Mauzauza ya EPA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauzauza ya EPA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 4, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,878
  Likes Received: 83,359
  Trophy Points: 280
  ...kama ambavyo viongozi wote wanavyotakiwa kuorodhesha mali zao?

  Date::12/4/2008
  Kambi ya upinzani wahoji mabilioni ya Mramba, Yona
  Na Salim Said
  Mwananchi

  SIKU chache baada ya mawaziri wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona, kutolewa gerezani kwa kuwasilisha hati za mali zenye thamani ya jumla ya Sh6.2 bilioni kama dhamana, wapinzani wameeleza kushtushwa na kiwango hicho cha mali kumilikiwa na watumishi wa serikali.

  Hati za mali za Mramba, ambaye pamoja na Yona wameshtakiwa kwa makosa ya kutumia vibaya ofisi wakati wakiwa mawaziri, ni zile za nyumba yake na za washirika wake zenye thamani ya Sh3.14 bilioni, wakati hati za mali za Yona zilikuwa ni nyumba zake tatu zenye thamani ya jumla ya Sh3 bilioni.

  Kiwango hicho cha thamani za mali kimewashtua wanasiasa wa upinzani.

  Baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) na chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamehoji uhalali wa mtumishi wa umma kumiliki mali yenye thamani ya zaidi ya Sh3 bilioni.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, viongozi wa Chadema na CUF walisema mshahara wa mtumishi wa umma unaeleweka.

  Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa CUF, Ismail Jussa alisema ingawa dhamana ni haki yake, lakini Yona ameushangaza umma kumiliki mali yenye thamani hiyo ya fedha.

  "Kimsingi, dhamana ni haki yao lakini tatizo linakuja pale mtumishi wa umma anapoweza kujidhamini mwenyewe kwa mali yenye thamani ya mabilioni ya shilingi," alionyesha mshangao Jussa.

  Kwa mujibu wa Jussa, kitendo cha waziri huyo mstaafu kujidhamini kwa mali ya mabilioni hayo kinaweka maswali mengi dhidi ya viongozi wa serikali.

  Jussa, ambaye ni mwanasheria kitaaluma, pia alihoji kasi ya kusikilizwa kwa rufaa yao wakati kuna watu wengi wamekata rufaa, lakini bado wanaendelea kusota rumande bila rufaa zao kusikilizwa haraka.

  "Mimi, kama mwanasheria sioni tatizo la kupewa dhamana, lakini rufaa yao na ile ya serikali dhidi ya walimu inaibua maswali mengi ambayo majibu yake ni magumu kuhusiana na uhuru wa mahakama," alisisitiza Jussa.

  Naye afisa habari wa Chadema, David Kafulila alisema haiwezekani kwa mtumishi wa umma kumiliki mali za namna hiyo.

  "Hizo mali za Sh2.9 bilioni ni sehemu tu ya mali za Yona... kachomoa tu kidogo ili ziweze kumtoa nje, lakini alizipata kwa mshahara gani hata kama ni waziri," alihoji Kafulila.

  Alisema mazingira kama hayo ya kutatanisha kwa kiongozi kumiliki mali za thamani hiyo, ndiyo yaliyovifanya vyama vya upinzani nchini kutaka uhakiki wa mali zote za viongozi wa serikali pamoja na akaunti zao za benki, lakini walikataliwa.

  Kafulila alitoa mfano wa waziri wa zamani wa miundombinu, Andrew Chenge ambaye alijiuzulu kutokana na kuhusishwa na kashfa ya ununuzi wa rada na kubainika kuwa ana akaunti yenye dola 1 milioni nje ya nchi, akisema ndilo lililojitokeza kwa mawaziri hao wawili.

  "Kama mtu anaweza kumega sehemu tu ya mali yake yenye thamani ya 2.9 bilioni na kutoa kama dhamana mahakamani, kwa nini asiziite Sh.1 bilioni vijisenti," alihoji Kafulila.

  "Tunataka uhakiki wa mali za viongozi wa serikali kufanyika ili kugundua madudu ya kifisadi," alisema Kafulila.

  Aliongeza kwamba rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa alitangaza mali zake wakati anaingia madarakani, lakini aliondoka kimyakimya huku Rais Jakaya Kikwete akingia kimyakimya pasipo kujulikana mali zake.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,595
  Likes Received: 5,776
  Trophy Points: 280
  Swala lingine zinalipiwa kodi kwa ufasaha???????????
   
