Mauaji ya watu 3 Ilala - Dar

Mauaji ya watu 3 Ilala - Dar

Ni sawa tu hawa wanyama hawana shukrani yalishanikuta mimi hayo,mtu anakuwa na wewe kwa malengo baadae anasepa,nilitaka kuua mtu mimi,hawa wanawake huwa wana roho ngumu sana huwa hawajui watu unajinyima nini,wazee mpaka yakukute ndio mtaelewa,hakuna kitu kama kuheshimu feelings za mtu,mimi tangu nitake kumtwanga huyu mnyama risasi naogopa sana binadamu kama mimi naweza kutwanga mtu risasi mwenzako anaweza nini?
 
yaleyale ya ufoo. na hili pia mlengwa hakufa na jamaa kishajiua tayari. nani anayefuata..?
 
Mwanamke hana Dhamana na Sisi Wanaume Tumezidi UBWEGE NAZI ( UJINGA ) acha tu Akina Dada Watutese na Watupelekeshe Watakavyo! Unaacha Kumsomesha Ndugu Yako wa Damu Unahangaika Kumgharamikia Demu TENA WENGINE HUWA MNANIBOA KWELI KWANI UTAKUTA DEMU HAKUTAKI LAKINI WEWE UNAKOMAA TU. Acha MTESWE TU MALOFA WAKUBWA NYIE! Mimi Niliacha KUPENDA RASMI MWAKA 2010 na Sasa UKINIONA na DEMU UJUE NAMDANGANYA TU NA NAKWENDA KUMBATUA KISHA NAHAMISHA KAMBI. Mwanamke hata Umpe Nini na Hata UMSUGUE VIPI bado tu ATAGONGWA NJE na MASELA na KIBAYA ZAIDI MASELA WA SIKU HIZI WANAJUA KWELI KUSIMAMIA SHOW ( KUGEGEDA ) na Wengi Wao WANAGONGA * 148 * 01# OK ( KINYELEO ). Ukiwa Masikini UNAKANYAGIWA, UKIWA TAJIRI NAPO PIA UNAKANYAGIWA Hivi Nyie Dada Zangu NANI KAWAROGA? Cha Msingi Sasa ni Kuishi Kama MAFIA tu UNATAFUTA DEMU na UNAMSETI AKUZALIE MWANA, AMLEE KISHA AKIKUA TU MKUBWA MAMA ANASEPA kwa Kumpa Hata MTAJI Kisha Wewe Unaishi tu na Mwanao. DADA ZANGU MNATIA SANA HASIRA NDIYO MAANA NASI MIDUME SASA TUNAISHI KIMAGUMASHI na KIMINYATO. Badilikeni Jamani MNATUUMIZA........................................................:smile-big:
 
jamani msisikie hii habari nimeishuhudia kwaq macho imetisha sana nilijua ni yale ya westgate.

mimi mnataka kujua sababu ni nini hasa
Dah! Pole kwa ulichokiona. Nasikia ni yale ya dizaini ya kina ufoo.
 
Aya mapenz nikitu gan mpayanafikia hatua ya kuuwa watu dunia hii
 
Huyu ndio muuaji aliyeua kwa bastola na na kisha kujimaliza yeyemwenye jijini Dar leo.....Wivu wa Mapenzi wadaiwa kuwa Chanzo


muuaji.png

Mapema leo asubuhi milio ya risasi zaidi ya kumi ilisikika eneo la Ilala Bungoni karibu na baa maarufu ya Wazee (Club ya Wazee), watu watatu wakiripotiwa kufariki kutokana na tukio hilo linaloelezwa kuwa limetokana na wivu wa kimapenzi.

Dereva mmoja wa tax kituo cha Bungoni ambaye alikuwa shuhuda wa kwanza, alisema mapema leo asubuhi alipata mteja aliyehitaji kupelekwa sehemu, ila kabla hawajafika huko walipokuwa wanataka kwenda jamaa ambaye ndiye alikuwa ni muuwaji alimuomba akatishe safari na kumtaka ampeleke sehemu nyingine.

Dereva huyo aliendelea kusimulia kuwa alimpeleka jamaa mpaka aneo la tukio hilo kwenye nyumba iliyopo pembeni mwa Hotel mpya iitwayo MM.

Mara baada ya kufika hapo, jamaa alitoa sh. 5,000 na kumkabidhi dereva ila cha kushangaza ni kitendo cha jamaa huyo kutoa bastola wakati akiwa anaelekea kwenye geti la nyumba.

Wakati jamaa anaelekea getini mlango ulifunguliwa na gari aina ya Toyota Surf ilitoka ikiwa na watu wanne ndani, mwanaume mmoja ambaye alikuwa akiendesha gari , mama mmoja na wadada wawili.

dereva.png

Jamaa akiwa na bastola alianza kuwashambulia watu waliokuwa ndani ya gari hilo na kumpiga risasi dereva na mdada mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Carol...Baada ya dreva tax kuona hali imechafuka ilimbidi akimbie.

Vyanzo vingine vinaeleza kuwa katika tukio hilo jamaa pia alimpiga risasi ya mgongoni mama wa mwanamke aliyemuua na pia alimpiga msichana mwingine risasi ya mguu.

Mtuhumiwa na dereva aliyekuwa akiendesha gari walifariki palepale huku msichana mmoja akielezwa kufariki akiwa njiani kuelekea hospitali.

Bado haijafahamika moja kwa moja chanzo cha mauaji hayo licha ya watu wengi kudai kuwa ni wivu wa mapenzi
 
Sawa tu,bado wewe uliyekuwa unaishi ulaya sasa ulikuja na kodi za kuchanga!!me jamaa namfeel sana mtu mpaka ujitoe sio mchezo mtu anakuwa kakuchafua mbaya,
 
Back
Top Bottom