Mke wangu amekubali nimuadhibu viboko vitano ili yaishe

Covax

Member
Feb 15, 2021
95
400
Nilivyosafari kuenda kwenye shughuli zangu za biashara takriban mwezi moja na nusu, jana nilirudi nikakuta mke wangu hayupo kasafiri na kuenda kwa Dada yake kukaa huko na nyumbani hamna mtu yeyote kuna giza kote, nikakagua nyumba yote na Kigari changu nikaona vyote viko salama nikamshukuru Mungu kwa hilo, nilienda kwa majirani labda wana taarifa yoyote kawachia na yuko wapi wakaniambia huyu hayupo nyumbani karibia mwezi na wiki niliduwaa

Nikampiga simu yake, mbona haupo nyumbani uko wapi? kaniambia iko kwa Dada yake Kinondoni nikamuomba anipe funguo wa nyumbani nipate kuingia na kupumzika, ka nialekeze nije nimsubirie kwenye kituo fulani nikaenda faster usiku huo nilivofika nikampigia simu takriban dakika 10 Dada mtu kajitokeza na funguo akanipa sikumsemesha kitu nikaondoka zangu mpaka nyumbani nikaingia ndani nikaona kila kitu kipo sawa ila kuna dalili za kuwa nyumba imekaa zaidi ya mwezi bila watu.

Sikumpigia simu tena kwasababu nilikuwa na hasira za kufa mtu nikajipa time nitulie kwanza, ila nilikua najiuliza huyu mwanamke nimfanye nini, kumtimua sio rahisi kwasababu ana kitoto changu kichanga mwaka moja na nusu kina nyonya, kwao hakuna mazingira mazuri kulea mtoto japo wanaishi Town ila mama aliekuwa nguzo ya familia alishafariki, Baba yake kashastaafu maisha yao kwa jumla sio, hawana uhakika wa kula milo mitatu, nyumba yao niya urithi tena wako zaidi ya watoto nane.

Mimi niko 38 na mke wangu iko 34 kumuacha manaake ni wakika wa kulea watoto wangu wawili utakua mgumu lakini kwasababu kipato chao ni duni sanaa, huyu mwanamke kanifanyia visa vingi kwanza ni muongo sana alishawahi kunificha kifo cha Mama yake kashaniongopea mambo mengi lakini kwasababu hayana madhara ya moja kwa moja na ya puuzia tu, nilifikia maamuzi mtoto wetu wa std 4 kumpeleke shule ya bweni sio kwamba nilipenda hapana kumuepusha kuiga tabia mbaya za mama ake.

Niseme tu mimi sina bahati katika kupata mke sahihi, kwasababu kabla ya huyu nilikua kuna Dada moja tume date nae takribani miaka 4 tukabahatika na kupata mtoto kilicho kuwa kimebakia nikuenda ku kujitamblisha kwao tu, ila yule demu hapana, alikuwa anasafiri almost kila weekend yani yeye na safari za kuenda makwao, aruhusi, mauleedi Dua, yalikua too much paka makonda wa ma busi ya kuenda Tanga wakaanza kumjua alikua anajua mabus yote ya route iyo duh nikaona huyu anifae kabisa nikampiga chini.....sasa this time nikashirikisha wazee wangu wanitafutie mke serious kwa kweli wazee hawakuchelewa wakaniambia tayari njoo muonane nikaenda nikaridhia na nikafanya utaratibu wa kumchukua, nilikaa nae kama mienzi mitatu duh nikaja kumkuta kumbe anakula mirungi (veve) nilichoka nikaona sina namna(mke wakutafutiwa ni shida). ndo nikaja kumpata huyu, ila nimemchoka vituko vyake ila sina la kufanya, pesa yangu elimu yangu havinisaidie kwasasa isipo kuwa uvumilivu tu.

Leo kama saa nane huyu bibie (mke) kanipigia simu kuniuliza hatima yake.....nikamwambia mie siwezi kuongea hi issue kwenye simu pata sehemu tuongea ana kwa ana akanielekeza pa kumkuta tuyaongee, nikaendesha ki (baby walker) changu paka pale, nilivofika akaanza kuwa mkali najifanya kuleta mambo ya nyuma nikawa kimya kwasabb alilenga kuniondoa kwenye mada, tu nikamuuliza anataka lipi kajibu kurudi nyumbani kwanini ulipacha eti ana paogopa duh nikamuuliza sasa ukurudi unaenda kukaa nani kwasababu baada ya wiki moja naenda kusafiri tena utapakimbia? Akasema hapana eti hatarudia. Ila huyu mama muongo mambo mengi anaapa ila anayarudia tu.

To cut the story short nilimpa option tatu achague moja. Kum -suspend kwa miezi mitatu akiwa kwao au aombe talaka au nimpige viboko vitano. Kaamua nimchape viboko vitano yaishe. ila personally am not a violent man na sijawahi kuchapa mke yeyote hili jambo lime nipa wakati mgumu sanaa, namimi sitaki unafiki nataka nafsi yangu iridhike, akifanya adhabu yangu yoyote.

Wakuu ndo nimemfikisha home sina hata 30minutes sijui ndo nimchape au kuna adhabu nyingine zaidi ya hiyo mnishauri, ila kumbukeni huyu mwana mke ni msumbufu sanaa muonģo ila sijawahi kupata ushahidi wowote wa uzinzi kwake. Naomba ushauri na uzoefu wenu ahsanteni.
 

bilu97

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
836
1,000
Kama aliondoka kwa sababu ya kuogopa fresh mana angeweza hata kuingiza wanaume hapo ! kama una uhakika anakupenda na ania ya kweli ya kuishi na wewe basi kuhusu uwongo muelekeze tu hupendi ila kama unahisi anakusaliti fanya uchunguzi kama kweli piga chini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom