wa unajitetea ... but kuna ile ya nakwenda motoni lakini nakwenda motoni nikiwa clean. Found guild out of cicumstances. Naimagine mwanamke/mume ambaye mkewe/mumewe amekuwa busy kwa muda mrefu (sijui kama tunakubaliana kuwa kuna wanandoa wengine wanakaa hata miaka miwili. mitatu wakiwa ignored simply because mume amejipatia mahali pa kulaza kichwa chake. Anahemea (Ingawa amepata pa kulaza kichwa chake.
How do we help??
Aksante Darl. Tunakubaliana lkuwa kuna sababu hakuna marefu yasokuwa na chanzo. Baadhi ya marefu haya ni
Kwa Mke
1. Mume kwa sababu moja au nyingine he doesnt find the wife attractive anymore- anaanza kudoubt penzi lake kwakev2. Baada ya kuwekwa kwenye himaya ya mume, mume akaamua kuyarudia makoloni au koloni lake na mapenzi yote kuhamia kwa small houses na yale maviapo ya laiti ningejua nisingemuoa. (Ikifikia hali hii jua kuwa uwezekano wa mke kumketisha mume chini kumweleza kuwa hapendi alivyobadilika siku hizi, ni ndogo sana. Mume atafanya juu chini asimpe nafasi mke kumbana.
2. Mume ameshamchoka, (after three to four years love lifespan yake imekwisha - kuwa alimwoa outs of infatuation and not love. Sasa all he feels kwa mkewe ni hatrage and hata muda wa discuss naye issues anaona kero e.t.c.
Mume:ri ikamtia jeu nzu1
1. Mke amepata kazi nzuri ikamtia jeuri na kumwona mume mwanaume suruali hana hali wala muhali
2. Mke amepata mshefa huko barabarani mwenye kumfanya amwone mumewe si mali kitu asimbabaishe (kumbuka victim hapa ni Mbaba anayenyimwa haki zake za ndoa. e.t.c.
Sasa hapa victims tunawashauri vipi kurejesha mawasiliano?????
Nakubaliana a wewe asilimia mia kwa mia.
Kelvin sweetheart, msitari wangu wa mwisho unaelezea kabisa kuwa hakuna sababu yoyote inayokubalika kwa kucheat. Ishu yangu ipo kwenye hizo nukuu mbili. Cheating an lack of communication.
Chukulia mifano hii
Scenerio I. Mwanamke mwenye mumewe ambaye (kwa sababu anazozijua yeye) anamdharau, anamuignore, hamjali na kumwuumiza psychologically. Na mwanaume huyo huyo hana compromise wala haitaji discussion yoyote ndani ya nyumba hata kama analeta chakula, analipa ada kwa watoto n.k But hana intimacy na mkewe. Na kwa bahati mbaya mke huyu hana guts/ uwezo wa kuquit hiyo relationship (either watoto, jamii n.k)
Scenerio II. Mwanaume anayeishi na mke anayemdharau, hamjali, yeye na remote (kama mnavyolalamika hapa). Mke ambaye kushiriki tendo la unyumba ni nadra, e.t.c..
Jamii inapoombwa kutoa ushauri kati ya hawa, mara nyingi utasikia mwanaume anaambiwa ......Kiboko ya mkeo, mtafutie msaidizi (nyumba ndogo) atanyooka. Lakini mwanamke anaambiwa avumilie ndio maisha ya ndoa yalivyo!!
Tukisema tuapply communication skills hapa, hebu tupeni ujuzi wengine hapa, katika situation kama hii, unavunjaje ukimya??
Topic ngumu hii Jamani... Inapasua kichwa ile mbaya!! Na Roho kuuma mno! I wish kwamba Mungu angeweka ukioa/olewa feelings zinafia hapo na wala huwezi pata hisia juu ya mwingine kamwe - Married life would have been So simple! Enways tuendelee.....
