Wakuu JF heshima mbele sana,
- Well, kitendo cha Rais kuwabadili mawaziri waliokuwa wakituhumiwa kuhusika na upotevu wa hela za wananchi na ripoti ya CAG, kina maana moja tu kwamba hata na yeye ameridhika kwamba kuna ukweli au FACTS katika tuhuma walizokuwa wakituhumiwa nazo, ninasema great second day kwa Taifa, kwanza ilikuwa kuweka ripoti wazi to the public na kuruhusu mjadala wa public!
- Sasa ifike mahali pa kufanya kweli, yaani Watuhumiwa wote kufikishwa kwenye mkondo wa Sheria, haki itakua imetendeka na sio otherwise, kwanza haki kwao mawaziri maana wanahitaji kuwa wasafi mbele ya public na pili Serikali kulinda heshima yake kwamba sasa ipo serious, ama sivyo kuitoa ripoti ya CAG to the public itakuwa ni kazi ya bure, I mean mawaziri na viongozi wetu wakijua kwamba madhara ya kuiba ni kujiuzulu tu na kuachiwa ukale mihela ya wananchi tutakua tunajenga taifa la kusadikika, na itakuwa kazi kubwa kumpitisha Rais wa CCM 2015!
- MHESHIMIWA RAIS, UBARIKIWE KWA KUSIKILIZA MAONI YA WANANCHI, SASA TWENDE MBELE ZAIDI TUFIKE KWENYE SHERIA NA WOTE WENGINE HAO MAKATIBU NA WAKURUGENZI ULIOSEMA KWENYE HOTUBA YAKO KUWA WANAHUSIKA NA WAO PIA UWE MWENDO WA KUELEKEA KWENYE SHERIA!, NI SHERIA TU NDIO INAWEZA KUTUSAFISHA WOTE, SERIKALI NA MAWAZIRI WALIOACHWA!
MUNGU AIBARIKI TANZANIA!
William @DSM CITY!