Watu watatu,wameuwawa maeneo ya ilala bungoni kwa risasi.
Ilikuwa ni kama sinema ambapo alitokea kijana mmoja akashuka kwenye tex huku kashika bastola, alienda katika geti lililo karibu na hotei mpya ya M.M na kujibanza, gafla geti lilifunguliwa na gari kutoka ndani likiwa na watu wa nne, wanawake 3 na dereva mmoja mwanaume. Jamaa akiwa kajibanza alianza kushambulia ile gari na kuwaua watu wawili dereva na mwanamke mmoja na kuwajeruhi wengine wawili na kisha yeye kijipiga risasi na kufa hapo hapo.
Imeelezwa kuwa kati ya waliojeruhiwa ni mama mzazi na huyo msichana alieuliwa, pia msichana ni mdogo wake (hivyo wote ni mama na watoto wake wawili) ila mwanaume aliekuwa anaendesha gari hajajulikana alikuwa ni nani..
Imeelezwa kuwa yalikuwa ni mambo ya kimapenzi!