Mavazi ya kubana - Athari kwa wanawake

hivi huyo jamaa aliyetoa hii taarifa alisomea wapi na huu utafiti alifanyia wapi,Unajua wachina ni waatalaam sana wa tiba za asili (chinese traditional medicine).hizi habari ziliniumiza kichwa ikabidi nimuulize profesa mmoja wa tiba asilia za kichina akajibu"hamna kitu kama hicho".yaani hapa nipo hoi,sasa hawa wanajjiita maproffesa hizi research walizifanya kweli?hapa china kila mwanamke anavaa jeans isipokuwa kwa sasa ni summer
 
Wanawake wavaao suruali watahadharishwa

na Esther Mbussi

WANAWAKE wanaovaa suruali aina ya jinzi na nguo za kubana, wako kwenye hatari ya kupata magonjwa hatari pamoja na kuharibika maumbo yao ya asili.

Dk. Amos Dadaoh wa Chuo Kikuu Huria Tanzania kinachotoa tiba kwa kutumia mimea, alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima. Aliongeza kuwa, suruali imetengenezwa kama vazi maalumu kwa wanaume.

"Suruali imetengenezwa likiwa vazi maalumu kwa wanaume na kwamba mwanamke kwa maumbile yake anatakiwa kuvaa mavazi yanayompa nafasi yaani yasiyobana,"alisema Dk. Dadaoh.

Alisema magonjwa wanayoweza kuyapata kutokana na mavazi hayo ni pamoja na kuota mizizi kwenye kizazi, moyo kuwa mkubwa na kushindwa kufanya kazi kama kawaida.

Alisema suruali ya kubana inahamisha mafuta kutoka kiunoni kwenda kwenye moyo na kizazi. Mafuta hayo husababisha mwanamke kushindwa kusukuma mtoto wakati wa kujifungua.

"Mwanamke ambaye amezoea kuvaa suruali hasa aina ya jinzi ya kubana, pia yuko kwenye hatari ya kupoteza uhalisia wa umbo lake na kuwa kama simba - juu kuwa mpana na chini mdogo - kwani anabana mafuta kwenye mapaja ambayo yanaingia moja kwa moja kwenye kizazi na kwenye moyo," alisema Dk. Dadaoh.

Dk. Dadaoh alisema mwanamke kiasili ni wa pembe tatu na mavazi yake ni ya kuachia na yenye nafasi yasiyobana kwenye kati kati ya mapaja.

"Ukiangalia Wakorea na Wajapani hawana kiuno wala makalio, wako bapa, ni kwa sababu ya tabia ya mazoea ya kuvaa suruali za kubana," alisema Dk. Dadaoh.

Pia alisema kina dada wenye mazoea ya kubana matiti, tumbo na kiuno pia wako kwenye hatari hii ya kupata magonjwa aliyoyataja hapo awali, kwani mafuta yanaganda kwa kukosa mwelekeo maalumu na ndiyo sababu wasichana wengi siku hizi wana matumbo makubwa (vitambi).

Alitoa ufafanuzi kuwa matatizo hayo yanayosababishwa na mavazi hayo, hayaleti madhara haraka kwa mvaaji kuvaa mara moja na kuathirika baada ya kuvua, bali huja taratibu kutokana na umri na mazoea ya kuvaa mavazi hayo kwa muda mrefu.

Your views please!

Ni wapi katika hii taarifa hapo juu imesemwa kwamba huyo Mganga amefanya utafiti?

Mbona mna introduce vitu ambavyo havipo?

Mganga amesema kwamba kigezo chake ni kwamba Wajapani wa kike wanapenda suruali ndio maana hawana matako.

Lakini hapo hapo kasema madhara ya suruali kwa Wanawake ni magonjwa ya moyo.

Sasa mbona Wajapani wasio na matako hawaongozi kwa magonjwa ya moyo?

Habari ya utafiti iko wapi hapo juu?
 
Ebu tubishane kwa hoja jamani kama huo utafiti ni sumu then kuja na wako bwana.
Personally ilo vazi huwa sipendagi akina dada wavae japo wengine huwa lawatoa.
Ila tufanyeje watu wanayapenda.
Mbaya zaidi waweza kuta mdada kakazia ilo vazi alafu pale mahara pametuna utazani puto sijui anakuwa kakazia na matambara au ndo maumbile yake basi ilil mradi tuu kusumbua watu.
Kwa wanaopendeza waendelee tuu izo impacts ni mbele ya safari ila kama wayajari maisha yako ni bora ubadilike
 
huo utafiti aliufanya kwa sample ya aina gani, wapi na wanawake waichana wa umri ganihadi walipofikia umri gani.
Je genetics na tabia za watu majibu ya utafiti wake kwa kiasi gani.
-hawa wasichana wenye maunmbo anayoyasema walivaa hizo jeans kwa miaka mingapi? na aliwafuatilia tangu wakiwa na umri gani?
-hao kina mama wenye hayo maumbo wanalianza kuvaa tangu usichana wao?

Bado hajasema chochote, zaidi ya kuonyesha kuwa haya maumbo yanamkera sana sana, mno mno.
 
inaeleke huyu daktari anafukuza wateja, kwani amejionyesha jinsi alivyo empty hapo juu.
 
Habari wakuu!
Kama medical student napata taabu kidogo kukubaliana na huyu mtafiti kwa sababu hakuleta scientific data kutetea hoja yake,lakini pia ninavyojua mtafiti sometimes huwa anatafuta lugha nyepesi ya kufahamisha umma ule utafiti wake,ukizingatia kuwa watz wengi tuna ufinyu wa elimu hivyo,labda,ilikuwa ngumu kumwaga analysis yoyote hapo katika media.
Nipo hapa China nasoma na wachina,wakorea,wa vietnam,japanese etc class;
(1).Wasichana wamaonekana kuwa na normal englishfigures(kama baadhiya wabongo)
(2).Wanawake ambao ni seniors hapa university(masters na kuendelea)plus staff members wanaanza kuonesha dalili zakuwa na makalio flat,vitambi n.k,wenye umri mkubwa kuanzia miaka38 na kuendelea tayari wana hali hiyo(% kubwa,siyo wote)
(3).Kuna nguo za ndani fulani ambazo zina tight tumbo kwa ajili ya kupunguza kitambi,zina soko sana hapa China kwa affected ladies.Kwenye matangazo ya hizo nguo wanaonesha mechanism yake ni kuhamisha fat kutoka tumboni na kuelekeza makalioni,kwa wale ambao imewasaidia hiyo tiba wanaonekana kuwa na figure za kibantu.LAKINI SIJASIKIA WAKIAMBIWA WASIVAE JEANZ ILI KUONDOKANA NA HILO TATIZO.
Kwa hivyo yawezakuwa ni changamoto kwetu kuliweka katika scientific analysis ili kama ni kweli liweze kusaidia wote duniani,na tusijione kuwa WATZ hatuwezi kufanya hivi vitu,hawa wachina hawatuzidi kitu zaidi ya uwajibikaji.(Here I mean Siyo kama KABOKA Alivyo m despise professor wetu over Chinese one)
 
Naweza kusema, kwa utafiti wa Daktari wetu, kwamba mtu mwenye miguu membamba wazazi wake walimvisha tight nappies au chupi za kubana .... na kachelewa kutembea kwa sababu hiyo kwani miguu haikuweza kusupport mwili .... wazazi tuwe wangalifu tena hasa kwa watoto wa kike ... wa kiume hata akiwa na vijiti ... atavificha kwenye suruali
 
Hili la wanawake na nguo za kubana silijui, lakini nimeshasikia kwamba wanaume wanaovaa chupi za kubana na suruali za kubana na pia kuoga maji ya moto wanaongeza infertility na hivyo kuongeza uwezekano wa wake zao au washikaji (wanashika nini vile...:)) kupata mimba.
 
Wanawake wavaao suruali watahadharishwa
na Esther Mbussi

“Ukiangalia Wakorea na Wajapani hawana kiuno wala makalio, wako bapa, ni kwa sababu ya tabia ya mazoea ya kuvaa suruali za kubana,” alisema Dk. Dadaoh. !

