Mauzauza ya EPA

Alipoulizwa kama ni sahihi kwa Bw. Mgonja kutohusishwa kwenye mashitaka yanayomkabili, Bw. Mramba alidai wadhifa wa uwaziri ni wa kisiasa na mtendaji ni katibu mkuu ndio maana yanaibuka maswali mengi.

- The dataz sasa ni kwamba majaji wote muhimu wa hizo kesi huu ni msimu wao wa likizo za mwaka, kwa hiyo hawapo mjini wanarudi Januari ndio mchezo utaendelea, cha muhimu sasa ni sisi wananchi kutafuta habari zaidi wahusika na ufisadi wapo wapi? Wako huru?
 
Mauzauza ya EPA

na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

UTATA wa zilipo fedha zilizorejeshwa na kampuni zilizoiba fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), umeendelea kuigubika nchi, baada ya kubainika kuwa fedha hizo hazijaingizwa kwenye mfuko ulioelekezwa na Rais Jakaya Kikwete wakati akilihutubia Bunge, Agosti 21 mwaka huu.

Fedha hizo ambazo ni zaidi ya sh bilioni 70, zilitakiwa ziende Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), ambapo zingefunguliwa dirisha maalumu, lenye jukumu la kutoa mikopo kwa wakulima ambao kwa miaka mingi wamekosa fursa hiyo.

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumapili, umebaini kuwa fedha hizo zimehifadhiwa katika akaunti maalumu ambayo mpaka hivi sasa maelezo yake bado yamegubikwa na utata, kwa sababu kila ofisa wa Wizara ya Fedha na Uchumi aliyeulizwa juu ya akaunti hiyo, ameshindwa kutoa jibu linaloeleweka.
Tangu awali baadhi ya watu walionyesha wasiwasi wao kuhusu urejeshaji wa fedha hizo kama ni kweli zimerejeshwa au ilikuwa mbinu ya kisiasa ya serikali kutaka kuzima joto la wananchi, wapinzani na wahisani waliotaka fedha hizo zirejeshwe na watuhumiwa wafikishwe katika mikono ya sheria.

Watu hao waliweka wazi msimamo wao kuwa fedha hizo hazikurejeshwa bali ilikuwa ni janja ya serikali ili waweze kupata misaada kutoka kwa wafadhili ambao awali walitishia kutochangia bajeti ya serikali mpaka majibu sahihi na hatua za wizi wa EPA zichukuliwe.

Shinikizo hilo inadaiwa ndilo lililomfanya Rais Jakaya Kikwete kuamua kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daudi Ballali, pamoja na kuunda timu ya uchunguzi chini ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, baada ya mkaguzi wa nje, Ernst & Young, kuthibitisha kuwapo kwa wizi katika akaunti hiyo, unaofikia kiasi cha sh bilioni 133.

Mkurugenzi wa Benki ya Rasilimali (TIB), William Mlaki, hivi karibuni alikaririwa na vyombo vya habari kuwa fedha hizo hadi sasa hawajazipokea.

Alisema inawezekana serikali inajiandaa kuwapelekea fedha hizo ambazo Rais Jakaya Kikwete alishaweka wazi dhamira ya serikali yake kuzipeleka TIB ili ziwasaidie wakulima.

"Mpaka sasa fedha za EPA, bado hazijaingia kwetu na si jukumu letu kuulizia fedha hizo zitakuja lini, kazi yetu ni kuzipokea na kuratibu zoezi la utoaji mikopo kwa wakulima," alikaririwa Mlaki.


Kauli hiyo ya Mlaki, inazidisha utata kuhusu ukweli wa urejeshaji wa fedha za EPA ambazo uchotwaji wake unahusishwa na matumizi ya uchaguzi mkuu uliopita.

Inadaiwa kuwa mbinu za kuchota fedha hizo, zilifanywa na viongozi wa juu wa Serikali ya Awamu ya Tatu kwa kushirikiana na mwanasiasa na mfanyabiashara maarufu nchini ili zikisaidie Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu uliopita.

Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, tena kwa nyakati tofauti, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba na Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha, Amos Makala, wamekanusha chama chao kuhusishwa na wizi huo.

Mfanyabiashara huyo ndiye anayeaminika alikuwa mmiliki halali wa Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited iliyochota sh bilioni 40, lakini hadi hivi sasa hajafikishwa mahakamani au kutajwa mbele ya umma.

Kutotajwa kwa mfanyabiashara huyo kunatokana na ukweli kuwa ndiye anayejua siri yote ya Kagoda na viongozi waliomuagiza kuzichota fedha hizo na hata matumizi yake pamoja na kujua nani kapata kiasi gani na kwa kazi gani.

