Mauaji ndani ya msikiti wa Chumo

Mauaji ndani ya msikiti wa Chumo

Uislam ulitamalaki kwa nguvu ya umoja

Lakini kwa sasa umoja baina ya waislamu hakuna

Tumetenganishwa na mambo ya makundi (madhehebu)

BAKWATA WANAJIONA WAO NDIO WANAHAKI DHIDI YA WAISLAMU
na kazi yao kujikomba kwa watawala tangu nazaliwa sijawahi kuona bakwata wakitoka hadharani kukemea jambo baya zaidi ya kuiipendekeza BAHASHA ZA KAKI MBAYA SANA
 
Bila kusahau huyu ndugu yetu aliye kua mwanafunzi UDSM pia walimuua kwa dhulma anaitwa Almasi Allah amkubali
 
Attachments

  • FB_IMG_1522225669779.jpeg
    FB_IMG_1522225669779.jpeg
    98 KB · Views: 47
NUKUU:
"Askari walikwenda Chumo msikitini, wakapiga risasi wakachukua watu 10 tumefika damu zimetapakaa, walivyorudi mmoja kafa, mmoja hana jicho, mmoja wakamnyoa ndevu kwa kumchoma moto, mnapotuambia nchi hii ina amani na utulivu mimi siwaelewi" - Suleiman Bungara (Bwege) Mb - Kilwa.

[HASHTAG]#MUHIMU[/HASHTAG]
Haya yaliyoripotiwa na Mhe. Bungara ni machache kati ya mengi ambayo askari wetu wameyafanya na wanaendelea kuyafanya dhidi ya baadhi ya viongozi na waumini wenzetu wa dini ya kiislam katika kile kiitwacho vita dhidi ya ugaidi.

Pamoja na madhira hayo wanayokutana nayo viongozi wetu wa dini na baadhi ya waumini wenzetu wa dini ya kiislam nchini sijawahi kuona jitihada zozote zinazofanywa na taasisi ijulikanayo kama Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) chini ya kiongozi wake mkuu Ndg. Abubakar Zuber kulaani au kutafuta suluhu ya jambo hilo.

Pamoja na hayo naomba niwakumbushe askari wetu wapendwa na jeshi la Polisi kwa Ujumla wake.

Polisi wetu ninyi mmepewa dhamana kubwa ya kulinda usalama wa raia na mali zao, na mkae mkijua kua raia karibu wote wa Nchi hii tunawategemea sana katika kulinda usalama wa maisha yetu na mali zetu,
hivyo ni vema mkazingatia mafunzo, utaalam na weledi wa hali ya juu kwa mujibu wa kanuni mbalimbali za maswala ya usalama zinavyowataka pindi mnapohisi kuna viashiria vya uvunjifu wa amani katika eneo lolote na si kutumia Miguvu katika sehemu inayohitajika Akili na Maarifa.

Najua Askari wetu wanakabiliana na changamoto mbalimbali za mishahara isiyokidhi mahitaji yao lakini pia kufanya kazi kwa maagizo na mashinikizo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa, nawaomba sana msivunjike moyo kwa kua taifa na watanzania tunawategemea sana katika kuimarisha usalama wetu na wa mali zetu.

Hivyo muitumie dhamana hiyo vizuri kwa kutenda haki kwa watu wa makundi yote kwa kua ninyi ni binaadam na mkumbuke kua kuna maisha baada ya Dunia ambayo yataamuliwa na matendo yenu hapa Duniani aidha Peponi au Jahannam (Motoni)

[HASHTAG]#Tujitafakari[/HASHTAG]

Pamoja na Polisi kutotumia mbinu rafiki kafika kushughulikia changamoto za uhalifu au viashiria vyake naamini kuna shida katikati ya hao waumini na mashehe. Kuna wawili au watatu wana agenda zao sasa wanaponza wenzao. Haingii kichwani polisi wachukie waumini wa mskiti mmoja pekee kati ya yote iliyopo Kilwa. Tusiwe wepesi wa kulaumu bila kujua taarifa za upande wa pili.

Intelijensia ipo kila mahali na usishangae kati ya waliochukuliwa na pengine mmoja hatarudishwa na huyo ndiye intelijensia.
 
Hivi Tanzania nani aliwaroga maana enzi za mwalimu watu walikuwa wamoja leo hii nasikia mambo mageni sana humu hadi kauli zisizo jenga zimo humu tuweni makini tuendako hatupajui maana mwenyezi mungu ndio anajua hamna mtu ana huwakika baada ya masaa mawili nini itatokea kwahiyo ombi langu kwa Watanzania na watu wote dunia msidharauliane kwa lolote lile muheshimiane na kuwepo na mipaka ya utani na kwa uwezo wake muumba kila kitu atatusaidia Aameen .
 
watanzania wanaoupinga huu uislamu hata hatuelewi kitu gani kimetokea.mpaka wametokea kuchukiwa na baadhi ya wakiristo kiasi hiki na kama ni huo ugaidi tunajiuliza ni ugaidi upi waislamu wa tanzania walioufanya kwa watanzania wenzao? Au ubaya gani Waislamu wa Tanzania waliofanyia wasio waislamu Tanzania kiasi cha kuchukiwa hivi au ni chuki tu ambazo pengine wamefundishwa na viongozi wao wa dini maanake hatuwaelewi hawa wenzetu. Yaani watu wanasherekea na kuunga mkono manyanyaso na mauaji waliofanyiwa watanzania wenzao hii inasikitisha sanaa. Tunakoelekea ipo siku tutajuta.
Mimi pia nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara kuwa wanzetu wakristo tumewafanyia nini sisi waislam? Najiuliza swali hili kwasababu tupo nao maofisini, tupo nao katika misiba yao na ya kwetu, tupo nao kwenye shida za kuuguliwa, tunakula nao, tunakunywa nao na baadhi yao tumeoleana nao, tupo nao kwenye masoko tukiuza na kununua bila hata kuuliza dini.

Wakristo tuelezeni sisi waislamu wa Tanzania tumewakosea nini?? Sijaona mkristo yoyote hapa mtaani kwetu amedhuliwa na muislam kwasababu ya dini labda ziwe ni sababu binafsi ambazo hata wakristo hufanya pia. Je hizi chuki wakristo wamefunzwa na watawala wa dunia au viongozi wao wa makanisa??

Mi hata sielewi! yaani ifike mahali mkristo auawe kanisani kwasababu ambazo hazipo clear halafu nishangilie kisa alieuwa ni mkristo!!! That can't be possible, To me, Humanitarian imperative comes first, religion second.
 
Kuwatesa na kuua waumini eti kwakuwa umewakuta msikitini usiku siyo utetezi. Uislsmu una ibada za usiku " KIAMLAILI". Pia misikitini ndipo wanapofikia kulala watu TABLIH. Lakini kama alivyoandika chige, wale wanaodai ni ugaidi waseme juu Ben Saanane na Tundu Lissu nao ni Magaidi?
exactly
 
Pamoja na Polisi kutotumia mbinu rafiki kafika kushughulikia changamoto za uhalifu au viashiria vyake naamini kuna shida katikati ya hao waumini na mashehe. Kuna wawili au watatu wana agenda zao sasa wanaponza wenzao. Haingii kichwani polisi wachukie waumini wa mskiti mmoja pekee kati ya yote iliyopo Kilwa. Tusiwe wepesi wa kulaumu bila kujua taarifa za upande wa pili.

Intelijensia ya ipo kila mahali na usishangae kati ya waliochukuliwa na pengine hatarudishwa ni intelijensia.
Tupewe hayo maelezo ya inteligensia yenye ushahidi usiotia shaka. Hata wewe sio rahisi mtoto wako auawe mbele ya macho yako halafu unaambiwa ni mwizi bila uthibitisho halafu utakubal kirahisi rahisi. Tusishabikie tu mambo kwasababu yamewakuta wenzetu
 
Maneno ya kipumbavu ya kuunga mkono mauaji na manyanyaso wanayofanyiwa hawa waislamu na maiti zote zilizo okotea kwenye maviroba ni waislamu waliouliwa
Halafu tuluvyo wanafiki eti nchi ya amani hakuna amani yoyote nchi hii. Na hao wanaofanyiwa huu umyama ni binadamu wenzenu na ni watanzania lakini tofauti iliyopo ni sio wakanisa. Kwa hii ni jinsi gani nchi hii ilivyo na ubaguzi wa dini.
Ukweli mnaujua ila mnajificha vichwa kama mbuni mkidhani hamuonekani. hakuna siri duniani. kama hawa polisi wanafanya haya ya kumnyanyasa mtu kwa sababu ya dini yake Mungu atashughulika nao. na nijuavyo mimi kama hivi ndivyo hakuna muumin wa uislam au kiongozi wa uislam anayeweza kuuvumilia unyanyasaji au unyanyapaa wa kiiman hata kwa dakika moja au mbili kama walivyo wakristo. Ila ukimya wa viongozi wa kiislam unaashiria kuwapo kwa jambo jingine linalofanywa na hawa jamaa kwa kivuri cha uislam. Polisi msimuonee mtu kisa dini yake. ila anayepanga uharibifu na aharibiwe yeye.
 
watanzania wanaoupinga huu uislamu hata hatuelewi kitu gani kimetokea.mpaka wametokea kuchukiwa na baadhi ya wakiristo kiasi hiki na kama ni huo ugaidi tunajiuliza ni ugaidi upi waislamu wa tanzania walioufanya kwa watanzania wenzao? Au ubaya gani Waislamu wa Tanzania waliofanyia wasio waislamu Tanzania kiasi cha kuchukiwa hivi au ni chuki tu ambazo pengine wamefundishwa na viongozi wao wa dini maanake hatuwaelewi hawa wenzetu. Yaani watu wanasherekea na kuunga mkono manyanyaso na mauaji waliofanyiwa watanzania wenzao hii inasikitisha sanaa. Tunakoelekea ipo siku tutajuta.
Mberesero alichokifanya chuo kikuu cha garisa kenya unakijua? waliokamatwa Mozambique makosa yao unayajua? leo kenya kesho mozambique keshokutwa wapi? Endeleeni kujificha kichwa kama mbuni mkidhani kiwiliwili hakionekani.
 
Inteligensia yetu ya Tanzania naomba ifanye kazi bila kukurupuka pamoja na usalama wa raia pia wafanye kazi zao kwa umakini sana hawa tuko nao masaa 24 wanatujua sisi watanzania vizuri ila tunaomba chuki binafsi na kazi uliyoapa usichanganye pamoja na tamaa ya duniani kwa uwezo wake mola Tanzania itakuwa mfano kuigwa duniani.
 
Mberesero alichokifanya chuo kikuu cha garisa kenya unakijua? waliokamatwa Mozambique makosa yao unayajua? leo kenya kesho mozambique keshokutwa wapi? Endeleeni kujificha kichwa kama mbuni mkidhani kiwiliwili hakionekani.
Waingie kwenye nchi ya watu wauwe viongozi wao wauwe wananchi hawana nguvu ya kupambana nao. Wanaamua na wao kulipiza kisasi vile wanavyoweza halafu mnawaita magaidi. Hizo za Kenya na huko kwengineko hazituhusu kabisa hapa kwwtu. Munaanza chokochoko na walio wajinga wakiingia kwenye huu mtego muwamalize ?
 
Na mpigwe tu maana hakuna namna....
Mmezidi kucheza ma-karate misikitini badala ya kuswali.

Imekuwa kawaida kuwafundisha vijana wetu mashuleni judo na karate, kutumia majambia, na siku hizi mpaka meditation mnafanya ndani ya masjidi za mashule.

Mimi narudia kauli ya Pinda aliposema
"Na wapigwe tu"
No please! Usidhani uko salama. Kuna siku utapigwa wewe ndio utaelewa machungu ya maonevu.
 
Mberesero alichokifanya chuo kikuu cha garisa kenya unakijua? waliokamatwa Mozambique makosa yao unayajua? leo kenya kesho mozambique keshokutwa wapi? Endeleeni kujificha kichwa kama mbuni mkidhani kiwiliwili hakionekani.
Kwa hiyo Mberesero katumwa na Waislamu Wote wa Tanzania aue wale Wanafunzi wa Garisa?
Hakika Generalization ni tatizo sana. Mtu ambae hana uwezo wa kuona na kuyajua hata yale yaliyo mbali na yeye ndio huwaza kua kila akionacho basi ndio kiko hivyo hivyo kila mahali.
Ngoja nikuulize, wewe hujawahi kusaidiwa na Muislamu yeyote asie Mberesero mpaka unafikia kudhani kua kila Muislam yuko kama Mberesero?
 
Asigwa leo sijapenfezwa na mchango wako hata kidogo.
Mimi ni mkristo tena mkristo kweli lkn siwezi kiwachukia ndg zetu waislam kiasi hicho.
Siyo waislamu wote ila magaidi fulani ndani yake!
 
Maoni kwa Rais wangu mpendwa tuhurumie sisi viumbe wa mwenyezi mungu ambao hutajakamilika kwa lolote lile ukiwa pamoja na wewe pia ila mungu amekuteuwa uwe msimamizi wetu na kutuongoza kwa Amani na upendo mungu akupe uwezo mkubwa wa kuweza kugundua yule binaadamu ambaye hapendi Amani tuliyokuwa nayo leo hii Tanzania na kuleta fitna ya kuchonganisha Serekali na waislam au wakristo yarabi akuoneshe na umshuhulikie kweli kweli
 
Kwa hiyo Mberesero katumwa na Waislamu Wote wa Tanzania aue wale Wanafunzi wa Garisa?
Hakika Generalization ni tatizo sana. Mtu ambae hana uwezo wa kuona na kuyajua hata yale yaliyo mbali na yeye ndio huwaza kua kila akionacho basi ndio kiko hivyo hivyo kila mahali.
Ngoja nikuulize, wewe hujawahi kusaidiwa na Muislamu yeyote asie Mberesero mpaka unafikia kudhani kua kila Muislam yuko kama Mberesero?
Maelezo yako wapelekee wahusika mi nitakusaidia nini. mi najaribu kutoa angalizo tu kuwa wako watu wanauchafua uislam kwa maslahi ya matumbo yao. huo ni mfano hai.
 
Maelezo yako wapelekee wahusika mi nitakusaidia nini. mi najaribu kutoa angalizo tu kuwa wako watu wanauchafua uislam kwa maslahi ya matumbo yao. huo ni mfano hai.
Nawe Hilo angalizo lako si ungewapelekea wahusika pia?
 
Back
Top Bottom