Mawasiliano ndo kitu kinachotofautisha level ya mahusiano. Kama mwenza wako tunasema 'ur better half' halafu unawasiliana na jf (ni mfano tu)zaidi kuliko yeye,usitegemee mahusiano yako na mwenza wako kuwa better than yako na jf(ambapo utaongeza na communication kabisaa).
Ni kweli cheating is a premeditated action,tena a very well planned! Lakini kukosekana kwa communication ni chanzo cha yote. Hata mume kushindwa ku-communicate feelings zake kwa mke,mke ku-communicate na mume kuhusu matamanio yake kwake is all abt communication! Ila kwa wanawake tunajitahidi ku-communicate in the form ya 'kulalamika' na ukishaanza kuitwa vuvuzela ndo unaimalizia communication with the last nail. Mara ngapi umesikia mwanamke akimuambia mumewe 'sitakuuliza wala kulalamika juu ya hili tena,EVER!!' Na mume kujiskia sasa ndo uhuru umetangazwa? Na hii ya mwanaume kulalamika mkewe hapendi sex, samahani kwa kuwakwaza for nina hakika nitawakwaza,ni kosa la mume kushindwa kuwasiliana na feelings za mke! Kama flirting unayofanya na small house ungefanya half of it nyumbani mambo yangekua bam-bam,lol!mtu anondoka home asubuhi,anapotea kutwa anatokea saa tano usiku na pombe zilizochachia mdomoni halafu anategemea intimacy? Hiyo ni communication breakdown,trl wanahusika! Tofauti ya mzazi wako na mwenza iko kwenye communication tuuuu!narudia kuomba radhi kwa kuwakwaza
Mchumba wangu kapata kazi juzi juzi hata miezi miwili haijapita!! Tangu apate kazi, mawasiliano yamekuwa shida! sababu anachoka akirudi kutoka kazini anadai anaingia jikoni moja kwa moja! Na hata wakati wa weekend, nayo inakuwa shida kumpata!!
Nirudi nyuma kidogo! wakati hajapata kazi, tulikuwa tunawasiliana vizuri sana tena sana tu! Sasa hapo ndo napoanza kunusa harufu ya ama kuachana (which is not a solution at all) au kuvumilia huku nikijipa maumivu makali ya hisia za huyo mchumba wangu kunicheat. Kwa hiyo nachotaka kusema hapa, watu wanaobligation nyingi sana kwenye mahusiano! ukikuta wanamahusiano wako na furaha muda wote basi hao wanakitu kinachowaweka pamoja pengine kikitoweka wanaweza wasiwe na furaha tena kwani ni wachache sana siku hizi wanaweza kuvumiliana kutokana na previous life story zao.
"Hata mume kushindwa ku-communicate feelings zake kwa mke,mke ku-communicate na mume kuhusu matamanio yake kwake is all abt communication! Ila kwa wanawake tunajitahidi ku-communicate in the form ya 'kulalamika'
Na hii ya mwanaume kulalamika mkewe hapendi sex"
king'asti umenena but, hapa nagundua kuna matatizo mawili, moja ni lack of comminication na la pili ni how to communicate,
hii ya kulalamika si njia nzuri ya ku-communicate hata kidogo tena inaweza kuongeza matatizo mengine ikaonekana wewe ni mlalamishi na hakuna
mwanaume anayependa mwanamke mlalamishi so ni lazima muwe wabunifu wa kujua nzuri ya ku-communicate.
Babu nimekuelewa ni kweli kuwa hii si sababu ya kwenda nje ya ndoa. But leo Mjukuu wako Mtiifu mmenichanganya kabisa kwa sababu mwanzoni nilidhani hii kwenu huwa ni ticket halali ya kutoka maana hapa hapa nilishasoma sana mwanaume akijalalamika kuhusu mapungufu ya mkewe mnamshauri atafute nyumba ndogo!! Au ni mimi tu nlichanganya madawa?!Nakubaliana na wewe kwamba wapo watu ambao wanaweza kujikuta wameachwa njia panda na wenzao bila sababu yoyote ya msingi wala maelezo ya maana!
