. Mwenyekiti wa CC ni Rais. Sasa ona hii ni nini kama si kujiangusha? Hivi hujui kuwa Rais anateua mawaziri kumsaidia kiserikali na anateua secretariat ya CCM ili imsaidie kichama? Hivi na mawaziri wakiamua kukagua uhai wa wizara zao nao wakasema Kinana na Nape watoswe? Tuache hizo, hii ni kazi ya CDM kuisema serikali ya CCM na wala si sec ya CCM kuisema hadharani serikali yao.
 
Nape tena. Hachoki kuimba nyimbo zisizo na kiitikio? Hivi kamati kuu yao huyo Jakaya hakuwepo kwenye hicho kikao hata wajaribu kutudanganya? Hatujasahau wimbo wao wa kujivua gamba. Kichekesho ni kuwa hata yule aliyeamua kujitoa walikwenda mbio kumramba miguu wakimsihi asimalizie kujivua gamba.
Wanacoweza kfanya CCM ni kuwatetea wale majagili na wasirika wo wakuu ambao ni sehemu muhimu ya vigogo wake.
Eti hawajamwambia awaodoe ila wameshauri tu!!! aibu kwao. Kazi hiyo inawezekna na CDM tu ambao hawawezi kuuma maneno. Poleni CCM na nawatakia mandalizi mema kuwa chama cha upinzani kuanz 2015. kama tume haitawabeba.
teh teh...
 
CC kama wanaona mbali wangegundua matatizo yote hayo ni Mh. Kikwete.
Kama cc ya ccm ina ubavu wamtose Kikwete kukinusuru chama
 
wale wahu wako wapi kwenye huu uzi?! Sixgate, Faiza etc. Wako wapi, waje wakatae au wakubali!! Mijitu mingine bure kabisa!
 
...

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kuwatosa mawaziri saba wanaotajwa kuwa ni mizigo kwa serikali inayoongozwa na chama hicho.

Hatua hiyo ya kuwatosa mawaziri hao waliohojiwa na Kamati Kuu (CC), iliyokutana juzi mkoani Dodoma, inalenga kukinusuru chama katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwaka 2015.
Mawaziri waliowekwa kwenye kikaango cha kung’olewa ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza; Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa; Waziri wa Utumishi, Celina Kombani na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia.



Wengine ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda; Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo na Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.



Tanzania Daima Jumapili, imedokezwa kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho wamekuwa wakitaka mawaziri wanaofanya vibaya kwenye wizara zao wawajibishwe kila mara ili kuiepusha serikali kuchukiwa na wananchi.

Inadaiwa wanataka utaratibu uliokuwa ukifanywa miaka ya nyuma na chama chini ya utawala wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere wa kuwaita mawaziri na kuwahoji kwenye vikao vya chama urejewe.



Hoja kubwa wanayoijenga ni kuwa chama ndicho kinachopata wakati mgumu katika chaguzi kwa sababu ya watendaji au mawaziri kutowajibika ipasavyo.


Inaelezwa kwa muda mrefu kumekuwa na mipango ya kuwaondoa mawaziri hao, lakini mazingira ya kuwaondoa ndiyo yamekuwa yakikosekana. Lakini hivi sasa mkakati umeshaiva.
Inadaiwa ziara za kuimarisha chama zilizofanywa na viongozi wa CCM katika mikoa ya Ruvuma, Mbeya, Njombe na Mtwara ndizo zimetumika kuandaa mashtaka ya mawa
 
Tusubiri kama watatoswa kweli. Ajabu ni kuwa sioni wengine watakaoteuliwa wanaoweza kufanya tofauti na hawa wa sasa.
 
Angalia hii kutoka Gazeti la Mwananchi....."Kwa mfano Waziri husika hajafika kwa muda wa miaka minne na nusu mkoani Ruvuma ambako ndiko kuna ghala la chakula na tulipofika Tunduma tulikuta foleni pale mizani huku watumishi wakiwa wanafanya kazi kwa saa tisa, lakini baada ya kueleza udhaifu huo sasa wanafanya kwa saa 24,"

Hivi waziri lazima afike kila sehemu?
 
Hata hii Mkuu wanatudanganya tu!

JK hawezi mtosa Dr Kawamba na Adam Malima!

Nape anajifurahisha tu
Yaani hasa huyo Shukuru jmn, huyo anatakiwa aondolewe haraka kunusuru sekta ya elimu na Mulugo afuatie!
 
Hii cc ya maccm wangekuwa wana akili wangeanza na mwenyekiti wao maana yeye ndio alikuwa anaahidi ahidi tu hovyo hovyo. Mara kigoma kuwa dubai ya africa (tumuulize vipi?) meli mpya kureplace ilozama ziwa victoria 1999 iko wapi?? Barabara kuzunguka mlima k'njaro zi wapi?? Barabara ya arusha-mkalama-iramba i wapi??
Huyu alikuwa awe wa kwanza kuondolewa.
 
Comedy nyingine nzuri sana, Kikwete ndio Mwenyekiti WA CC halafu CC inamshauri Rais awachukulie hatua aliowateua!!!!!!
 
Baada ya hapo nimesikia vibaka wa buku 7 Lumumba wanajiandaa kuja na threads nyingi kwamba CCM ni mfano wa kuigwa kwa kufanya maamzi magumu. Hebu watazame jinsi wanavyojipanga kuleta umbeya!!
attachment.php

Mkuu Hiroshima,

Hii Picha na comment zake imenichekesha sana...Kumbe ndio maana upuuzi umekuwa mwingi hapa JF.
 
Kale Kachanga Ka Mkulima Lazima Katolewe Kwanza, Haiwezekani Baraza Lifeli Mara Mbili Chini Yake, Yeye Anashinda GAMBUSHI!
 
Raisi mwenyewe ndio mzigo namba 1.Hivi yeye huwa haoni uzembe wa mawaziri wake mpaka bunge au kamati kuu ya chama imshinikize?!

Hivi hata utekelezaji wa maazimio ya bunge tatizo ni mawaziri peke yao bila JK kuhusika?

Haya ndio madhara ya Raisi kutwa kupiga misele badala ya kuangalia nchi inakwendaje

Raisi ukingojea kuletewa taarifa tu, ujue kazi itakushinda.

Huu ndiyo ukweli, kikwete ndiyo zigo la kutupwa. Katika familia kama watoto wameoza ujue ni uvundo wa baba unawaathili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom