Mfua suleiman
Member
- Feb 27, 2014
- 60
- 62
NUKUU:
"Askari walikwenda Chumo msikitini, wakapiga risasi wakachukua watu 10 tumefika damu zimetapakaa, walivyorudi mmoja kafa, mmoja hana jicho, mmoja wakamnyoa ndevu kwa kumchoma moto, mnapotuambia nchi hii ina amani na utulivu mimi siwaelewi" - Suleiman Bungara (Bwege) Mb - Kilwa.
[HASHTAG]#MUHIMU[/HASHTAG]
Haya yaliyoripotiwa na Mhe. Bungara ni machache kati ya mengi ambayo askari wetu wameyafanya na wanaendelea kuyafanya dhidi ya baadhi ya viongozi na waumini wenzetu wa dini ya kiislam katika kile kiitwacho vita dhidi ya ugaidi.
Pamoja na madhira hayo wanayokutana nayo viongozi wetu wa dini na baadhi ya waumini wenzetu wa dini ya kiislam nchini sijawahi kuona jitihada zozote zinazofanywa na taasisi ijulikanayo kama Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) chini ya kiongozi wake mkuu Ndg. Abubakar Zuber kulaani au kutafuta suluhu ya jambo hilo.
Pamoja na hayo naomba niwakumbushe askari wetu wapendwa na jeshi la Polisi kwa Ujumla wake.
Polisi wetu ninyi mmepewa dhamana kubwa ya kulinda usalama wa raia na mali zao, na mkae mkijua kua raia karibu wote wa Nchi hii tunawategemea sana katika kulinda usalama wa maisha yetu na mali zetu,
hivyo ni vema mkazingatia mafunzo, utaalam na weledi wa hali ya juu kwa mujibu wa kanuni mbalimbali za maswala ya usalama zinavyowataka pindi mnapohisi kuna viashiria vya uvunjifu wa amani katika eneo lolote na si kutumia Miguvu katika sehemu inayohitajika Akili na Maarifa.
Najua Askari wetu wanakabiliana na changamoto mbalimbali za mishahara isiyokidhi mahitaji yao lakini pia kufanya kazi kwa maagizo na mashinikizo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa, nawaomba sana msivunjike moyo kwa kua taifa na watanzania tunawategemea sana katika kuimarisha usalama wetu na wa mali zetu.
Hivyo muitumie dhamana hiyo vizuri kwa kutenda haki kwa watu wa makundi yote kwa kua ninyi ni binaadam na mkumbuke kua kuna maisha baada ya Dunia ambayo yataamuliwa na matendo yenu hapa Duniani aidha Peponi au Jahannam (Motoni)
[HASHTAG]#Tujitafakari[/HASHTAG]