Mauzauza ya mke wangu

Junior Lecturer

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
904
526
¤ Kazi zote za nyumbani anamwachia dada wakazi.

¤ Kazini kwake amesha vuruga na wenzake karibia wote mpaka bosi wake.

¤ Kachukua mkopo 12m toka bank ya crdb hajanishirikisha mwezi wa tatu sasa nimeprove kwenye salary sleep zake.

¤ Hana muda nami tena tukiwa home yupo busy na raptop yake, nikitangulia kulala yeye anachelewa kuja kulala, akitangulia yeye busy tu na mambo yake.

¤ Mtaani amesha korofishana na watu kibao.

¤ Mtoto wetu na dada wakazi kila siku wana nambia wewe na mama hamko sawa myamalize.

¤ Hana story tena na ndungu zangu hawapigi simu hata wakimpigia hapokei akipokea majibu yake ni yamkato sana.

¤ Hashauriki hambiliki ,hanisikilizi kabisa.

¤ Majibu yake kwa sasa hanamuda wa kurumbana wala kumnyenyekea mwanaume mtumzima kama mimi.

¤ Sasa nafua mwenyewe nikiwepo nyumbani au dada wakazi.

¤ Ndugu hameshindwa kurudisha upendo unaooweka kila kukicha.

Nataka ni mnyoshe mkewangu wandoa naomba ushauri wenu.

Binafsi nataka niondoke nyumbani walau nikapumzike mbali na jiji hili for 6months.ushauri tafadhari.
 
Natoa ushauri huu kwa unyenyekevu sana tafadhali kabla ujaamua kutengana au kuachana na mkeo au mumeo onana na mwanasheria na wala sio padre au mchungaji au sheikh, utapata ushauri mzuri sana kuhusu usalama wako wewe na wa mali zako
 
Pole sana mkuu, usikimbie nyumba yako kaka, jaribu kutulia ufanye maamuzi sahihi
 
¤ Kazi zote za nyumbani anamwachia dada wakazi.

¤ Kazini kwake amesha vuruga na wenzake karibia wote mpaka bosi wake.

¤ Kachukua mkopo 12m toka bank ya crdb hajanishirikisha mwezi wa tatu sasa nimeprove kwenye salary sleep zake.

¤ Hana muda nami tena tukiwa home yupo busy na raptop yake, nikitangulia kulala yeye anachelewa kuja kulala, akitangulia yeye busy tu na mambo yake.

¤ Mtaani amesha korofishana na watu kibao.

¤ Mtoto wetu na dada wakazi kila siku wana nambia wewe na mama hamko sawa myamalize.

¤ Hana story tena na ndungu zangu hawapigi simu hata wakimpigia hapokei akipokea majibu yake ni yamkato sana.

¤ Hashauriki hambiliki ,hanisikilizi kabisa.

¤ Majibu yake kwa sasa hanamuda wa kurumbana wala kumnyenyekea mwanaume mtumzima kama mimi.

¤ Sasa nafua mwenyewe nikiwepo nyumbani au dada wakazi.

¤ Ndugu hameshindwa kurudisha upendo unaooweka kila kukicha.

Nataka ni mnyoshe mkewangu wandoa naomba ushauri wenu.

Binafsi nataka niondoke nyumbani walau nikapumzike mbali na jiji hili for 6months.ushauri tafadhari.

Mtwange yellow card, asipojirekebisha piga pyepyeeeeee then mtwange Red Card atoke ndani na wewe usifanya substation si unajua red card haina substation
 
uondoke uende wapi? Ongea na mke wako kwa undani ajue kabisa kwamba anachofanya hupendwezwi nacho,mwite mshenga wenu kama ikishindikana nyie wawili kuyamaliza, simama kwenye nafasi yako kama mwanaume,usiendekeze hayo mambo yake,mwambie sitaki kufuliwa nguo na mfanyakazi pasipo sababu maalumu,mweleze ukiwa nyumbani laptop ikae mbali.hataki aondoke yeye maana hataki ndoa,atakuwa ameichoka kwa kuishi maisha ya usingle wakati yupo kwenye ndoa.
 
Asha Ngedere kacharuka ndani ya Ndoa sasa mume akimwona anatetetemekaaaaaaa
 
Back
Top Bottom