Mauaji ndani ya msikiti wa Chumo

Mfua suleiman

Member
Feb 27, 2014
60
62
FB_IMG_1523538113418.jpeg


NUKUU:
"Askari walikwenda Chumo msikitini, wakapiga risasi wakachukua watu 10 tumefika damu zimetapakaa, walivyorudi mmoja kafa, mmoja hana jicho, mmoja wakamnyoa ndevu kwa kumchoma moto, mnapotuambia nchi hii ina amani na utulivu mimi siwaelewi" - Suleiman Bungara (Bwege) Mb - Kilwa.

[HASHTAG]#MUHIMU[/HASHTAG]
Haya yaliyoripotiwa na Mhe. Bungara ni machache kati ya mengi ambayo askari wetu wameyafanya na wanaendelea kuyafanya dhidi ya baadhi ya viongozi na waumini wenzetu wa dini ya kiislam katika kile kiitwacho vita dhidi ya ugaidi.

Pamoja na madhira hayo wanayokutana nayo viongozi wetu wa dini na baadhi ya waumini wenzetu wa dini ya kiislam nchini sijawahi kuona jitihada zozote zinazofanywa na taasisi ijulikanayo kama Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) chini ya kiongozi wake mkuu Ndg. Abubakar Zuber kulaani au kutafuta suluhu ya jambo hilo.

Pamoja na hayo naomba niwakumbushe askari wetu wapendwa na jeshi la Polisi kwa Ujumla wake.

Polisi wetu ninyi mmepewa dhamana kubwa ya kulinda usalama wa raia na mali zao, na mkae mkijua kua raia karibu wote wa Nchi hii tunawategemea sana katika kulinda usalama wa maisha yetu na mali zetu,
hivyo ni vema mkazingatia mafunzo, utaalam na weledi wa hali ya juu kwa mujibu wa kanuni mbalimbali za maswala ya usalama zinavyowataka pindi mnapohisi kuna viashiria vya uvunjifu wa amani katika eneo lolote na si kutumia Miguvu katika sehemu inayohitajika Akili na Maarifa.

Najua Askari wetu wanakabiliana na changamoto mbalimbali za mishahara isiyokidhi mahitaji yao lakini pia kufanya kazi kwa maagizo na mashinikizo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa, nawaomba sana msivunjike moyo kwa kua taifa na watanzania tunawategemea sana katika kuimarisha usalama wetu na wa mali zetu.

Hivyo muitumie dhamana hiyo vizuri kwa kutenda haki kwa watu wa makundi yote kwa kua ninyi ni binaadam na mkumbuke kua kuna maisha baada ya Dunia ambayo yataamuliwa na matendo yenu hapa Duniani aidha Peponi au Jahannam (Motoni)

[HASHTAG]#Tujitafakari[/HASHTAG]
 
Kinachonisikitisha kwa waislamu huwa hawaoni madhila yanayofanywa na watawala mpaka pale wanapoguswa wao au maslahi yao ndio utasikia wakilalamika Jamii yao inaonewa.Kuna usemi ,"Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu."Msisubiri mpaka yawakute ninyi muanze kulalamika.Shirikianeni na watu wa jamii zingine ambao ni waathirika wa haya maonevu.Sauti ziipazwa kwa pamoja zinakuwa na nguvu kuliko kila mmoja akipaza sauti kivyake.Mwisho ninawapa pole kwa madhila yaliyowafika.
 
Juzi Tundu Lissu kafanyiwa operesheni ya 20 baada ya kunyeshewa mvua ya risasI...

Mwaka mmoja unusu umetimia na Ben Saanane haijulikani alike

Ni takribani miezi 4 sasa Mwandishi wa Mwananchi Communications haijulikani alipo

Itoshe tu kusema kwamba; haya mambo hayana mmoja! Chuki zako za kidini zinaweza kukufanya uone hao ni magaidi ya Kiislamu yacheza karate misikitini lakini hao niliokutajia sijui wanacheza karate misikiti ipi!

Tumeshuhudia hata viongozi wa Kikristo wakihojiwa uraia wao mwaka huu kwa sababu za kijinga kabisa!

PUNGUZA CHUKI ZA KIDINI...
 
Kuna baadhi ya waislmu ni magaidi (hata huko alikozaliwa mtume wanapambana nao pia). Sasa unakuja unafiki wa waislamu ni pale fala mmoja anasema TAKBIR, wengine wanaitikia kama mbuzi then wanaenda kuua watu kwa kutumia imani ya ua nenda ahera, then hawajiulizi hivi kuua ndiyo suluhisho
Siwezi kushangaa comment hii kutolewa na pro-government kwa sababu ikiwa serikali yenyewe pamoja na chama chake wanaeneza chuki seuze wafuasi wake!

Endeleeni hivyo hivyo kuua na kutupa watu baharini cuz' hicho ndicho serikali yoyote ya kidikteta duniani inachoweza kufanya kwa umakini huku vikaragosi vyao vikitetea mauaji hayo kwa justification mbalimbali!

