Huu sio utu wala sio utanzania. Siasa ni imani sio uadui
Siasa zisituondolee utu Watanzania. Siasa ni imani kama ilivyo dini.... kama ilivyo unaweza kuwa mchungaji akatokea mwanao ameolewa na shehe au ukawa shehe na mwanao ameolewa na mchungaji au mtoto wa mchungaji. Ndivyo unaweza kuwa Chadema na watu wako wengine wakawa CCM au ukawa CCM watu wako wengine wakawa ACT au chadema. Huwezi kuwachukia na kufurahia matatizo yao.
Unaweza furahi mpinzani wako kwenye siasa akishindwa kwenye kura au wanachama wakimkimbia sababu ushindi utakuja kwako lakini kamwe binadamu mwenye utu huwezi furahia kifo. Siasa sio vita jamani
Bujibuji huyo jamaa ni wa kupuuzwa