CCM Kata ya Jangwani yasoma Khitma Kuwarehemu Wapigania Uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,922
30,271
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) KATA YA JANGWANI IMESOMA KHITMA KUWAREHEMU WAPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA

CCM Kata ya Jangwani leo wamesoma khitma kuwarehemu wapigania uhuru wa Tanganyika waliotangulia mbele ya haki.

Wana CCM wa KATA ya Jangwani kwa kuzingatia kuwa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM pale Lumumba ipo ndani ya Kata ya Jangwani kwa kushirikiana na viongozi wamesoma khitma ya kuwarehemu wazee wote walioshiriki katika harakati za ukombozi wa Tanganyika kuanzia enzi za African Association hadi TANU na CCM.

Khitma ilifanyika katika uwanja wa Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Kariakoo, Zakaria Digosi Lumumba Avenue.

Hakika hili ni jambo la zuri na limewafariji wanachama na wapenzi wengi wa CCM na khasa wale ambao wazee wao walikuwa mstari wa mbele katika kupambana na ukoloni.

1694892684003.png
 
Back
Top Bottom