Mawaziri 6 sasa mikononi mwa TAKUKURU! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri 6 sasa mikononi mwa TAKUKURU!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, May 7, 2012.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Wakuu JF heshima mbele sana,

  - Well, kitendo cha Rais kuwabadili mawaziri waliokuwa wakituhumiwa kuhusika na upotevu wa hela za wananchi na ripoti ya CAG, kina maana moja tu kwamba hata na yeye ameridhika kwamba kuna ukweli au FACTS katika tuhuma walizokuwa wakituhumiwa nazo, ninasema great second day kwa Taifa, kwanza ilikuwa kuweka ripoti wazi to the public na kuruhusu mjadala wa public!

  - Sasa ifike mahali pa kufanya kweli, yaani Watuhumiwa wote kufikishwa kwenye mkondo wa Sheria, haki itakua imetendeka na sio otherwise, kwanza haki kwao mawaziri maana wanahitaji kuwa wasafi mbele ya public na pili Serikali kulinda heshima yake kwamba sasa ipo serious, ama sivyo kuitoa ripoti ya CAG to the public itakuwa ni kazi ya bure, I mean mawaziri na viongozi wetu wakijua kwamba madhara ya kuiba ni kujiuzulu tu na kuachiwa ukale mihela ya wananchi tutakua tunajenga taifa la kusadikika, na itakuwa kazi kubwa kumpitisha Rais wa CCM 2015!

  - MHESHIMIWA RAIS, UBARIKIWE KWA KUSIKILIZA MAONI YA WANANCHI, SASA TWENDE MBELE ZAIDI TUFIKE KWENYE SHERIA NA WOTE WENGINE HAO MAKATIBU NA WAKURUGENZI ULIOSEMA KWENYE HOTUBA YAKO KUWA WANAHUSIKA NA WAO PIA UWE MWENDO WA KUELEKEA KWENYE SHERIA!, NI SHERIA TU NDIO INAWEZA KUTUSAFISHA WOTE, SERIKALI NA MAWAZIRI WALIOACHWA!

  MUNGU AIBARIKI TANZANIA!  William @DSM CITY!
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wale mawaziri waliofikishwa mahakamani miaka ya nyuma akina yona na mramba mpaka leo kesi zao ziko mahakamani hawajahukumiwa... hawa wengine wako wengi mno na nina uhakika itachukua miaka 10 mpaka kesi zao kukamilika, tutazidi kupoteza hela za walipa kodi kuendesha hizi kesi alafu mwisho wa siku watapatikana hawana hatia....waste of money and waste of time

  Na kuna wengine wako kwenye hizi kashfa na bado ni mawaziri..mheshimiwa hajawatimua wote so hao aliowabakiza tuwafanyeje!!??

  Rais wetu kapangua mawaziri, Mkuu wa Polisi nae kapangua safu yake ya makamanda wa polisi...Je Nani atapangua safu ya mahakimu/Majaji wanaoendesha kesi zetu za hapa nchini? maana huko mahakamani nako kunanuka rushwa na ufisadi nani atafanya hivyo na ni lini tutegemee hilo bwana Malecela??!!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Mkapa je?
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Iundwe independent elimination squad.

  Inachunguza, inahukumu, ina eliminate kila afanyae madudu awe ni waziri au tarishi. Siku anayokuwa eliminated, anawekewa na hukumu yake na ushahidi kamili wa madudu aliyofanya.

  Wakifika watano tu! ukimpa mtu hata soda atakataa! wacha "takrima" na "ten percent".
   
 5. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Hakuna lolote, labda yy Jk ajipeleke mahakamani kwanza ! Mbona bado kaweka walaji wengine kulinda maslahi yake ktk sekta flan flan ? Katibu mkuu km yule Komba alimpa zawadi ya ubalozi Uganda baada ya kufanikisha kuuza wale wanyama sasa kama kweli yy hausiki basi amtimue yule haraka na kumrudisha ajibu mashtaka !

  What about Jahiro ? Blandina Nyoni anajulikana tangu zamani, hao akina Mapunjo wanajulikana madili yao na yy mwenyewe tangu wakiwa wizara kibao mpaka alipmvuta Ikulu, na then kumpeleka viwanda na biashara ambako yy ni mmoja wa hao wenye makampuni feki na JK anajua siku nyingi.

  WTF, mnampa sifa kuwa yy ndiyo aliamua report ijadiliwe, kwani hii ni report ya CAG ya kwanza ? Ni upinzani ndiyo umesababisha haya yote na baadhi ya wabunge wa CCM baada ya kufuatilia wakagundua ni kweli wenzao wanakomba bila huruma na JK anajua na kuhusika thru mtandao plus RZ1. Mbona yule DED aliyetafuna mahela akiwa Bagamoyo, rafiki yake mkubwa ndiyo kampa u RC Arusha ?