Kwa hali ilivyo, Kagoda ndiyo kampuni inayoonekana kuitikisa nchi kama wamiliki wake watatajwa na kufikishwa mahakamani, kwani hawatakubali kushitakiwa peke yao bila kuwataja viongozi waliowatuma kufanya wizi huo.

Hali hiyo ndiyo iliyomfanya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakhia Meghji, kutoa ufafanuzi kwa umma kuwa fedha zilizochotwa zilitumika kwa mambo ya usalama na si ufisadi kama ambavyo baadhi ya wanasiasa, akiwemo Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa, walivyokuwa wakisema.

Msumari wa moto juu ya utata wa urejeshwaji wa fedha za EPA na ufisadi hivi karibuni ulishindiliwa na mfanyabiashara maarufu nchini na mwachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jafar Sabodo, ambaye alisema serikali inafanya mchezo wa kuigiza na haina nia thabiti ya kutatua matatizo ya rushwa.

Sabodo ambaye ni rafiki wa karibu wa marehemu Mwalimu Nyerere na mfadhili wa mfuko wa taasisi ya Mwalimu Nyerere na CCM, alifikia hatua ya kusema yuko tayari kukisaidia chama chochote cha upinzani katika uchaguzi ujao, kuiangusha CCM madarakani, kwa madai kuwa imeshindwa kuondoa tatizo la rushwa nchini.

Wachambuzi wa masula ya siasa wanadai kupandishwa mahakamani kwa mawaziri wawili ya serikali iliyopita Basil Mramba (Fedha) na Daniel Yona (Nishati na Madini), ni mpango wa kuwasahaulisha wananchi juu ya mwenendo wa kesi ya EPA, hasa kuendelea kufikishwa mahakamani kwa watuhumiwa wengine.

Mpango huo uliasisiwa kutokana na joto la wananchi kutaka wamiliki wa Kampuni ya Kagoda inayohusishwa na wafanyabiashara, wanasiasa maarufu na wakongwe nchini, kuzidi kushika kasi kiasi cha kumfanya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuweka bayana kuwa joto hilo likizidi, wamiliki wake watajulikana.

Wadadisi hao wanaendelea kubainisha kuwa mpango huo kwa kiasi fulani, umefanikiwa, kwani watu walihamisha macho na masikio yao kutoka EPA na kuhamia kwa Yona na Mramba, ambao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salam kwa kosa la kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya sh bilioni 11.7, kwa kutoa misamaha ya kodi kiholela katika sekta ya madini.

Wakati wingu zito likiwa limetanda kuhusu mahali zilipo fedha za EPA, kuna tetesi kwamba fedha hizo ndizo zilizotumika kulipa madai ya walimu ambao miezi miwili iliyopita walitishia kugoma nchi nzima kushinikiza kulipwa fedha zao za malimbikizo zinazofikia sh bilioni 16.
 
Mbona tuliambiwa Sabodo nae ni fisadi mkumbwa. Tafuteni ukweli kwani kila mtu anataka kumchezea mwenzake lakini watanzania si mambwege tena.
 
Hivi ndio vile viini macho wengi tulikuwa tunahofia. Nakumbuka Mh. Slaa alitaka fedha hizi zinazorudishwa zihakikiwe na bunge na kupangiwa matumizi na bunge. JK wa kujua kwamba ulikuwa ni mchezo wa mazingaombwe akaiteka mada na kudai fedha zitarejeshwa kwake na yeye ndio atazipeleka huko kwenye kilimo. Wasiwasi wa watu wengi ilikuwa ni kwamba fedha hizi hazijarudishwa ndio maana raisi akaingilia.

Yetu macho.
 
Utendaji wa serikali ya Jakaya inanichosa kabisa. Mgonja na mwenzie Mrisho inajulikana kabisa kuwa wanatuhumiwa najamii kuwa ni mafisadi; sasa badala ya kuwachukulia hatua za kisheria haraka iwezekanavyo tumewachelewesha mpaka sasa tunaambiwa wamestaafu kwa mujibu wa sheria. Hii ina maana kwamba hawa jamaa juu ya kutumia vyeo vyao kibadhilifu pia itatubidi sisi walipa kodi tuwalipe pension kila mwezi.Nadhani lakufanya sasa ni kuwanyang'anya pasi zao za kusafiria kabla hawajatoroka na wapandishwe kizimbani mapema iwezekanavyo.
 
Shalom na habari toka Dari salama ni njema na sikukuu yetu .
Nimeona nirudi jamvini ambako najua huwa hapakosi majawabu .Nimefuatilia kesi za EPA na sasa Mramba na Yona .Mimi kwa muona naona zote zina mwekeleo mmoja japokuwa sasa waendesha mashitaka yaani PCCB wameamua kutuzuga .Lakini pia katika hilo wanatuzuga zaidi kwa kuziita wizi na kutumia madaraka vubaya .
Kwa muona wangu naona kesi hizi ni kubwa na zilipaswa kuwa za Kuhujumu Uchumi wa Tanzania .Je nina kosea ama kesi hazijawa nna vingezo vya kuzifanya ziwe classfied kwenye Uhujumu Uchumi ?

