..Mawaziri saba watoswa.....

..Mawaziri saba watoswa.....

Nape Ana Nifurahishaga Sana Namfananishaga Na Yule Alo Kuwa Akimpigia Kerere Mwalimu SERIKALIII YOTE YA TANZANIA IMO MFUKONI MWANGU!
 
Nape Bwana Porojo Nyiiingi Kaingia Mikoani Kakuta Sifuri!
 
Hapo juu kuna mahali Nape kasema wamekuta foleni mizani Tunduma,Nafikiri wamekosea sio mizani inayosababisha ni kule boda km 10 kutoka mzani wa Magufuri,Hawa TRA walikuwa wanaringa sana unawakuta wafanyakazi muda wa kazi wapoVALENTINE BAR wanakunywa pombe foleni inakaribia kwa PANONE,Wakitoka hapo saa tisa jioni hakuna kuvuka,Mwakyembe alipokuja akawasha moto kwann wao wa lale wkt bandarini hawalali?Wakasema tatizo si wao ni wenzao wa Zambia kwa hiyo wakaenda kuongea nao wakakubaliana tar 1dec wakaanza kufanyakazi masaa 24.Nlichotaka kukanusha kauli ya Nape kwamba kazi inafanyika baada ya wao kwenda,si kweli ilikuwa ishawekwa kwenye mipango.Kwani Nape na Kinana ni nani mpk Zambia Revenue Authority iwaogope?Hata wasingekuja Tunduma bado makubaliano yangetekelezwa tu kati ya TRA na ZRA kwani walisha kubaliana.Msijikweze nyie
 
Najua huyo jk hawez fanya uamuz wowote wa kuwaondoa hao mawaziri! Shit
 
Hivi mama Prof.Tibaijuka amefanya nini au ni waziri kwa ajiri ya kigamboni tu!
 
Samaki mmoja akioza, wote wameoza!Serikali nzima iwajibike na sio mawaziri wachahe tu.
 
Pole sana kama unafikiri kuna jipya! Kwani hao si wamepatikana baada ya kuvunjwa baraza la mawaziri! Kinacho takiwa kuvunjwa ni chama.
 
...

Chama cha mapinduzi (ccm) kimeamua kuwatosa mawaziri saba wanaotajwa kuwa ni mizigo kwa serikali inayoongozwa na chama hicho.

hatua hiyo ya kuwatosa mawaziri hao waliohojiwa na kamati kuu (cc), iliyokutana juzi mkoani dodoma, inalenga kukinusuru chama katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwaka 2015.
mawaziri waliowekwa kwenye kikaango cha kung’olewa ni waziri wa kilimo, chakula na ushirika, christopher chiza; waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, shukuru kawambwa; waziri wa utumishi, celina kombani na waziri wa tawala za mikoa na serikali za mitaa (tamisemi), hawa ghasia.



wengine ni waziri wa viwanda na biashara, abdallah kigoda; waziri wa mifugo na uvuvi, mathayo david mathayo na naibu waziri wa fedha, saada mkuya.



tanzania daima jumapili, imedokezwa kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho wamekuwa wakitaka mawaziri wanaofanya vibaya kwenye wizara zao wawajibishwe kila mara ili kuiepusha serikali kuchukiwa na wananchi.

inadaiwa wanataka utaratibu uliokuwa ukifanywa miaka ya nyuma na chama chini ya utawala wa baba wa taifa, hayati mwalimu julius nyerere wa kuwaita mawaziri na kuwahoji kwenye vikao vya chama urejewe.



hoja kubwa wanayoijenga ni kuwa chama ndicho kinachopata wakati mgumu katika chaguzi kwa sababu ya watendaji au mawaziri kutowajibika ipasavyo.


inaelezwa kwa muda mrefu kumekuwa na mipango ya kuwaondoa mawaziri hao, lakini mazingira ya kuwaondoa ndiyo yamekuwa yakikosekana. Lakini hivi sasa mkakati umeshaiva.
inadaiwa ziara za kuimarisha chama zilizofanywa na viongozi wa ccm katika mikoa ya ruvuma, mbeya, njombe na mtwara ndizo zimetumika kuandaa mashtaka ya mawaziri hao ambayo waliyajibu walipoitwa kujitetea.
tanzania daima jumapili limedokezwa kuwa licha ya utetezi huo, kamati kuu imemtaka rais jakaya kikwete apime hoja zilizotolewa na wajumbe wa cc kama mawaziri hao wanafaa kuendelea na nyadhifa zao.



uamuzi wa cc



kikao cha cc kilichoketi juzi, kimemtupia mzigo wa kuwang’oa mawaziri rais kikwete ambaye ndiye aliyewateua.

akizungumza na waandishi wa habari, jana jijini dar es salaam, katibu wa itikadi na uenezi, nape nnauye, alisema cc imetoa mapendekezo kwa rais kikwete ambaye ndiye mwenye hatima ya mawaziri hao.



alisema rais kikwete ni mamlaka ya uteuzi wa mawaziri na ndiye atakayeamua kuwaadabisha, kuwasukuma au kuwaondoa madarakani mawaziri mizigo.



