MWANASIASA HURU
Senior Member
- Oct 4, 2012
- 180
- 244
Mimi ni dada wa miaka 38 nina watoto 3 kwenye ndoa nina miaka 13, mume wangu ana umri miaka 52.
Mwaka huu mwanzoni nilifuma sms kwenye simu ya mume wangu akijibu sms ya mchepuko.
Ni hivi mchepuko alimwandikia kwamba ana mimba yake, yeye akajibu kwamba sio mimba yake siku ambayo walikutana yeye akumaliza (sijui alikuwa na mana gani). Hiki kitu kimeniumiza sana moyo.
Nilikuwa nina uhakika kwamba anachepuka lakini nikajipa moyo anatumia condom. Baada ya kufuma hiyo sms ndio nikaamini kwamba ana kwenda bila kinga. Hiki kitu kinaniumiza sana moyo sijui nifanye nini ili nisahau, ukizingatia magojwa yalivyo mengi! Inatisha kwelikweli.
Naomba ushauri nitumia njia gani ili nikifute kwenye mawazo yangu.
Mwathirika.
Pole sana mpendwa, hizo ni changamoto tu ila zisikuumize bali zikufunze ujue tatizo lilipo kisha ulitatue. Usikimbie wala uckacrike kwani unazidi kumpa go ahead.
Cha mcngi yajibu haya maswali;
1. Akija nyumbani toka kazini huwa unampokeaje? Unampa mda kidogo wa kumsalimia na kujua mawili matatu aliyoyapitia tangu atoke asubui?
2. Baada ya hapo unampa huduma gani kuondoa uchovu, eg maji ya kuoga, kuandaa msosi nk
3. Mawasiliano yenu yakoje, we ni mtu mbishi, wa kupiga kelele akikosea, ama wa kununa ovyo?
4. Ukiwa na jambo la kimapenzi ama la kimaendeleo unamshirikishaje? Faragha ama ni mtu wa kubeba moyoni?
5. Je kwenye tendo takatifu unajumuika vip, unajiandaa vp na usafi wako kwa ujumla ukoje?
6. Unafahamu vtu gani anapenda? Anavipata vyote? Su unajitahidi kiasi gani kujua flavour zake?
7. Unaufahaamu mchepuko wake, ukoje ukijilinganisha nae? Unajiweka sawa kama awali ama cku hizi mambo mengi?
8. Baada ya tukio hilo, tabia yako imekuaje hapo ndani?
9. Je, wewe ama yeye, kuna anayetumia kilevi?
10. Je, unamshirikidhs Mungu wako msmbo haya na kuomba hekima?
Ni hayo tu kwa sasa, ila all in all, stay calm, be humble and wise in all tou talk and do. Pia acha kuhoji nafsi yako sana juu ya hili kwani ndo maumivu yanaongezeka.
Iambie akili au moyo tulia ni maisha.
Usikae mda mrefu bila kula kuepuka matatizo mengine.
Safari bado ni ndefu hivyo funga tumbo, jikaze, wanao wasijue sana au kabisa.
Stay Alive! And may God give you strength.