..Mawaziri saba watoswa.....

..Mawaziri saba watoswa.....

Sitaki kuamini kuwa JK ataenda against chama ambacho yeye ni mwenyekiti wake: In fact CCM wakifeli ktk mpango huu walionzisha, wakuwapiga chini mawaziri mizigo, watazidi kupoteza imani kwa watanzania. Huyu kawambwa cjui ana ushawishi gani kwa Mr. President au ni swahiba tuu?[/QUOTE Mkuu CHADEMA itabaki kuwa baba lao, Ccm hawawezi kumfukuza hata mjumbe wa nyumba kumi.
 
Matatizo ya CCM na serikali yake si matatizo ya mtu mmoja mmoja.Hata Lowassa alionewa tu kwani tangu aondolewe na kuwekwa Pinda kuna nini kimebadilika?Halafu Nape ana ugomvi gani na Chiza?Kwenda kutembelea Ruvuma ukiwa huna pesa wala majibu kwa matatizo ya wakulima itasaidia nini?Wao wote ni CCM kwa nini wasiitane na kuhojiana badala ya kupanda majukwaani na kupakana matope?Ukichunguza hapa utagundua wizara kama ya kilimo ni wizara za kiutendaji zaidi sasa serikali isipoinject pesa za kutosha huko ni lazima waziri aonekane "mvaa tai".Na hata hawa akina engeneer Chiza ni watu ambao historically ni watendaji kuliko wanasiasa.Usipowawezesha kufanya kazi zao hautawasikia kwenye porojo za kisiasa watakaa kimya tofauti na akina Wassira.Hivi ni watu wangapi wamepita pale kilimo?wamefanya nini tofauti na Chiza?wangapi wamepita pale elimu?wamefanya nini tofauti na Kawambwa?Nape kabla hujawavaa mawaziri,mwambie tu na aliyewateua kuwa yeye pia na chama chake ni mzigo mzito kwa taifa na hata hao mawaziri chama chao na ukiritimba wake ni mzigo mzito kwao!wanaogopa kusema tu ngoja tuwasaidie!kwa hiyo kama kujiuzulu ulipaswa kuanza wewe,na Kinana na mwenyekiti wenu!acha unafiki na sifa za kijinga.Msifikiri watanzania bado ni wale wale unaoweza kuwapulizia maskioni wakaanza kucheka kwa starehe ya kupuliziwa maskio huku ukiingiza vidole kwenye mifuko yao uwaibie no!no!no!matatizo ya serikali hii ni collective responsibility ya CCM.Anza wewe Nape kujiuzulu.
 
Kitu kinachonifanya niwachukie wabunge kuwa mawaziri ni kwamba,wabunge wetu wote ni wanasiasa,"much talkative"less action,wengi wapo hapo muda mrefu wakila vinono,si rahisi kufahamu changamoto zilizopo mezani kwa sasa,infact wamelewa sifa na fedha"


Mengine yanabaki kuwa maneno ya kupeana matumaini hewa!!!!!
Hapa ndipo penye shida; mawaziri hawatakiwi kuwa wabunge wala kuwa na uhusiano karibu na vyama
 
Baada ya hapo nimesikia vibaka wa buku 7 Lumumba wanajiandaa kuja na threads nyingi kwamba CCM ni mfano wa kuigwa kwa kufanya maamzi magumu. Hebu watazame jinsi wanavyojipanga kuleta umbeya!!
attachment.php
Hahaaa nimecheka sana, namuona Simiyu yetu kavua shati pale...
 
sasa huu umekuwa mchezo wa kuigiza yaani kila kukicha baraza la mawaziri linararuliwa na kuunda jipya sasa hii tafsiri yake nini, ina maana hapo ile sera ya chama kwanza mtu baadae ndo madhara yake haya sasa
 
Hv kuna waliobaki ccm wanafaa kuwa mawaziri..!? Kwa waliobaki hata profesa majimarefu ataukwaa uwaziri. Kwa muda mfupi karibu wabunge wote wasomi ndani ya ccm wamejaribiwa kuwa mawaziri.
 
Hivi baraza la Mawaziri wanafanya vikao mara ngapi kwa mwaka, mwezi au week? Na je katika vikao hivyo huwa mawaziri au makatibu wakuu huwa wanatoa taarifa za utendaji wa wizara zao? Na je JK huwa analizika na taarifa hizo?
Tatizo kubwa hapa ni JK ndo wakuajibishwa wa kwanza kama CC muna ubavu. Baba kiguu na njia kila Siku hata hajui maendeleo ya watoto wake shuleni (mawaziri)
 
ukiona mtoto wa jirani amekutukana ujue si bure ametumwa na mzazi wake. Nape amepata wapi ujasiri wa kumsema Kawambwa tena wazi wazi? Hili nalo ni picha jingine nataka kuona mwisho wake, je JK ataweza kuwatosa watoto wa kwao? Na je kama waliokuwepo wote akili zao zimedumaa, nani ataweza kuziba mapengo hayo yaliyojitokeza?
 
