Mawaziri 7 wabunge 70 wa CCM kujiunga CHADEMA!

Kama wanamaanisha kweli wajiuzuru nyadhifa zao sasa na kujiunga CDM. kama wanasubiri vipindi vyao vya uongozi viishe watakuwa ni ma-optunist tu hawana kitu.

Umeona eeeh! Hawa jamaa ni wanafki,na hapa ndipo VIONGOZI WA CHADEMA wanapaswa kutafakari,kama JAMES MILYA alivyofanya,hawa nao wajiudhulu nyadhifa zao hapo CCM na watangaze nia zao kuhamia CHADEMA,bila hivyo,tutegemee kuja kuibiwa tena.
 
hao waliomba kujiunga cdm ndio wanaotoa siri za serikali ni baraka kwa ccm kuwa magamba yanaondoka yenyewe yanakimbilia cdm

Serikalini hakunaga siri kama hulijui hilo,siri ni ya mtu mmoja tu mkizidi zaidi ya hapo,ujue hiyo sio siri tena
kalaga baho na ujinga wako.
 
Umeona eeeh! Hawa jamaa ni wanafki,na hapa ndipo VIONGOZI WA CHADEMA wanapaswa kutafakari,kama JAMES MILYA alivyofanya,hawa nao wajiudhulu nyadhifa zao hapo CCM na watangaze nia zao kuhamia CHADEMA,bila hivyo,tutegemee kuja kuibiwa tena.

Yes inatakiwa waachie nyazifa mapema ndipo wajiunge,tofauti na hapo waendelee kukaa hukohuko.
 
Mwenyekiti wa chadema freeman Mbowe amasema amepokea maombi ya mawaziri7 na wabunge70 wa ccm kujiunga chadema.

Chanzo: Tanzania daima
Kila siku hapa JF tunaelezwa kuwa wabunge na mawaziri wa CCM ni vilaza/wezi sasa inakuwaje Mwenyekiti wa CDM anawakubali kuingia kwenye chama kinachojihisi kuwa ni makini na wazalendo.Haya bana wakaribisheni.
 
Mwenyekiti wa chadema freeman Mbowe amasema amepokea maombi ya mawaziri7 na wabunge70 wa ccm kujiunga chadema.

Chanzo: Tanzania daima

Mwananchi:
mods watusaidie kubadili hapo kwenye heading. Hii habari sio tetesi. Ni dhahiri na source imeainishwa.
 
paganda zingine bwana! Si angefanya kimya kimya? Kama ni kweli hapakuwa na sababu ya kuweka hadharani haya, yasije kuwa kama ya ccjee?
 
Wanakaribishwa ila walowekwe kwa maji yalotiwa omo kali kwa miaka minne kabla ya kujiridhisha kuwa magamba yametakaswa.
 
CCM ina mbinu nyingi watajiunga wote 2013 chadema watarudi ccm mwaka 2015 June...... cdm bado watoto kwenye siasa ccm chama kikongwe kina wanachama mpaka mwituni
 
Mie sioni ubaya....kama chama kiwape muda wa malezi kabla ya kuanza kufanya shughuli za chama....wote hawawezi kuwa mamluki (Shibuda)...kuna wengine wana nia ya kweli (Dr.Slaa)!
 
Hata Slaa alipobamizwa kwenye kura za maoni alikimbilia chadema. Taka taka na uozo wa uadilifu hatuukubali CCM.
 
hao waliomba kujiunga cdm ndio wanaotoa siri za serikali ni baraka kwa ccm kuwa magamba yanaondoka yenyewe yanakimbilia cdm

Magamba hayataki kuondoka 7bu yanajua ccm itawafanyia fitina ila waliochoshwa na uchwara wa ccm ndo wanaondoka nadhani hata magamba sugu yanajulikana na ccm na wanatamani yawatoke ila hawawezi na wanashindwa kuwaondoa kwa nguvu
 
hao waliomba kujiunga cdm ndio wanaotoa siri za serikali ni baraka kwa ccm kuwa magamba yanaondoka yenyewe yanakimbilia cdm

Ukimvua kobe gamba lazima afe, kwani gamba ndio uhai wake. Wabunge na wananchi walimshauri rais kuwa Magamba kwa sasa yapo 8 lakini yeye akavua 6 tu. Hayo mawili yaliyobaki yataendelea kukua na kumfunika kobe mzima.
 
Hata Slaa alipobaizwa kwenye kura za maoni alikimbilia chadema. Taka taka na uozo wa uadilifu hatuukubali CCM.

Jiwe walilolikataa waashi.......hata hivyo paka na panya hawawezi kuishi pamoja kwa amani....
 
Back
Top Bottom