Shut up and move on!....so what?.
...unaonaje tukihamishia mazungumzo yetu private?
Shut up and move on!....so what?.
Scenario 2
Tukisema alikua na biashara ingine, Tungependa kuifahamu ina mtaji kiasi gani na aliupata wapi. Pili mrahaba aliokuwa anaupata kutoka kwenye kampuni alilipa kodi????? Je hiyo company/hiyo biashara ingine auditing report zake zinaonyesha faida ama hasara?????? kama Faidi je zililipa kodi???? Je walideclare hiyo biashara yao wakati wakiwa serikalini????
...unaonaje tukihamishia mazungumzo yetu private?
Oh no i don't like private...siyo safe kabisa....public is good kama unashika inakuwa powa sana then unaend up apologizing like Jesse jacson.
Watuhumiwa EPA kurejeshewa fedha
Neema Mgonja
Daily News; Thursday,December 04, 2008 @21:15
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imeamuru baadhi ya washitakiwa katika kesi za ufisadi waliokuwa wametoa fedha taslimu kwa ajili ya kupata dhamana, warudishiwe fedha zao.
Mawakili wa washitakiwa katika kesi inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Hezron Mwankenja, waliomba kwa vile tayari Mahakama Kuu ilishalegeza masharti ya dhamana dhidi ya mshitakiwa mmoja Iman Mwakyosa, basi uamuzi huo utekelezwe kwa washitakiwa wote.
Katika kesi hiyo, washitakiwa ni wanne, Rajab Maranda, Esther Mary Komu, Mwakyosa na Bosco Kimela, ambao wote walishitakiwa kwa madai ya kuiba Sh milioni 207. Mawakili wa washitakiwa hao, Makaki Masatu aliomba kwa vile tayari Mahakama Kuu imelegeza masharti kwa Mwakyosa, ni vyema wateja wengine pia wakalegezewa masharti hayo.
Mwakyosa ametoka kwa masharti ya kutoa fedha taslimu Sh milioni 26 au hati ya thamani ya kiasi hicho. Awali katika kesi hiyo, Mwakyosa na wenzake waliamriwa kila mtu kutoa Sh milioni 104 fedha taslimu ili wapate dhamana. Uamuzi huo ulimwia mgumu Mwakyosa na hakutimiza masharti hayo, hali iliyomlazimu apeleke maombi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuomba kulegezewa masharti ili aweze kutoa hati.
Ombi hilo lilikubaliwa na mahakama hiyo na kupunguza kiasi cha fedha kutoka Sh milioni 104 hadi Sh milioni 26 au kutoa hati ya thamani ya kiasi hicho. Jana kesi hiyo ilipokwenda kwa ajili ya kutajwa, Hakimu Mwankenja alikubaliana na maombi hayo ya washitakiwa na akaamuru mahakama kuwarudishia fedha zao washtakiwa ambao tayari walishatoa fedha taslimu na wako nje kwa dhamana.
Kutokana na maombi ya mawakili, naamuru washitakiwa wengine nao warudishiwe fedha zao ili watoe kiasi ambacho kimetajwa na Mahakama Kuu, alisema Mwankenja. Washitakiwa ambao walishatoa zaidi ya Sh milioni 100 na kupata dhamana ni Maranda, Komu na Kimela.
Kutokana na amri hiyo, washitakiwa hao sasa kila mmoja atarudishiwa fedha zake zote na watatoa hati au Sh milioni 26. Jana Maranda na Bosco waliwasilisha hati, ila ni hati ya Bosco pekee ilipokelewa wakati hati aliyowasilisha Maranda haikuwa na barua kuthibitisha hati hiyo, hivyo mahakama kutoikubali hadi pale itakapoambatanisha na barua. Esther kwa upande wake, wakili wake hakuwapo hivyo mahakama ilimwelekeza kuwa awasilishe hati hiyo siku kesi hiyo itakapoenda kusikilizwa Januari 20.
Babu wewe naoye unazidi kuboa
umeshindwa vipi kutuletea orodha badala ya hizi articles?
Inakuaje hizi nyumba walizoweka thamani zilikuwa MILLION 5 wakati wananunua SERIKALINI na leo hii baada ya miaka mitano zina thamani YA MAMILLION?
It doesn't make any sense at all. WHO WAS THE APPRAISER? MKAPA?
...kama ambavyo viongozi wote wanavyotakiwa kuorodhesha mali zao?
Date::12/4/2008
Kambi ya upinzani wahoji mabilioni ya Mramba, Yona
Na Salim Said
Mwananchi
SIKU chache baada ya mawaziri wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona, kutolewa gerezani kwa kuwasilisha hati za mali zenye thamani ya jumla ya Sh6.2 bilioni kama dhamana, wapinzani wameeleza kushtushwa na kiwango hicho cha mali kumilikiwa na watumishi wa serikali.