Haya sasa Jk anakaribishwa kuzungumza msibani, ngoja tuone hapa.......
 
Wana majembe kibao, Mfn. Komba, Nkamia na wengine wengi.
Kuna hatari ya kuingiza "mawaziri wapya wabovu zaidi ya waliokuwepo!"who shall suit,for the post among ccm MPs?mapito yatakuwa mlemle,na walewale,president JK mtihani mgumu huu,my "opinion"wenye rekodi za utendaji bora tutawapata kule alipotokea PROF.SOSPETER MULONGO
 
Unahisi? Mbona chadema kumtimua zzk kwenu ni tatizo vip kwa ccm kufukuza inakuwa uwajibikaji? Achen propanga na upotoshaji pale chadema inapowajibisha wazembe na wanaokiuka taratibu.

Chadema wakifanya haram! Yaleyale yakifanywa na ccm halali ni kweli huwa mnafikiri vema kabla ya kuponda, kukashifu kwa cdm na kusifia na kuhalalisha yaleyale kwa ccm? Kuweni wazalendo badala ya kutumika ovyo kuwapigia debe mafisadi Taifa likiteketea.

Sababu za kuwajibishwa ziambatane na ushahidi wa wazi.
 
...

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kuwatosa mawaziri saba wanaotajwa kuwa ni mizigo kwa serikali inayoongozwa na chama hicho.

Hatua hiyo ya kuwatosa mawaziri hao waliohojiwa na Kamati Kuu (CC), iliyokutana juzi mkoani Dodoma, inalenga kukinusuru chama katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwaka 2015.
Mawaziri waliowekwa kwenye kikaango cha kung’olewa ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza; Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa; Waziri wa Utumishi, Celina Kombani na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia.



Wengine ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda; Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo na Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.



Tanzania Daima Jumapili, imedokezwa kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho wamekuwa wakitaka mawaziri wanaofanya vibaya kwenye wizara zao wawajibishwe kila mara ili kuiepusha serikali kuchukiwa na wananchi.

Inadaiwa wanataka utaratibu uliokuwa ukifanywa miaka ya nyuma na chama chini ya utawala wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere wa kuwaita mawaziri na kuwahoji kwenye vikao vya chama urejewe.



Hoja kubwa wanayoijenga ni kuwa chama ndicho kinachopata wakati mgumu katika chaguzi kwa sababu ya watendaji au mawaziri kutowajibika ipasavyo.


Inaelezwa kwa muda mrefu kumekuwa na mipango ya kuwaondoa mawaziri hao, lakini mazingira ya kuwaondoa ndiyo yamekuwa yakikosekana. Lakini hivi sasa mkakati umeshaiva.
Inadaiwa ziara za kuimarisha chama zilizofanywa na viongozi wa CCM katika mikoa ya Ruvuma, Mbeya, Njombe na Mtwara ndizo zimetumika kuandaa mashtaka ya mawaziri hao ambayo waliyajibu walipoitwa kujitetea.
Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa licha ya utetezi huo, Kamati Kuu imemtaka Rais Jakaya Kikwete apime hoja zilizotolewa na wajumbe wa CC kama mawaziri hao wanafaa kuendelea na nyadhifa zao.



Uamuzi wa CC



Kikao cha CC kilichoketi juzi, kimemtupia mzigo wa kuwang’oa mawaziri Rais Kikwete ambaye ndiye aliyewateua.

Akizungumza na waandishi wa habari, jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema CC imetoa mapendekezo kwa Rais Kikwete ambaye ndiye mwenye hatima ya mawaziri hao.



Alisema Rais Kikwete ni mamlaka ya uteuzi wa mawaziri na ndiye atakayeamua kuwaadabisha, kuwasukuma au kuwaondoa madarakani mawaziri mizigo.



“Aliyewaweka ndiye atakayewaondoa, Kamati Kuu haijamwabia awaondoe, inachokifanya ni kushauri tu. Lakini madaraka yote anayo rais aliyewachagua.


“Kwa mfano Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika hajafika kwa muda wa miaka minne na nusu mkoani Ruvuma ambako ndiko kuna ghala la chakula…, tulipofika Tunduma tulikuta foleni pale mizani eti watumishi wanafanya kazi kwa saa 9, lakini sasa wamebadilisha utaratibu huo wanafanya kwa saa 24 baada ya sisi kwenda,” alisema.


Nape akiwa katika ziara ya siku 26 mikoa mbalimbali, aliwataja mawaziri hao ambao wamekuwa mizigo katika serikali ya Rais Kikwete na kumtaka awatimue.



Hata hivyo Waziri Chiza na Kawambwa walisema kuwa hawafanyi kazi kupitia majukwaa ya siasa na wanasubiri kuitwa na Kamati Kuu, ili waieleze wanavyofanya kazi.