 3. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kusema kweli me like everybody else nimeshangazishwa sana na mtu wa selikali kuwa na thamani kubwa hivyo ya nyumba....The thing is my dad amefanya serikalini enzi hizo za nyerere na Mwinyi na alikuwa mtiifu sana i wonder how come hana nyumba za thamani kubwa hivyo?....whats going on people watu wengi wanahangaika na maisha tanzania na kuna watu wengine wanatajirika kwa kutumia migongo yao this is not fair at all.
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Babu wewe naoye unazidi kuboa

  umeshindwa vipi kutuletea orodha badala ya hizi articles?
   
 5. C

  CottonEyeJoe JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2008
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Labda mzee hakutaka kuji invovle na biashara zingine zakumuongezea kipato, inawezekana vile vile hakupenda kuji involve kwenye biashara ya real estate, the fact that one man has and another doesnt should not be a reason for you to suspect that they earn those assets illegally, thats a ujamaa way of thinking, bottom line is some ppl embraced capitalism faster than others whilst others remain stuck in the socialism era, now inspite of their wrong doings how can that be the fault of Yona and Mramba???
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Dec 4, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,135
  Trophy Points: 280
  ..halafu wananchi hatuelezwi ni mali gani zilizotumika kupata dhamana hiyo.

  ..kuna matatizo/mapungufu makubwa sana jinsi waandishi wetu wanavyoandika kuhusu kesi hii.
   
 7. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  As you know back in days real estate was not a big deal as now...Hata kama ukinunua nyumba cost yake ilikuwa ndogo sana...ukilinganisha na sasa hivi what i hear ni kwamba mtu ananunua kiwanja for million 30 tshillings hizo ni almost 40,000 dollars.I think enzi hizo watu walikuwa wanaendesha nchi kiuhalali compared to now.

  Yona na mramba wametoka na dhamana ya 6.2 billions yenye thamani ya nyumba zao.imagine mtu wa serikali ana nyumba yenye thamani ya billions of money while me i am working hard everyday lakini sipati hela hiyo...i also need to have good life nime husstle kiasi cha kutosha na nimejaribu kuwa innocent like my dad ila now i am totally tired nahitaji deal pia aaah this is not fair at all i need to upgrade pia,
   
 8. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Hivi hiyo sheria ya viongozi kutangaza mali zao ipo vipi Tanzania? Anayejua atujulishe vizuri, na hizo records zipo wapi? Kama Kikwete hakutangaza mali maana yake sio sheria ni hiari ya mtu, right?

  Hii habari kusema ukweli sijapenda ilivyokaa, imeandikwa kiwivu wivu na kimajungu. Kuwa mtumishi waserikali haina maana kuwa huna shughuli zengine, kama kweli hawakuzitaja hizo mali hapo sawa, lakini mwandishi hajatuonyesha hivyo.
  Ndio 3 Bil ni hela nyingi, lakini sio nyingi kiasi hicho, mtu wa miaka 60+ anaweza kutengeneza hizo hela in his lifetime.
   
 9. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hahaha... nyie mnacheza... Mramba anakaa Mawenzi Road Masaki.. His house has to be worth not less than a billion. tena that compound id kinda big so labda 1.5 million dollars (kiwanja tuu) na nauhakika kauziwa nyingine ya serikali for aroud 30-35 million lakini its worth not less than a billion pia... hizo legit. sasa plus madili, jamaa anakisu kinooomaaa.. somewea around 20million Dollars.. wewe Kelly sijui hata ufanyeje u will probably never get there. Accept it.. Chakuchekesha, mke wake mwalimu wa sekondari (ya serikali) haha. Tanzania nchi ya ajabu. Lakini mimi kwakweli Mkapa kuwauzia watumishi wa serikali nyumba (and i dont mean mawaziri) was not such a bad thing.. its about time watu weusi angalau nao wawe na value.. sio wahindi tuu
   
 10. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,230
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Mie sishangai hao jamaa maeneo yao kuwa na thamani kubwa hivyo maana ardhi inapanda thamani kila kukicha Dar eneo dogo tu utaambia milioni tano kumi, sasa kama mtu ana kuwanja kwa mahekta na kina mali zingine zenye thamani kama nyumba kwanini kisifikishe thamani ya milion 400 na ziadi. Kiwanja kariakoo huna bilions hujaamisha mtu tena padogo tu pa kujenga jengo la kubanana.

  wana haki ya kuweza kujidhamini na hizo mali zao. sasa kama nazo zilipatikana kifisadi hapo sitii neno. Lakini usifadi ndio kinga ya fisadi hilo lisisahaulike
   
