..Mawaziri saba watoswa.....

..Mawaziri saba watoswa.....

Baada ya hapo nimesikia vibaka wa buku 7 Lumumba wanajiandaa kuja na threads nyingi kwamba CCM ni mfano wa kuigwa kwa kufanya maamzi mazito. Hebu watazame jinsi wanavyojipanga kuleta umbeya!!
attachment.php

...njaa tu hawa ingekukwa enzi za nguvu kazi bababake njembe lingewahusu!!!
 
Baada ya hapo nimesikia vibaka wa buku 7 Lumumba wanajiandaa kuja na threads nyingi kwamba CCM ni mfano wa kuigwa kwa kufanya maamzi magumu. Hebu watazame jinsi wanavyojipanga kuleta umbeya!!
attachment.php

umenichekesha sana, hawa ndo akina simiyu yetu, marcopolo, infweero et al? nimecheka kweli, nasikiaga tu buku7 kumbe ndo wanafanya kazi ivi? loh

kweli ccm imekwisha reality ndo kitu muhimu kuliko hawa waliojipanga kuwahadaa watanzania. dah ccm anakimbizwa mpaka basi
 

...

jomba tangia aanze kupiga sub zote zimeoza juu mpaka chini maparachichi tu!!!

.....
olo lyobhoya elentwe pyee .....
Kitu kinachonifanya niwachukie wabunge kuwa mawaziri ni kwamba,wabunge wetu wote ni wanasiasa,"much talkative"less action,wengi wapo hapo muda mrefu wakila vinono,si rahisi kufahamu changamoto zilizopo mezani kwa sasa,infact wamelewa sifa na fedha"
 
Safi sana ccm, napendekeza Prof. Maji marefu apewe wizara ya elimu, Lusinde Viwanda, mch. Lwakatare Uvuvi, kapuya kilimo.
 
Mamlaka ya uteuzi inafanya kazi kwa kuogopa au kuona aibu kuwaudhi wateuliwa. Chama kinatumika kuweza kuondoa wale mamlaka inaona haiwataki.
 
Huu ni wakati wa Zitto kuhama na kupewa Wizara. Safi sana Nape. Napendekeza Kitila apewe nafasi ya Kawambwa.
 
Heading haiendani kabisa na maelezo.

Mods mshughulikieni mleta mada kwa uzushi

cc

mods wote - invisible, paw. Fang, melo
 
Safi sana ccm, napendekeza Prof. Maji marefu apewe wizara ya elimu, Lusinde Viwanda, mch. Lwakatare Uvuvi, kapuya kilimo.
Mariam msabaha apewe nafasi ya zitto halafu lema achukue ya said arf
 
Source ni tz daima? Gazeti la mbowe????? Linalomtumikia mbowe kwa hisani ya mtei...taarifa ya kutunga hii
 
Dk. Slaa: Tukishika dola tutaruhusu utengenezaji pombe ya gongo


Saturday, 14 December 2013 · Posted in OMG, Siasa


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.


"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.


Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.


Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.


Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.


"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.
CHANZO: NIPASHE
 
Source ni tz daima? Gazeti la mbowe????? Linalomtumikia mbowe kwa hisani ya mtei...taarifa ya kutunga hii
Njaa tu zinakusumbua! By the way, kwenye picha hii ya vibaka wenzako wa buku 7 uko wapi?

attachment.php
 
Kwa mara ya kwanza niwapongeze ccm kwa hili, ni wajibu wao ambao walikuwa wakiukwepa siku nyingi, ccm itachukiwa na wananchi kama mawaziri na watendaji wengi serikalini watashindana kwa kula posho badala ya kutoa utumishi uliotukuka kwa wananchi, mawaziri wengi wamepewa nafasi zao kama zawadi, hawana wanachoweza zaidi ya kuuza sura tu, mfano kina mulugo,kawambwa, sofia simba,Adamu malima, hawa ghasia, kristofa chiza, na wengineo. Lakini bado napata shida kwenye kuwapata mawaziri wazuri zaidi ya hawa, maana wabunge wengi ni wabovu, na wengi walishinda kwa kutoa milungula wakati wa uchaguzi! Pia namhurumia sana rais kikwete katika hili!
 
Hapo changa la macho hafukuzwi mtu. Mtakuja kuniambia. Undugunaizesheni umejaa sana serikali ya CCM. Eg Anna Mkapa na Sumaye,Kikwete na Membe(mtu na ndugu. Chukua picha ya Kikwete na Membe ziweke hivi na hivi fananisha)Kikwete na Kalambwa,mama Salma na Ritz1. CCM haiwezi maamuzi magumu. Kama watawafukuza watawapa tuwizara tungine. Akitaka ufanisi wizara ya afya wampe mheshimiwa MziziMkavu. Pia Rais wa angani anawezaje kujua matatizo ya wananchi? Jamani wangenipa angalau na mimi nilete mabadiliko.
 
...

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kuwatosa mawaziri saba wanaotajwa kuwa ni mizigo kwa serikali inayoongozwa na chama hicho.

Hatua hiyo ya kuwatosa mawaziri hao waliohojiwa na Kamati Kuu (CC), iliyokutana juzi mkoani Dodoma, inalenga kukinusuru chama katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwaka 2015.

Kikao cha CC kilichoketi juzi, kimemtupia mzigo wa kuwang’oa mawaziri Rais Kikwete ambaye ndiye aliyewateua.

Akizungumza na waandishi wa habari, jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema CC imetoa mapendekezo kwa Rais Kikwete ambaye ndiye mwenye hatima ya mawaziri hao.
Alisema Rais Kikwete ni mamlaka ya uteuzi wa mawaziri na ndiye atakayeamua kuwaadabisha, kuwasukuma au kuwaondoa madarakani mawaziri mizigo.
“Aliyewaweka ndiye atakayewaondoa, Kamati Kuu haijamwabia awaondoe, inachokifanya ni kushauri tu. Lakini madaraka yote anayo rais aliyewachagua,” alisema Nape.
Nape tena. Hachoki kuimba nyimbo zisizo na kiitikio? Hivi kamati kuu yao huyo Jakaya hakuwepo kwenye hicho kikao hata wajaribu kutudanganya? Hatujasahau wimbo wao wa kujivua gamba. Kichekesho ni kuwa hata yule aliyeamua kujitoa walikwenda mbio kumramba miguu wakimsihi asimalizie kujivua gamba.
Wanacoweza kfanya CCM ni kuwatetea wale majagili na wasirika wo wakuu ambao ni sehemu muhimu ya vigogo wake.
Eti hawajamwambia awaodoe ila wameshauri tu!!! aibu kwao. Kazi hiyo inawezekna na CDM tu ambao hawawezi kuuma maneno. Poleni CCM na nawatakia mandalizi mema kuwa chama cha upinzani kuanz 2015. kama tume haitawabeba.
 
Back
Top Bottom