Waziri Kawambwa, alijinasibu kwa kujifafanisha na mti wenye matunda ambao hauishi kupigwa mawe kila kukicha.
Waziri Chiza alimtaka Nape aache kukimbilia kuzungumza hadharani juu ya madai ya wakulima wa korosho na badala yake atafute sababu ya wakulima hao kutolipwa na serikali.
Mabadiliko ya mawaziri
Kama Rais Kikwete ataamua kulifanyia mabadiliko Baraza la Mawaziri itakuwa ni mara ya tatu, ambapo mwaka 2008, alilivunja kutokana na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kujiuzulu kuguswa na kashfa ya kuipa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura Kampuni ya Richmond.

Mabadiliko mengine aliyafanya Mei mwaka jana baada ya wabunge na wadau mbalimbali kushinikiza kuondolewa kwa mawaziri waliodaiwa kutowajibika ipasavyo.



Maagizo mengine ya CC



Kamati Kuu pia imeiagiza serikali iangalie upya upatikanaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima wa pamba nchini.
“Chama kimeiagiza serikali kutowalazimisha wakulima kutumia mbegu ya Quiton badala yake elimu itumike zaidi badala ya nguvu,” alisema Nape.



Aliongeza kuwa CC imeitaka serikali kuangalia upya urasimu katika uwekezaji wa viwanda nchini hasa vinavyoongeza thamani ya mazao na kutoa ajira nchini.



Nape aliongeza kuwa kuhusu kilimo cha mkataba kwa wakulima wa pamba, serikali imetakiwa kuratibu utaratibu wake ikiwemo kutowalazimisha.


Kuhusu wakulima wa korosho, alisema kuwa kamati hiyo imeisisitiza serikali kujipanga kutatua tatizo la korosho na kuhakikisha inabanguliwa nchini.


“Serikali inatakiwa kuangalia upya orodha ndefu ya makato kwa wakulima, hasa wa korosho na vyama vya msingi au mamlaka zinginezo ili kuondoa makato yasiyo ya lazima na kuongeza kipato cha mkulima.


“Kuhusu pembejeo za ruzuku Kamati Kuu imepokea taarifa ya malalamiko ya wakulima juu ya ufanyaji kazi wa mbolea ya Minjingu na kuagiza wananchi wawe huru kutumia mbolea wanayoitaka badala ya kulazimishwa,” alisema.


Kwa upande wa wakulima wa mahindi, Nape alisema kuwa serikali imetakiwa kumalizia malipo yaliyobaki na kuhakikisha wanakomesha utaratibu wa kuwakopa wananchi mazao yao bila kuwalipa.


“Utaratibu uwekwe wa kufanya tathimini mapema ya mahitaji na uwezo wa kununua mahindi wa serikali ili kuepusha utaratibu wa kuchukua mahindi ya wakulima bila kuwalipa,” alisema.


Nape alisema kwa upande wa madai ya walimu, CC imeiagiza serikali kukamilisha uhakiki wa madai hayo na kuwalipa haki zao ikiwemo kuhakikisha madeni hayazaliwi tena.


Kamati hiyo pia imekemea watendaji wachache wanaojihusisha na ubadhirifu kwenye halmashauri mbalimbali nchini.



“Serikali imeshauriwa kuangalia upya sheria kama zinakidhi mahitaji ya wakati na mazingira ya sasa ili kuongeza uwezo wa udhibiti na kuokoa pesa za walipakodi zinazopotea kwa walafi wachache kwenye halmashauri mbalimbali nchini,” alisema Nape.

Source: Tanzania Daima

Note: CCM wameshaona hali ni mbaya AHADI Hazitekeleziki cc maisha bora ...kigoma kuwa Dubai


- Kichwa cha habari na habari yenyewe ni vitu viwili tofauti na ndilo gazeti kuu la wenzetu huko upande wa pili, vipi Kapuya viliishia wapi?

Le Mutuz
 
Hapa hakuna kitakachofanyika, hiyo ndiyo imetoka tena. Unaposema Chama cha Mapinduzi kinatoa maagizo ya utekelezaji kwa serikali una maana gani wakati boss wa chama ndiye huyo huyo boss wa serikali. Kwa tafsiri rahisi ni kwamba Mwenyekiti wa CCM Mh. Jakaya kikwete anatoa maagizo ya utekelezaji kwa serikali inayoongozwa na Mh. Jalaya Kikwete it doesn't make sense. CCM na Serikali ni taasisi mbili tofauti na lazima ziongozwe na watu wawili tofauti ili kuwe na uwajibikaji na kwamba ikiwezekana Mwenyekiti wa chama amuwajibishe Rais wa nchi. Nchi hii ndivyo ilivyo unaweza kukuta Mwenyekiti wa shirika fulani ndiye huyo huyo mtendaji mkuu wa shirika hilo hilo, uwajibikaji uko wapi na nani ana wajibika kwa nani. Majanga.
 
Back
Top Bottom