..Mawaziri saba watoswa.....

..Mawaziri saba watoswa.....

Watanzania kuweni macho,msije mkawa mnafukuza malaika kwa kusikiliza malalamiko ya mashetani!Nuru na giza havichangamani hata siku moja.Mheshimiwa Chiza kama JK atawasikiliza hawa ni bora urudishe na kadi yao uende kinondoni ukachukue ya CHADEMA.Kule ndiko waliko malaika wenzio.Nepi namuuliza tu,hivi hayo unayozungumza majukwaani kuhusu Chiza ni ya kweli?Na kama ni kweli matatizo ya kilimo nchini chanzo ni Chiza au chama chenu na serikali yake?ni kweli Chiza ndio tatizo au umepata platform ya kuondoa mtu ambaye ni kikwazo kwa maslahi ya watu binafsi pale wizarani?Watanzania kuweni makini sana.Hiki chama hiki!Hiki chama hiki!hiki chama hiki!hii serikali hii!Mungu anajua.
 
kweli kaka mpaka sasa hivi tuna post idara ya irrigation haijapewa hata thumuni.nape anabadilisha kocha wakati timu mbovu
Hii ndio tatizo la mambo ya siasa,yaani wanasiasa wanaongea sana ili kupata huruma kwa wananchi,lakini inapokuja ktk kutekeleza walichokiongea ndio tatizo linapoanzia,huwezi kusimamia wizara kama haina pesa,Nape anadhani Engineer chiza anatozitoa wapi pesa za kuendesha wizara,kama serikali haitoi pesa ktk wizara husika,hata akija maraika,ataonekana hawezi kuongoza,
Nape igeni china-CPC,watatekeleza kwa kuwezesha wizara kufanya kazi na si kupanda majukwaani na kupiga kelele kuwa huyu hafai.
kwa mfano,watanzania wamelipia huduma ya umeme na tatizo kubwa mpaka sasa ni nguzo na wire hakuna,inamaana Tanesco hawana pesa ya kununua hivyo vitu na upo uwezekano pesa zilizotakiwa ziende Tanesco hazijafika hadi leo,Nape alitakiwa kuisimamia serikali isambaze pesa kwa wizara zake na si kukimbilia ktk majukwaa ya siasa na kuwataja wale wanaosimamia sera kuwa ni mzigo,mzigo sio hao,mzigo ni nyie wanasiasa mnaoingiza siasa hadi ktk maswala ya kiutendaji.
utasikia siku za mwisho wa mwaka pesa zinavyomiminika ktk mawizara na unaelezwa eti utumie milioni 300 ndani ya siku 7 na report ifike sehemu husika.kwanini pesa hizo haziletwe mwanzo wa mwaka na zikafanya kazi inayokusudiwa?
Napeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,acheni siasa bwana.
 
Sio hao tu bado wapo wengine na huwa
najiuliza muda uliobaki hao wapya watafikia
Ahadi alizotoa rais ama ni kutengeneza ulaji
 
Waziri Chizza amemtaka Nape aache kukimbilia kuzungumza hadharani na badala yake aseme kwanini Serikali haijawalipa wakulima wa korosho.........hapa Napo kuna ukweli fulani.
 

...Mkuu jamaa wana phd ya mazingaombwe...

Wakina Nchimbi wako wengi. Ike kesi ya Kainerugaba Msemakweli ya kuwataja vihiyo wa elimu hivi iliishia wapi baada ya wakina Makongolo Mahanga kutishia kumshitaki?
 
Raisi mwenyewe ndio mzigo namba 1.Hivi yeye huwa haoni uzembe wa mawaziri wake mpaka bunge au kamati kuu ya chama imshinikize?!

Hivi hata utekelezaji wa maazimio ya bunge tatizo ni mawaziri peke yao bila JK kuhusika?

Haya ndio madhara ya Raisi kutwa kupiga misele badala ya kuangalia nchi inakwendaje

Raisi ukingojea kuletewa taarifa tu, ujue kazi itakushinda.

Yeye mwenyewe haoni utendaji mbovu wa wateuliwa wake,anasubiri kusikia,nimeambiwa ooh wanasema,nk,huyu kilaza wa Elimu Kawa-Mbwa ndio ilitakiwa awe wa kwanza kutimuliwa tena na viboko juu,maana ameifanya Elimu ya Taifa letu kama ndio platform ya umburula wake.
 
Baada ya hapo nimesikia vibaka wa buku 7 Lumumba wanajiandaa kuja na threads nyingi kwamba CCM ni mfano wa kuigwa kwa kufanya maamzi magumu. Hebu watazame jinsi wanavyojipanga kuleta umbeya!!
attachment.php

Ahaaa haaaaa,naona Sixgate kaamua kuvua Shati kabisa.
 
Mwenyekiti wa Chama ambaye ndiye Rais wa serikali anateuwa Waziri ambaye hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake halafu anapelekwa kwenye Mahakama inayosimamiwa na Mwenyekiti.Hii imekaaje na Kamati ya katiba imependekeza nini kuhusu hili?.
 
Nimefrahi..., Bora Kawambwa aondoke muasisi wa muungangano wa Tanganyika na Zimbabwe awe waziri kamili.
 
baada ya hapo nimesikia vibaka wa buku 7 lumumba wanajiandaa kuja na threads nyingi kwamba ccm ni mfano wa kuigwa kwa kufanya maamzi magumu. Hebu watazame jinsi wanavyojipanga kuleta umbeya!!
attachment.php

samahani jamani , naomba kuuliza , hivi hapo ni mwaisela , sewahaji au wodi ya wazazi pale temeke hospital ?
 
Back
Top Bottom