Hati za mali za Mramba, ambaye pamoja na Yona wameshtakiwa kwa makosa ya kutumia vibaya ofisi wakati wakiwa mawaziri, ni zile za nyumba yake na za washirika wake zenye thamani ya Sh3.14 bilioni, wakati hati za mali za Yona zilikuwa ni nyumba zake tatu zenye thamani ya jumla ya Sh3 bilioni.
Kiwango hicho cha thamani za mali kimewashtua wanasiasa wa upinzani.
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) na chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamehoji uhalali wa mtumishi wa umma kumiliki mali yenye thamani ya zaidi ya Sh3 bilioni.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, viongozi wa Chadema na CUF walisema mshahara wa mtumishi wa umma unaeleweka.
Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa CUF, Ismail Jussa alisema ingawa dhamana ni haki yake, lakini Yona ameushangaza umma kumiliki mali yenye thamani hiyo ya fedha.
"Kimsingi, dhamana ni haki yao lakini tatizo linakuja pale mtumishi wa umma anapoweza kujidhamini mwenyewe kwa mali yenye thamani ya mabilioni ya shilingi," alionyesha mshangao Jussa.
Kwa mujibu wa Jussa, kitendo cha waziri huyo mstaafu kujidhamini kwa mali ya mabilioni hayo kinaweka maswali mengi dhidi ya viongozi wa serikali.
Jussa, ambaye ni mwanasheria kitaaluma, pia alihoji kasi ya kusikilizwa kwa rufaa yao wakati kuna watu wengi wamekata rufaa, lakini bado wanaendelea kusota rumande bila rufaa zao kusikilizwa haraka.
Mimi, kama mwanasheria sioni tatizo la kupewa dhamana, lakini rufaa yao na ile ya serikali dhidi ya walimu inaibua maswali mengi ambayo majibu yake ni magumu kuhusiana na uhuru wa mahakama, alisisitiza Jussa.
Naye afisa habari wa Chadema, David Kafulila alisema haiwezekani kwa mtumishi wa umma kumiliki mali za namna hiyo.
Hizo mali za Sh2.9 bilioni ni sehemu tu ya mali za Yona... kachomoa tu kidogo ili ziweze kumtoa nje, lakini alizipata kwa mshahara gani hata kama ni waziri, alihoji Kafulila.
Alisema mazingira kama hayo ya kutatanisha kwa kiongozi kumiliki mali za thamani hiyo, ndiyo yaliyovifanya vyama vya upinzani nchini kutaka uhakiki wa mali zote za viongozi wa serikali pamoja na akaunti zao za benki, lakini walikataliwa.
Kafulila alitoa mfano wa waziri wa zamani wa miundombinu, Andrew Chenge ambaye alijiuzulu kutokana na kuhusishwa na kashfa ya ununuzi wa rada na kubainika kuwa ana akaunti yenye dola 1 milioni nje ya nchi, akisema ndilo lililojitokeza kwa mawaziri hao wawili.
Kama mtu anaweza kumega sehemu tu ya mali yake yenye thamani ya 2.9 bilioni na kutoa kama dhamana mahakamani, kwa nini asiziite Sh.1 bilioni vijisenti, alihoji Kafulila.
Tunataka uhakiki wa mali za viongozi wa serikali kufanyika ili kugundua madudu ya kifisadi, alisema Kafulila.
Aliongeza kwamba rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa alitangaza mali zake wakati anaingia madarakani, lakini aliondoka kimyakimya huku Rais Jakaya Kikwete akingia kimyakimya pasipo kujulikana mali zake.
Kuna utata mkubwa kuhusu tathmini ya mali hizo kama ilifanywa na wataalamu katika mambo ya valuation. Hata katika majiji yenye gharama kubwa za maisha kama New York, London na Paris n.k. nyumba haziappreciate haraka kiasi hicho. Naona wakubwa walishaamua kuwakingia kifua. Kuna dalili ya hii kesi itajaa usanii wa hali ya juu na matokeo yake jamaa kuonekana hawana hatia. Maana si kitu cha kawaida hata kidogo Waziri wa mambo ya ndani kuwatembelea watuhumiwa wakiwa rumande na maelezo aliyoyatoa hayakuwaridhisha Watanzania wengi wanaofuatilia sakata la mafisadi hawa. Tusubiri tuone mwelekeo wa kesi hii.
Inakuaje hizi nyumba walizoweka thamani zilikuwa MILLION 5 wakati wananunua SERIKALINI na leo hii baada ya miaka mitano zina thamani YA MAMILLION?