Na yule Tundu Lissu mliyetaka kumuua bila shaka na mwenyewe ni gaidi!!

Itoshe tu kusema kwamba, serikali yoyote dhalimu duniani has 1001 Reasons to Murder Her Citizens and will always have one more reason to murder!
 
Siwezi kushangaa comment hii kutolewa na pro-government kwa sababu ikiwa serikali yenyewe pamoja na chama chake wanaeneza chuki seuze wafuasi wake!

Endeleeni hivyo hivyo kuua na kutupa watu baharini cuz' hicho ndicho serikali yoyote ya kidikteta duniani inachoweza kufanya kwa umakini huku vikaragosi vyao vikitetea mauaji hayo kwa justification mbalimbali!

Na yule Tundu Lissu mliyetaka kumuua bila shaka na mwenyewe ni gaidi!!

Itoshe tu kusema kwamba, serikali yoyote dhalimu duniani has 1001 Reasons to Murder Her Citizens and will always have one more reason to murder!
Sioni ulichoandika hapo. Serikali hii ya awamu ya 5 unaiita ya kidkteta ? Kikwete alituambia. Wakitaka kuichafua serikali. Waonyeshe fly over. SRG. Viwanja vya ndege. Dawa hospitalini. Elimu bure etc
 
Imezuka tabia ya waislam kusolist pesa uharabuni kwa kisingizio chakuunda na kuimarisha vikundi vya kutetea Uislam. ambapo kiukweli vikundi hivi ndivyo vinazaa ugaid watu wanafundishwa mambo kinyume na maagizo ya quran kwa maslahi ya watu wenye tamaa ya fedha na mali na hivyo kuchangia uvunjifu wa amani maeneo mbalimbali duniani. hivyo serikali fanyeni kazi yenu msiyumbishwe na itikadi ya mtu. kama kuna hivyo vikundi hakikisheni mnavisambaratisha watu warudi mashambani wakalime wafanye kazi sio kulala na kuishi maeneo ya ibada. Tukinyamaza tukaendelea kumfuga chatu siku akianza kula watu tusipige kelele maana tumemfuga wenyewe.
 
chige unajitia kuutetea uislamu wakati hata juzuu 3 hujamaliza. Little knowledge is poison. Wewe ndio wale tunaokutana nao Kimara kwenye viti moto halafu huku mkisema ya Kimara tuyaache Kimara. Muislam gani wewe unatukana ovyo ovyo. Uislamu wa kweli ni uungwana. Usafi. Usomi. Utanashati etc
 
kwani hao maaskari waliotenda hayo walikuwa ni wakristo kuanzia rais wenu mpaka mwenyekiti wa serikali za mitaa ni waislam
 
Chige unajitia kuutetea uislamu wakati hata juzuu 3 hujamaliza. Little knowledge is poison. Wewe ndio wale tunaokutana nao Kimara kwenye viti moto halafu huku mkisema ya Kimara tuyaache Kimara. Muislam gani wewe unatukana ovyo ovyo. Uislamu wa kweli ni uungwana. Usafi. Usomi. Utanashati etc
Look at you!! That's why nikakuambia you're talking nonsense!

Awali nimezungumzia habari za dictatorship and possibly you know less about me!! Been criticizing JPM's dictatorship style since then!

Lakini wakati nimezungumzia dictatorship, ukaleta habari za flyover! Does it add up?

Umehama kwenye flyover, unaleta habari za kutetea Uislamu!

Tundu Lissu niliyemuongelea ni Mwislamu?

Ben Saanane ni Mwislamu?

Mwandishi wa Mwananchi Communication ni Mwislamu?

Viongozi wa dini niliosema wanahojiwa uraia wao ni Waislamu?

Unadai Mwislamu gani mimi natukana hovyo! Narudia; what you're writing is NONSENSE! Where did I say i'm Muslim?

Btw; hivi ni mtu wa namna gani wewe unaibuka from nowhere unamwambia mwenzako alichoandika ni utumbo wa nguruwe? Au ndivyo ulivyofunzwa kwenu hivyo?

USIJIFANYE UNANIJUA wakati you know nothing about me!
 
Na mpigwe tu maana hakuna namna....
Mmezidi kucheza ma-karate misikitini badala ya kuswali.

Imekuwa kawaida kuwafundisha vijana wetu mashuleni judo na karate, kutumia majambia, na siku hizi mpaka meditation mnafanya ndani ya masjidi za mashule.

Mimi narudia kauli ya Pinda aliposema
"Na wapigwe tu"
Hujielewi wewe.
Kumbuka maneno ya Tundu Lissu kuwa awamu hii hakuna aliye salama. Sasa wewe leo shabiki kwa kuuwawa muislam,baadae Akwelina,Ben kapotezwa wewe endelea kushabikia tu. Mpaka auawe babako au mamako ndio utajua polis sio watu wazuri.
 
Back
Top Bottom