WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,459
- 952
Wanawake wavaao suruali watahadharishwa
na Esther Mbussi
WANAWAKE wanaovaa suruali aina ya jinzi na nguo za kubana, wako kwenye hatari ya kupata magonjwa hatari pamoja na kuharibika maumbo yao ya asili.
Dk. Amos Dadaoh wa Chuo Kikuu Huria Tanzania kinachotoa tiba kwa kutumia mimea, alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima. Aliongeza kuwa, suruali imetengenezwa kama vazi maalumu kwa wanaume.
Suruali imetengenezwa likiwa vazi maalumu kwa wanaume na kwamba mwanamke kwa maumbile yake anatakiwa kuvaa mavazi yanayompa nafasi yaani yasiyobana,alisema Dk. Dadaoh.
Alisema magonjwa wanayoweza kuyapata kutokana na mavazi hayo ni pamoja na kuota mizizi kwenye kizazi, moyo kuwa mkubwa na kushindwa kufanya kazi kama kawaida.
Alisema suruali ya kubana inahamisha mafuta kutoka kiunoni kwenda kwenye moyo na kizazi. Mafuta hayo husababisha mwanamke kushindwa kusukuma mtoto wakati wa kujifungua.
Mwanamke ambaye amezoea kuvaa suruali hasa aina ya jinzi ya kubana, pia yuko kwenye hatari ya kupoteza uhalisia wa umbo lake na kuwa kama simba - juu kuwa mpana na chini mdogo - kwani anabana mafuta kwenye mapaja ambayo yanaingia moja kwa moja kwenye kizazi na kwenye moyo, alisema Dk. Dadaoh.
Dk. Dadaoh alisema mwanamke kiasili ni wa pembe tatu na mavazi yake ni ya kuachia na yenye nafasi yasiyobana kwenye kati kati ya mapaja.
Ukiangalia Wakorea na Wajapani hawana kiuno wala makalio, wako bapa, ni kwa sababu ya tabia ya mazoea ya kuvaa suruali za kubana, alisema Dk. Dadaoh.
Pia alisema kina dada wenye mazoea ya kubana matiti, tumbo na kiuno pia wako kwenye hatari hii ya kupata magonjwa aliyoyataja hapo awali, kwani mafuta yanaganda kwa kukosa mwelekeo maalumu na ndiyo sababu wasichana wengi siku hizi wana matumbo makubwa (vitambi).
Alitoa ufafanuzi kuwa matatizo hayo yanayosababishwa na mavazi hayo, hayaleti madhara haraka kwa mvaaji kuvaa mara moja na kuathirika baada ya kuvua, bali huja taratibu kutokana na umri na mazoea ya kuvaa mavazi hayo kwa muda mrefu.
Your views please!