Msaada wako unatakiwa kunielewesha tafadhali .
 
Shalom na habari toka Dari salama ni njema na sikukuu yetu .
Nimeona nirudi jamvini ambako najua huwa hapakosi majawabu .Nimefuatilia kesi za EPA na sasa Mramba na Yona .Mimi kwa muona naona zote zina mwekeleo mmoja japokuwa sasa waendesha mashitaka yaani PCCB wameamua kutuzuga .Lakini pia katika hilo wanatuzuga zaidi kwa kuziita wizi na kutumia madaraka vubaya .
Kwa muona wangu naona kesi hizi ni kubwa na zilipaswa kuwa za Kuhujumu Uchumi wa Tanzania .Je nina kosea ama kesi hazijawa nna vingezo vya kuzifanya ziwe classfied kwenye Uhujumu Uchumi ?

Msaada wako unatakiwa kunielewesha tafadhali .

Jamani hakuna hata mjuvi mmoja wa jambo hili anifungue macho ?
 
Mkuu, hizo kesi ni sehemu ya usanii. Ukirejea sheria, hayo makosa waliyoshitakiwa nayo ni madogo sana ukilinganisha na uzito wa kitu kilichofanyika. Na tna nadhani kuna hesabu za kuwatoa hapo baadaye kwani mashitaka waliyoshitakiwa nayo ni ragisi kujitetea, mathalani, msingi wa mashitaka ya Yona na Mramba ni kuwa walifanya maamuzi mabaya walipokuwa madarakani. lakini ipo sheria inayompa waziri uhuru wa kufanya maamuzi kwa kuzingatia busara zake. sasa unawezaje kusema kuwa busara zao (walizotumia kufanya maamuzi) ni makosa? Ni uzugaji tu mkuu
 
Japokuwa sijapata jibu lakini umenisaidia ama kwenye Mramba na Yona kuna mahali nimesikia mwendesha mashitaka anasema ushahidi haujakamilika .Lakini Hosea alisema kuna kesi 5 kubwa na zime kamilika je kama hakuna ushahidi kwa nini wamewapeleka mahakamani ?
 
Kesi za mafisadi zinatakiwa ziwe both jinai na uhujumu uchumi...Huwezi kuhujumu uchumi kama hufanyi hivyo kwa kupitia jinai...
 
Shalom na habari toka Dari salama ni njema na sikukuu yetu .
Nimeona nirudi jamvini ambako najua huwa hapakosi majawabu .Nimefuatilia kesi za EPA na sasa Mramba na Yona .Mimi kwa muona naona zote zina mwekeleo mmoja japokuwa sasa waendesha mashitaka yaani PCCB wameamua kutuzuga .Lakini pia katika hilo wanatuzuga zaidi kwa kuziita wizi na kutumia madaraka vubaya .
Kwa muona wangu naona kesi hizi ni kubwa na zilipaswa kuwa za Kuhujumu Uchumi wa Tanzania .Je nina kosea ama kesi hazijawa nna vingezo vya kuzifanya ziwe classfied kwenye Uhujumu Uchumi ?

Msaada wako unatakiwa kunielewesha tafadhali .

Bwana Lunyungu,

Natumaini Unaendelea vizuri kushereheka na sikukuu ya Idd,

Hili suala nilishaligusia hapo nyumba kwamba hawa jamaa walitakiwa washtakiwe kwa sheria ya kuhujumu uchumi ya mwaka 1984(Economic and Organised Crime Control Act, 1984 (No. 13 of 1984)[media]http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/13-1984.pdf[/media]. Unajuwa wakati mwingine tunachezea shele na hawa 'wakubwa'.

Bwana, Lunyungu soma kifungu cha 25- DPP ndo mwenye kauli ya mwisho kuhusu mashtaka ndani ya sheria hii.

Shadow.
 
Japokuwa sijapata jibu lakini umenisaidia ama kwenye Mramba na Yona kuna mahali nimesikia mwendesha mashitaka anasema ushahidi haujakamilika .Lakini Hosea alisema kuna kesi 5 kubwa na zime kamilika je kama hakuna ushahidi kwa nini wamewapeleka mahakamani ?

Huo ni sehemu ya usanii uliofanywa katika hili. Hosea aliahidi tangu mwaka jana akisema anawapa wale krismas tu afanye vitu vyake. krismas nyingine imefika bado hajakamilisha ushaidi!
 
Back
Top Bottom