Mawaziri kuunguruma mkutano wa CCM kesho Jangwani

Feb 8, 2012
92
8
Chama cha mapinduzi kitatumia mbinu ya kujijengea imani kwa wananchi kwa kuwatumia mawaziri watendaji kazi wasio na kashfa kama akina Magufuli ili kupangua hoja za CHADEMA katika harakati za Movement for Changes.Magufuli atapata fursa ya kuelezea jinsi gani serikali ya CCM ilivyofanikiwa kuboresha miundombinu.Vilevile atakuwepo waziri Steven Wassira kuelezea mafanikio ya CCM katika kukua kwa uchumi.
 
Hata kama watawatumia hao mawaziri kiukweli serikali imewashinda ila wanaona haya tu kuwaachia wengine wajaribu kusongesha hili gurudum.
 
Chama cha mapinduzi kitatumia mbinu ya kujijengea imani kwa wananchi kwa kuwatumia mawaziri watendaji kazi wasio na kashfa kama akina Magufuli ili kupangua hoja za CHADEMA katika harakati za Movement for Changes.Magufuli atapata fursa ya kuelezea jinsi gani serikali ya CCM ilivyofanikiwa kuboresha miundombinu.Vilevile atakuwepo waziri Steven Wassira kuelezea mafanikio ya CCM katika kukua kwa uchumi.
Magufuli ataeleza nini kuhusu ahadi aliyoitoa kwa wana Igunga wakati wa uchaguzi mdogo? Wassira naye atasimulia nini kuhusu uchumi wakati bado yuko ndotoni akiuchapa usingizi!
 
Bado tu wanaandaa mikiutano kuelezea watu kukua kwa Uchumi?
 
Duh nimemsikia Violet Mzindakaya akiuunguruma Clouds kupitia amplifier. Kijana anatiririka! Anasema mawaziri watakuwepo, kinana atakuwepo, mwakyembe atakuwepo, Magufuli atakuwepo, makamba mdogo atakuwepo, nk.
 
Magufuli ataeleza nini kuhusu ahadi aliyoitoa kwa wana Igunga wakati wa uchaguzi mdogo? Wassira naye atasimulia nini kuhusu uchumi wakati bado yuko ndotoni akiuchapa usingizi!

Mkuu Mag3 kwani wakandarasi wahajafika daraja la Mbutu?
 
Last edited by a moderator:

Hata magwanda ya khaki tunawakaribisha kesho hapo Jangwani, njooni msikilize ukweli ulivyo sio mnakaa kudanganya watu mtawapa simenti za bure.
 
Jamani Lusinde kesho naye apatiwe nafasi amwage cheche kwani tumemiss busara zake tangu uchaguzi wa Arumeru umalizike.
 
Uchumi unakua au unaporomoka?lazima uwe kichaa kutamka maneno ya wassira
 
Chama cha mapinduzi kitatumia mbinu ya kujijengea imani kwa wananchi kwa kuwatumia mawaziri watendaji kazi wasio na kashfa kama akina Magufuli ili kupangua hoja za CHADEMA katika harakati za Movement for Changes.Magufuli atapata fursa ya kuelezea jinsi gani serikali ya CCM ilivyofanikiwa kuboresha miundombinu.Vilevile atakuwepo waziri Steven Wassira kuelezea mafanikio ya CCM katika kukua kwa uchumi.
ahaaa apes ahaa apes ndani ya CHADEMA SQUARE.
 
Duh nimemsikia Violet Mzindakaya akiuunguruma Clouds kupitia amplifier. Kijana anatiririka! Anasema mawaziri watakuwepo, kinana atakuwepo, mwakyembe atakuwepo, Magufuli atakuwepo, makamba mdogo atakuwepo, nk.

Mkuu tangu vuguvugu la M4C lianze ulipotea ghafla.Karibu tena
 
Magufuli aulizwe na kueleze sababu za kuuza nyumba za serikali kwa bei ya chee tena mpaka kwa mtoto aliye chini ya miaka 18 huku akiacha wafanyakazi wa serikali wakitaabika.
 
Mkuu Molemo nipo sana nafuatilia kwa umakini sana vuguvugu zote: M4C na hii ya vua gamba vua gwanda vaa uzalendo! Siasa imefika patamu kwa kuwa sasa siasa zinafanywa bila virungu vya polisi. Sijasikia mshikemshike yoyote huko kusini au ni kwa kuwa CDM ilikuwa ugenini? Mkuu siasa za sasa naona zinabalance watu wanafanya mikutano bila vurugu; hiyo ndiyo siasa.
 
Last edited by a moderator:
Magufuli aulizwe na kueleze sababu za kuuza nyumba za serikali kwa bei ya chee tena mpaka kwa mtoto aliye chini ya miaka 18 huku akiacha wafanyakazi wa serikali wakitaabika.

Hivi kwenye mikutano kama hiyo kunakuwapo maswali kweli? Ngoja kesho Magufuli amwage takwimu za ujenzi na ukarabati wa barabara. Naona kama kesho atakuwa akihutubia huku matingatinga yakiwa yanapita pale jangwani huku yakiwa kazini kujenga barabara ya magari yaendayo kasi! Nadhani pia atawajibu kuhusu daraja la mbutu! Nasikia pia huko mwenge - Tegeta matingatinga yanapishana! Tabora nasikia pia matingatinga yanapishana. Huko mbeya matingatinga kila barabara! Nasikia daraja la malagarasi pia wakanda wanapiga mzigo wa kufa mtu. Kama namuona Magufuli akitiririka na data za idadi ya matingatinga yaliyojazana Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa barabara!
 
CCM wanahaha. Wanachopaswa kufanya ni kutenda wala si kusema majukwaani. Tumewapa dola na tunataka utendaji si longolongo.
 
Back
Top Bottom