Huenda jamaa anasema kweli maana kusingekuwa na dawa za kuongeza makalio na hips ... nafkiri waanzilishi ni hao hao kama si wajapani basi watakuwa wachina .. maana ni biashara kubwa sana sikuhizi hapa kwetu bongo ... na bei yake ... u ta blow

eeeeeeh!!!! nani atanisaidia kwa hili je .... sidiria .. mbona tunavaa miaka nenda miaka rudi maziwa yetu hayaishi?????
 
Jamani huyu jamaa ameongelea sana social aspect za uvaaji wa nguo za kubana. lakina naomba nichangie scientific aspect, ukweli ni kua nguo za kubana hasa jeans suruali pamoja mambo mengine huongeza JOTO na FUKUTO ktk sehemu za siri hivyo inabadilisha hali halisi ya hewa huku kunako yaani temperature inabadilisha ph ya huko yaani acidic basic ratio ya huko hivyo sehemu inruhusu vijidudu Bacteria na fungus ambao naturally washindwa kuishi kutokana na ph kua unsuitable ila sasa wanatanua na kusababisha miwasho harufu mbaya na ikizid hata hupunguza hamu ya mapenzi. hiyo ni pamoja na chupi ambazo si cotton yaani hazinyonyi maji, g string chupoi za kinadada wenzangu nk.
natumai nimeeleweka........
 
Mimi nafikiri tusijadili masuala ya utafiti wa kitaalamu sisi tuangalie mila na utamaduni wetu je unaturuhusu kuvaa hayo mavazi ya namna hiyo?
Maana haya yote tunayoyafanya tunayaiga kuto nchi zilizoendelea nilipokwenda uingereza mara ya kwanza mwaka 1998 kwa mara ya kwanza nikaona mabinti huko wakivaa mavazi haya ya kubana ikiwa pamoja na kuacha matumboyao inje.
Na baadaye yakaenea huku kuanzia miaka 2000 sasa kimsingi mimi nafikiri tuige yaliyo na manufaa kwetu tusiige mambo ambayo hayaendani na utamaduni wetu
 
...clap! clap! clap!

...angeongezea uvaaji wa chachandu kiunoni na miguuni kuna mshepu zaidi mwanamke ama kwa hakika ningempigia na makofi zaidi!
 
Jamani huyu jamaa ameongelea sana social aspect za uvaaji wa nguo za kubana. lakina naomba nichangie scientific aspect,

No, ameongelea scientific aspect of it. Supposedly. Maswala ya mafuta kubwana na jeans chini ya mwili na kupandishwa juu kwenye moyo kusababisha magonjwa yana sound kama scientific kuliko social.

ukweli ni kua nguo za kubana hasa jeans suruali pamoja mambo mengine huongeza JOTO na FUKUTO ktk sehemu za siri hivyo inabadilisha hali halisi ya hewa huku kunako yaani temperature inabadilisha ph ya huko yaani acidic basic ratio ya huko hivyo sehemu inruhusu vijidudu Bacteria na fungus ambao naturally washindwa kuishi kutokana na ph kua unsuitable ila sasa wanatanua na kusababisha miwasho harufu mbaya na ikizid hata hupunguza hamu ya mapenzi. hiyo ni pamoja na chupi ambazo si cotton yaani hazinyonyi maji, g string chupoi za kinadada wenzangu nk.
natumai nimeeleweka........

Sio kweli.

Science yako inapostosha!

Ph ni kipimo cha concentration za Hydrogen ions (-log H+).

Joto linaongeza au kupunguza vipi Hydrogen ions ?

Tafadhali!
 
Nadhani doctor huyu ni "Professor Maji Marefu;" inaelekea chuo kikuu huria kina madokata wa ajabu kweli kweli. Maelezo yake hayana hata punje moja ya sayansi. Kama kweli ni Dokta mwenye sifa basi inawezekana alitoa mawazo haya akiwa kilabuni.
 
Back
Top Bottom