 11. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  sasa kwa nini nisifike huko?Kama yeye kacheza deal hadi kafika hapo alipo sasa hivi why not me?.Ni kitu gani kitakachonifanya na mimi nisifike hapo alipo you never know...sema mimi nacheza ma deal legit ndiyo maana ina take a while to get where he is i guess nikicheza illegal deals yeah i will definetely make it within 6 month.....i promise you,
   
 12. K

  Koba JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...eti i promise you,wewe njaa zitakuua usipoangalia na cha kulia lia hapa oooh mimi mwaminifu ...ooohh mimi deal legit,maharage,chumvi na maji,who cares? njaa ni zako kula mwenyewe!
   
 13. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,595
  Likes Received: 5,776
  Trophy Points: 280
  mada imeingiliwa?
   
 14. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #14
  Dec 4, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ndugu kwang nimekuvumilia ila nimechoka..... Hushangazwi na 3Billion.

  Scenario 1
  Kiongozi wa mathalani wazii awe analipwa 2million kwa mwezi(baada ya kodi na makato mengine yote) wa miaka yote 40 na awe anasave zote (maana yake zhatumii hata sumni) atakuwa na 960Million. hata kama alikua ananunua viwanja then vinapanda thamani say alichokinunua kwa 40,000 miaka 30 iliyopita leo kinauzwa 30,000,000 bado kuna difference kubwa.

  Lakini kumbuka kazi alizokuwa anafanya ni full time. Na hadi Nyerere anaondoka madakani siidhani kuna mtu alikuwa na mali zenye thamani ya 200million. so may be last 20yrs ndio watu wamevuna hicho kiasi.

  Scenario 2
  Tukisema alikua na biashara ingine, Tungependa kuifahamu ina mtaji kiasi gani na aliupata wapi. Pili mrahaba aliokuwa anaupata kutoka kwenye kampuni alilipa kodi????? Je hiyo company/hiyo biashara ingine auditing report zake zinaonyesha faida ama hasara?????? kama Faidi je zililipa kodi???? Je walideclare hiyo biashara yao wakati wakiwa serikalini????

  Scenario 3
  Tukifanya same assumption kwamba mkewe nae alikua analipwa kiasi kama mumewe na hawakuwa wanakula wala kusomesha watoto (serikali ilikuwa inagarimia kila kitu) bado tutafikia 1.8billion.

  Lazima kuna either walikula rushwa, walijihusisha na madawa ya kulevya, waliuza mali za UMM wakagawana, walijigawia mali za UMMa ama walikuwa wafadhili wa mtandao wa majambazi waliokuwa wakivamixa bank au ni washirika wa kina kasusura.

  nawakilisha Bowbow
   
 15. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #15
  Dec 4, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  I hear you loud and clear!.....bs!
   
 16. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  You saw that uh!.....wink:)
   
 17. K

  Koba JF-Expert Member

  #17
  Dec 4, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...sio lazima usome kila kitu kilichoandikwa humu na kule kwenye mambo ya kikubwa kuna picha nyingi kuliko maandishi unaweza kwenda kule kujipa raha!
   
 18. f

  falesy Senior Member

  #18
  Dec 4, 2008
  Joined: Mar 15, 2006
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii sasa inanionyesha kuwa watnzania tuko nyuma ya wakati kwa umbali kati ya ukweli halisi na tukio la huo ukweli linapotokea.

  sijui mfumo wa upashanaji wa habari wa nchi hii kama uko kompetent kiasi cha kuwa na mambo haya yakitokea na kuona mambo yakitokea kisha tunakuwa mbele kujadili. hebu tuwe wachunguzi wa mambo,

  hawa waandishi (nyinyi) mnanishangaza na mnanichanganyaa, mboana mwataka kuwa wanasiasa? nyie mwataka kugombe ujumbe nec ccm na hata udiwani halafu mkikosa mnaanzakuikosoa serikali hizo ni roho za chuki?

  kuangalia leo mali za mramba na yona tuko too late tungeanza dhati day mzee wa vijisent amepata kasheshe mbona hatuko strategik? tukome tu kidogo........

  HATA TUKIMSEMA RAIS SANA KWA UONGO NA UZANDIKI TULIONAO HATUFIKI.
   
 19. K

  Koba JF-Expert Member

  #19
  Dec 4, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...sasa acha kulia lia njaa na kufikiri kila mwenye nazo ni fisadi!
   
 20. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #20
  Dec 4, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Shut up and move on!....so what?.
   
Loading...