  So wewe acha hizi sifa hewa unless sasa unavizia nafasi iliyobaki ya kuteuliwa ubunge !! Vp anakuja lini kufungua tawi lako la CCM...lol   
 6. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Interesting.........
   
 7. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  misamiati kama hii haipo nchini mwetu hata ikijitokeza huwa ni kiini macho na milango mingine ya kujipatia pesa tukumbuke kuwa Serikali yetu haina historia ya kushinda kesi mahakamani
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,747
  Likes Received: 82,686
  Trophy Points: 280
  ....Kipindi hiki ambacho msanii bado amejaa tele pale Ikulu hii itakuwa ni ndoto ambayo haitakuja kuwa kweli.
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Unabembeleza sheria kuchukua mkondo wake! tena kwa kumsifu rais, walikunyima kura kihalali kama akili yenyewe ndio hii.
  hii inatokea tanzania pekee
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,187
  Trophy Points: 280
  Wanashtakiwa Tanzania au The Hague?
  Kama ni Tanzania, hamna kitu ni longolongo dot com.
  Wapi kesi ya kina Mramba na Daniel Yona?
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,187
  Trophy Points: 280
  Kumbe huyu bwana ndiye yule zuzu aliyekuwa anajisifu kuwa amekaa sana nje?? Afadhali hakujitambulisha kuwa ni mwana JF, angetutia sana aibu
   
 12. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Kupitia report ya CAG, hao wahujumu wafilisiwe jamani! Nyongeza yake kizuizini miaka kumi, kisha wanaachiwa wakiwa hoi na hawawezi tusumbua tena.
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,198
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ha! Ha! ha! ha! ha! ! ! Mbona katurudishia walewale walio Chakachua kura za ubunge Kama rafiki yako na mbunge wako Mahanga
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  May 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hata wakipelekwa mahakamani wataishia kutakaswa tu na watatoka vifua mbele. Hakutakuwa na ushihidi (uwe upo au haupo) wa kuwatia hatiani moja kwa moja! Ingekuwa enzi za udikteta unachukuwa tu mali zao na ku freeze akaunti zao unawapeleka kuchunga ng'ombe huko kwao na wasikanyage mjini tena. Lakini sasa ndio tunaambiwa utawala wa kisheria na demokrasia. Wajanja wanatumia hiyo demokrasia na utawala wa kisheria kutuibia kisheria.
   
 15. Michese

  Michese JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nadhani ingekuwa vyema wangeanza na huyu
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  May 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Ribosome hii ni kali sana lakini naipenda. Hii ikifanyika mbona mambo yatakuwa safi kabisa. Mambo ya uchunguzi hadi upate ushahidi usio na shaka ati mahakama iwatie hatiani ni kama ndoto vile. Ukiwapeleka mahakamani wanaenda kuwa laundered!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  William @ DSM City Nilifungua Thread yako Nikijua huu ni uhamuzi wa ndani ya chama kuwa mumeazimia kuwafikisha Mahakani kumbe na wewe unataka usikie JF Wanasemaje kuhusu hili!Nafikiri una platfom nzuri ndani ya chama kumfikishia Raisi huu ujumbe wako. Majibu atakayokupa ndo utubandikie hapa!

  Mytake: Kuwapeleka mahamani is One Thing, Sheria kuchukua Mkondo wake is the 2nd Thing......Mramba,Yona na Wengine wapo Bunge Zimeishiwa wapi?

  Ubarikiwe Le Bahari Bongo kama NY au unasemaje!
   
 18. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Le Baharia wewe ndio unaongea hvyo? Katika ccm nani anayeweza kumvisha paka kengele? Labda Deo Filikunjombe ndio anaweza!! Si tu kupelekwa mahakamni na pia kufilisiwa mali walizopata kwa rushwa na kuhujumu uchumi...Kwa mshaara gani mtu uweze kununua nyumba ya dola 700k? Kwa mshaara gani uweze kujenga nyumba ya ghorofa 5 tena fasta fasta? Mkulo ni fisadi anashirikiana na al-sayeed pamoja na babylon kuficha mali zake,magari ya al-sayeed ni ya mkulo,majengo ya babylon ni ya mkulo.
   
 19. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Le Bahari Ebu tusaidie kuelewa Hivi Wazo la Kuwepo kwa Waziri asiyekuwa na Wizara Maalumu(Minister without Portifolio)Lilitolewa na CC au ni aloud thinking ya Mukulu mwenye? Hii Cheo kilikuwepo some years back then kikaondolewa,kimerudishwa tena Je,Kina Tija kwa Taifa lenye uchumi wa kama wetu?

  Heshima mbele kama Tai Mkuu!
   
 20. c

  crazyworld Member

  #20
  May 7, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimeipenda. Imekaa vizuri.
   
Loading...