“aliyewaweka ndiye atakayewaondoa, kamati kuu haijamwabia awaondoe, inachokifanya ni kushauri tu. Lakini madaraka yote anayo rais aliyewachagua.


“kwa mfano waziri wa chakula, kilimo na ushirika hajafika kwa muda wa miaka minne na nusu mkoani ruvuma ambako ndiko kuna ghala la chakula…, tulipofika tunduma tulikuta foleni pale mizani eti watumishi wanafanya kazi kwa saa 9, lakini sasa wamebadilisha utaratibu huo wanafanya kwa saa 24 baada ya sisi kwenda,” alisema.


nape akiwa katika ziara ya siku 26 mikoa mbalimbali, aliwataja mawaziri hao ambao wamekuwa mizigo katika serikali ya rais kikwete na kumtaka awatimue.



hata hivyo waziri chiza na kawambwa walisema kuwa hawafanyi kazi kupitia majukwaa ya siasa na wanasubiri kuitwa na kamati kuu, ili waieleze wanavyofanya kazi.


waziri kawambwa, alijinasibu kwa kujifafanisha na mti wenye matunda ambao hauishi kupigwa mawe kila kukicha.
waziri chiza alimtaka nape aache kukimbilia kuzungumza hadharani juu ya madai ya wakulima wa korosho na badala yake atafute sababu ya wakulima hao kutolipwa na serikali.
mabadiliko ya mawaziri
kama rais kikwete ataamua kulifanyia mabadiliko baraza la mawaziri itakuwa ni mara ya tatu, ambapo mwaka 2008, alilivunja kutokana na aliyekuwa waziri mkuu edward lowassa kujiuzulu kuguswa na kashfa ya kuipa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kampuni ya richmond.

mabadiliko mengine aliyafanya mei mwaka jana baada ya wabunge na wadau mbalimbali kushinikiza kuondolewa kwa mawaziri waliodaiwa kutowajibika ipasavyo.



maagizo mengine ya cc



kamati kuu pia imeiagiza serikali iangalie upya upatikanaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima wa pamba nchini.
“chama kimeiagiza serikali kutowalazimisha wakulima kutumia mbegu ya quiton badala yake elimu itumike zaidi badala ya nguvu,” alisema nape.



aliongeza kuwa cc imeitaka serikali kuangalia upya urasimu katika uwekezaji wa viwanda nchini hasa vinavyoongeza thamani ya mazao na kutoa ajira nchini.



nape aliongeza kuwa kuhusu kilimo cha mkataba kwa wakulima wa pamba, serikali imetakiwa kuratibu utaratibu wake ikiwemo kutowalazimisha.


kuhusu wakulima wa korosho, alisema kuwa kamati hiyo imeisisitiza serikali kujipanga kutatua tatizo la korosho na kuhakikisha inabanguliwa nchini.


“serikali inatakiwa kuangalia upya orodha ndefu ya makato kwa wakulima, hasa wa korosho na vyama vya msingi au mamlaka zinginezo ili kuondoa makato yasiyo ya lazima na kuongeza kipato cha mkulima.


“kuhusu pembejeo za ruzuku kamati kuu imepokea taarifa ya malalamiko ya wakulima juu ya ufanyaji kazi wa mbolea ya minjingu na kuagiza wananchi wawe huru kutumia mbolea wanayoitaka badala ya kulazimishwa,” alisema.


kwa upande wa wakulima wa mahindi, nape alisema kuwa serikali imetakiwa kumalizia malipo yaliyobaki na kuhakikisha wanakomesha utaratibu wa kuwakopa wananchi mazao yao bila kuwalipa.


“utaratibu uwekwe wa kufanya tathimini mapema ya mahitaji na uwezo wa kununua mahindi wa serikali ili kuepusha utaratibu wa kuchukua mahindi ya wakulima bila kuwalipa,” alisema.


nape alisema kwa upande wa madai ya walimu, cc imeiagiza serikali kukamilisha uhakiki wa madai hayo na kuwalipa haki zao ikiwemo kuhakikisha madeni hayazaliwi tena.


kamati hiyo pia imekemea watendaji wachache wanaojihusisha na ubadhirifu kwenye halmashauri mbalimbali nchini.



“serikali imeshauriwa kuangalia upya sheria kama zinakidhi mahitaji ya wakati na mazingira ya sasa ili kuongeza uwezo wa udhibiti na kuokoa pesa za walipakodi zinazopotea kwa walafi wachache kwenye halmashauri mbalimbali nchini,” alisema nape.

Source: Tanzania daima

note: Ccm wameshaona hali ni mbaya ahadi hazitekeleziki cc maisha bora ...kigoma kuwa dubai

maamuzi magumu hufanywa na wanaume wa kweli tu!
 