Hata hivyo siamini kama dawa yake ni kwenda kujianika uchi huko nje...Bado naamini kuwa mtu akiamua kuzini ni ameamua tu, kwani kuna watu wana mahusiano ya ajabu ajabu lakini hawatoki nje ya mahusiano yao.
...ilikuwaje wakafikia hatua hii ya ndoa?
Aksante Zinduna nafikiri ulimaanisha wanaume wanaongoza zaidi ya wanawake sio?!MJ1 kama unaweka mizani, wanawake ndio wanaoongoza kwa ku-cheat ukilinganisha na wanawake. Kwa sisi waawake kucheat huchukuliwa kama moja ya maamuzi magumu baada ya kutendwa sana na kuvumulia vituko vya wanaume kwa muda mrefu
.
ukizidisha kiasi cha "kupunguza kuliko ilivyokuwa (awali!)" ...ndio chanzo cha vurugu zote hizi...
mnakumbuka niliwahi leta mdahalo kuhusu wheel of life?
lile gurudumu lina apply kotekote!
Kwa sisi waawake kucheat huchukuliwa kama moja ya maamuzi magumu baada ya kutendwa sana na kuvumulia vituko vya wanaume kwa muda mrefu
...naam, naam.. angalau sasa tupo ukurasa mmoja, ndio maana nikasema wamefikaje hatua hiyo
ya kuamua kutembeza naniliu zao nje!...
Chanzo ni dharau, jeuri, kiburi, etc etc...period!!!
je, tuna haja kweli ya kutafuta mchawi aliyevunja "mawasiliano?"
"mawasiliano" yalivunjwa kwa makusudi mydarling...mimi sipendi wala sitaki kudharauliwa,
kurejesha mawasiliano kutawezekanika tu iwapo patafanyika U Turn ya ukweli ya wote wawili
kukiri makosa kwa kauli na vitendo...pia kujutia!
kinyume na hapo, hakuna kinachoweza sawazisha hayo.
....lol...umenifurahishha sana....
hisia za nini?
hapa sasa inategemeana na kiwango cha imani yako...kama roho imetakasika
kila tamanio utaajua ni nguvu ya kishetani...lakini kama imani yenyewe ni ya viraka viraka, weee!....!
Hahahaha AshaDii umewaza mbali mpenz but ni ukweli mtupu! Laiti ingekuwa hivyo. Mimi nilishashuhudia mahusiano ambayo mmoja wa wanandoa alijikuta kwenye wakati mgumu,ambao mwenzie alikuwa anamfanyia visa vya kila aina yaani ile ya mashati kurudi na milipstick, handkerchiefs za kike n.k lakini Mdada yule hakurevenge may be kwa sababu alikuwa na guts za kuquit. But kwa yule ambaye hana guts hizo, kuna mbinu yoyote ya kumsaidia akamketisha mumewena kuongea nae?Topic ngumu hii Jamani... Inapasua kichwa ile mbaya!! Na Roho kuuma mno! I wish kwamba Mungu angeweka ukioa/olewa feelings zinafia hapo na wala huwezi pata hisia juu ya mwingine kamwe - Married life would have been So simple! Enways tuendelee.....
Kuna kitu kinaitwa kwa lugha ya malikia ;HOPE!
Mtu akipenda anakuwa na hope! yaani ubaya wote unaweza kuwa dhahiri na kwa macho ya wengine hata asieleweke lakini mume/mke huyu na HOPE mambo yatabadilika siku moja! Ana HOPE kuwa mwenza atagundua thamani ya umoja wao na atajirekebisha! bahati mbaya hii mara nyingi imetokea kuwa FALSE HOPE!
Hali inaharibika na kuwa mbaya mpaka inafikia hatu hii!