Ukidhulumu lazima udhulumiwe

Ukidhulumu lazima udhulumiwe

Samia atosha tukutane2030

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
17,605
Reaction score
49,542
Tangu CAG aanze kusoma report hakuna ripoti iliyoonyosha matumizi ya fedha na mali za serikali kuwa 100/100 , namaanisha hakuna ripoti iliyoonyosha matumizi ya fedha za umma au mali za umma kwenda sawa kwa 100%.

Kila mwaka lazima watumishi waonekane kuweka dhuluma na upigaji wa fedha za umma.
Hii ni kanuni ya kiroho, ili serikali isiibiwe ni vyema nayo iache kudhulumu watumishi wake.

Kama mtumishi anakwenda likizo mwaka 2020 pesa ya nauli analipwa 2024 au mpaka sasa hajalipwa maana yake ni dhuluma imefanyika.

Serikali yenye matrilioni ya fedha inamdhulumu mtumishi mnyonge nauli na laki 2, 3 au 4.
Serikali inawadhulumu watumishi wake kwa maslahi duni.

Mpaka dunia itaisha serikali hii kila itakaposomwa ripoti ya CAG lazima wakute mahali imepigwa.
Hii itakoma siku serikali itakaposema sasa basi hakuna dhuluma tena kwa watumishi.

Mtumishi mmoja analipwa laki 6 huku mwenzake wa taasisi B analipwa milioni 1 laki 8 huku wote wana elimu sawa na wameajiriwa mwaka mmoja.

Serikali (viongozi) wasipanic watulie. Dawa ya dhuluma ni dhuluma.
 
Kwanini hatua hazichukuliwi?
Miaka yote 3 hakuna hatua kabisa!
Ndio maana wizi na ufisadi unashika kasi kwani hakuna hatua!
Au ndio ile "kula sawa na urefu wa kamba"?
RIP Magufuli
 
ananiambia walichukua majivu na kuni wakaweka kwenye sururia la makande ambayo Huwa tunanunua jero tu "tena anaweka na kachumbali" aiseee Roho iliniuma sana.
 
Back
Top Bottom