Jenerali Twaha Ulimwengu kipindi akiwa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM na Mbunge wa Taifa mwaka 1993 alisema hivi,
na nanukuu : 1) Kuna waroho wanaokitumia chama kwa manufaa yao.
2)Maadili ya TANU na CCM ya kupinga dhuluma lazima yalindwe.
3)Rushwa na uoza vitaangusha dola.
 
Filamu nyingine hii ya Magamba, Sterling: JK, Kamati Kuu ya CCM na Mawaziri saba, ngoja tusubiri tuone mwisho wake.
 
......ELIMU amteue James Mbatia maana naye aliteuliwa na J.K ... Teh teh teh teh
Magamba oyeeee
 
HABARI HIZI NI USANII NA WANACHEZEA KODI YANGU TU! WASHENZI HAWA WANANIKATA KODI KUBWA WAKATI KAZI WANAZOZIFANYA SIZIONI! Nakumbuka Bw. 1 jina nimelihifadhi, amewahi kulima mpunga pande za kasamwa geita akaajiri mtu shambani; kisha kaanza misele na safari zake bila kumkagua! Mara ya kwanza yule Mfanyakazi alichapa kazi vizuri lakini mara tu baada ya kusiha mbegu akawa hata yeye haendi shambani! Maji yalizidi mbegu zikaoza na zingine zikapelekwa na maji! Alipofika kuona mbegu/ shamba limeharibika aliamua kutimua mbio maana asingeweza lipa gharama ya hasara hiyo. Mwenye shamba wakati huo alikuwa Tabora akisubiri mavuno! Wakati ulipofikia akaja ili avune. Hakuamini! Maana hata ramani ya shamba hakuiona (Alikuta magugu tu) - MRADI KAMA NI WAKO MWENYEWE NDO MWENYE DHAMANA YA KUUSIMAMIA, SASA MKUU KAZIDI SAFARI ZA NJE! ATABADILI MPAKA BASI
 
CHADEMA na CCM wote ni wale wale kwani kila mmoja ana nia ya kutawala tu ndio maana mnatuletea uzi nyingi za kutugonganisha vichwa walala hoi. CCM tumekaa nanyi kwa miaka mingi alipoondoka mwenye chama chake kila mmoja akaanzabkukunja jamvi alilokalia mpaka sasa ni miaka 50. Najua chadema nao wakija watataka miaka 50 ili tuweze kuwatathimini na kuwalinganisha na CCM!!!!!!!!! Hapo mwananchi wa kawaida atakua na khali gani? au ndio mtakuja na uongi wa Kigoma kuwa sawa na Dubai? au ule wa mfuko wa saruji buku tano? CCM kweli mnaweza kujisafisha? au mnapenda Ma daktari wa falsafa kuendelea kufundishwa kazi na sisi div 5? je CHADEMA wote mpo safi au mtu akihoji tu mambo ya pesa na yeye anahojiwa? Maskini nchi yangu....
 
..

...Mods nisaidieni kurekebisha hapo juu !!

....hakuna kulala mpaka kieleweke!!!

maksibuku ng'wabhejasana.......

hata wangeachwa wote tu lakini mathayo davide mathayo ni zaidi ya kimeo ndani ya wizara ya mifugo
 
Hili gari lishakuwa bovu siku nyingi sana matengenezo yake yanahitaji gharama kubwa sana.
Wamiliki wa hilo gari hawana uwezo wa kubeba gharama.
 
Safi sana ccm, napendekeza Prof. Maji marefu apewe wizara ya elimu, Lusinde Viwanda, mch. Lwakatare Uvuvi, kapuya kilimo.

Umechemka ndugu,lala kidogo muda wa kazi bado na ukizingatia Korogwe hakuna foleni raha kweli kweli kwikwi kwiiii,Proph Maji Marefu hata la saba alimaliza kwa mbinde ni kama yule mbunge wa Njombe gani sijui anaitwa Deo Sanga(JAH PEOPLE)anasema anaelimu ya juu ya darasa la saba.CCM bana!fix nyingiiii.Kapuya alishachemsha hakuna nafasi ya uwaziri akacheze na wajukuu wa kike,huyu mch Lwakatare naye unene umemzidi hatutaki mawaziri wa kukaa ofisini akapambane na viongozi wa uvuvi tupate samaki wa maana.Sasa hivi huku Zambia hakuna kuvua samaki inakuaga kuanzia tar 1dec--28febr ukikutwa na samaki utaeleza vzr.Na wanamafanikio samaki anaetoka Kariba dam ni wa maana mdogo ni kilo 3!huwezi amini lkn ni kweli.Ukiwa Kashiba mtoni samaki unawona unasubiri wenyeji waje na ndoana akuuzie samaki mkubwa Tz namnuua hata 15000 kuku 4500--6000.Mrudishieni magufuri hiyo wizara tule bana
 
Naisi,veri gudi,wachunguzwe ikabainika madai ni ya kweli wawajibishe. CCM ndio mkombozi wa watanzania haina budi kuwasaidia watanzania. CCM IZI THE GAVAMENTI OF PIPO, FO THA PIPO ENDI BAI THA PIPO(Abraham Lincolin).
 
Back
Top Bottom