Kauli hii ya Mwenyekiti kuhusu mawaziri na wabunge wa Ccm, kujiunga na CDM. Ni muhimu sana na ya kupewa
kipaumbele, inatuhakikishia kama Ccm itayeyuka kama barafu muda si mrefu. Hao wahusika watajwa hapo
wasiwe na maswali ya kujiuliza na kuchukua muda, milango ya ukombozi ipo wazi kwenu, mnakaribishwa.
Kwani CDM ipo kwa kupigania haki ya wanyonge, kutokomeza umasikini na kuleta maendeleo, kikuu zaidi cha
kukamilisha hayo yote ni kuondoa ufisadi na rushwa katika mioyo na macho ya Watanzania.
Kwani ukichaguliwa kuwa na dhamana ya uongozi, tuchukulie mfano. Waziri, Katibu Mkuu na Mkurugenzi,
madhumuni ni kuongoza Wananchi na kuleta maendeleo, kwa wahusika wote watatu wasitegemee kutia mkono
na kuchukua hata senti tano, ambayo inaitwa pesa ya Serikali, bali ni kuilinda na kufanya kile kilichopangiwa.
hapo nina maana wawe na uhakika wa kuziba mianya yote ya ufisadi na rushwa katika sehemu husika.
na hapo ndio sifa ya Uwaziri, Ukatibu Mkuu na Ukurugenzi unapokuja, namalizia kwa kusema mwelekeo ni
Serikali mpya itakayoongozwa na CDM kabla ya 2015. DC wa Mbozi kesha kufungulieni milango na nyinyi amna
haja ya kuchelewa katika kuikomboa nchi.