Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,096
- 22,627
Ukijipa muda utagundua kuwa mtu anaekukosea kwa makusudi na bila kujali hisia zako akiwa na dhamira mbaya huwa anaishia pabaya pia. Hakuna mwanadamu mwenye jeuri kuliko nguvu za ulimwengu ambazo zinasimamiwa na MUNGU.Ninao wengi wa kuwalipa kisasi kiasi kwamba naishia kucheka na kusema acha ninywe bia maisha yaendelee. Hakika nimeamini nina hasira kali sana na Mungu ameota mbegu kuu njema ndani yangu.
Si muda sahihi wa kusema neno bali nashukuru yale mema niliyoyaongeza baada ya kusoma visa na simulizi kadhaa mahali hapa. Shukrani sana.
So ni vema kujipa muda, mtu amekufanyia ubaya kwa kusudi then kubali yaishe kisasi muachie MUNGU. Unaweza dhania kumkata na panga au kumchoma kisu itakuwa ni adhabu kali kwake kumbe wala ile sio kitu ila mkabidhi kwa aliyemuumba atawajibishwa huko.
Aiseeee maisha yanapoanza kumnyoosha mtu aliyekukosea na kukuumiza kiasi kwamba unakaa chini unajiuliza hivi MUNGU anaona ukorofi unaofanyiwa ama la? Kazi ya kunyooshwa ikianza utatamani kumpigia MUNGU magoti amuonee huruma. Wewe kaa kimya mwache ajifanye mjanja. Mkalie mbali na kata nae mazoea na mawasiliano basi. Dunia ikianza kumfunza mtu wa hivyo aiseee hakuna wa kuamulia. Maana ukishika panga ukataka kumkata watu wanaweza ingilia akatetewa, au ukisema umtumie wajuba wamdhuru still anaweza escape au ukajagundulika msala ukakurudia, au ukamwekea figisu watu wanaokuheshimu wakakusihi umsamehe. Ila Maisha sasa yakianza kumnyoosha mtajikuta ni ninyi wawili tu ndio mkitazamana mnajua kuwa sasa muda wa malipo umefika na nani analipia hesabu yake ya madhambi aliyomkosea mwenzake.
Hii kitu hata katika mahusiano ipo sana. Mwanaume au mwanamke anamuacha mwenzake kipindi ambacho hakukuwa na sababu yoyote ya msingi na kulikuwa na utulivu tu au anamfanyia mwenzake matukio ya kuvunja moyo na kuumiza hisia kwa makusudi kabisa then anategemea mwenzake ataelewa tu na kupuuzia maisha yaendelee. Watu wa hivi huko wanakokwenda MUNGU huwa anawapa wanachotaka ila anawanyima wanachostahili sababu unachostahili ndicho kitakupa furaha ila unachotaka kitakufanya ujiskie vizuri kwa muda tu then baadae balaa linaanza.
S