Matusi Redioni

sasa ngoja tukubali kuwa sisi tuliomsikia akitukana ni vichaa, wewe ndio mwenye akili timamu kutaka ushaidi wa upuuzi

Usikasirike unapoombwa ushahidi wa kile unachokidai. Kama huna ushahidi wa kuunga mkono madai yako ni bora na ni busara kukaa kimya kwanza hadi hapo utakapokuwa tayari na uhakika wa kile unachokidai.

Na ujue mimi sijakataa kuwa Kibonde katukana na sijakubali kuwa kweli katukana. Mpaka sasa nipo agnostic. Ukiniwekea ushahidi hapa nami nikasikie kwa masikio yangu kile mnachokidai kakisema, kelele zangu za kuomba ushahidi zitakoma.

Ni hivyo. Au mtu kuomba ushahidi ni kosa?
 

Jambo la kushangaza ni kuwa hii SI MARA YA KWANZA CLOUDS KUTUKANA HEWANI. Kwa bahati mbaya mara zote hizi anayetukana ni huyohuyo Kibonde ambaye mara nyingi anaoneka kuhodhi mijadala hiyo ya Jahazi. Tangu ameondoka Gardner hicho kipindi kimekosa radha, kimekosa maadili, kimekosa mwelekeo na haijulikani kwa siku hiyo wanaongelea au kujadiri jambo gani. TUNAWAOMBA TCRA WACHUKUE HATUA KWA CLOUDS FM ili radio zetu ziwe na nidhamu na zifuate maadili ya Kitanzania
 

Na nyinyi muache kukisikiliza. Sio kulia lia tu....hhihihihihhh Kibonde kasema hivi.....hihihiiii Kibonde kasema vile......mtalia hadi lini? Hupendi Clouds...sikiliza Times FM....huwapendi hao sikiliza Redio wani....ebo!
 
nahisi preta aliamka na hangover...so masikio yake yalikua a lil bit dead..
 

... cloud cloud.. kibonde kibonde..waaaacheenii kwani kuna mtu anawaalika mumskize... kama vp na nyie anzisheni radio zenu ili mtukane...
 
Mtoa mada hilo tusi si tusi kuzidi ya avatar yako hiyo! Japo sifaigilii kabisa kinachoendelea na Clouds FM kwa sababu inapoteza umaarufu hata na East Africa na akina Zembela, cha kuwashauri East Africa waweke kipindi kama hicho cha clouds mida hiyo ya kwenda nyumbani maana hakuna redio kwa sasa Clouds wamechemsha ubunifi zero, huwezi mtu ukawa unajua kila kitu, mipira wewe, siasa wewe, uchumi wewe, mambo ya viti virefu wewe, khaa Clouds fungukeni bwana.

Hoja yangu Preta hiyo avatar yako ni tusi tosha kwa sisi watoto wa miaka ya sitini na sabini huko, ilikuwa ukiona tu lesi lesi za gagulo ya mama yako ni aibu, sembuse na hiyo avatar yako? ahh jamani si afadhali ya TUSI LA KIBONDE?

Aluta contunua!
 

Wheww......kweli Alunta Continua
 
nahisi preta aliamka na hangover...so masikio yake yalikua a lil bit dead..

hivi eeeh.....dah....basi inaelekea wote tuliosikia tulikuwa na mning'ing'inio......
 

Nilisikiliza, ukweli hakutukana zaidi ya kusema kafanye kazi kwa mamako, najinsi anavyoongea haraka wengi mmetafsiri sivyo.
Hata hivyo mleta mada avatar yako ni matusi tosha, kama kweli umekereka na uliyodhani matusi ya kibonde nategemea utaona ni matusi pia kwa avatar yako isiyo na ustaarabu na heshima hata kidogo
Tafakari chukua hatua
 
nilishaacha kusikiliza long ago ..hii imenisaidia kutosikia haya yote
 

Umemaliza kila kitu mzazi!
 
kumekua na malalamiko mengi sana kuhusu huyu mtu kwanini alalamikiwe yeye tu? Kiukweli kuna wakati hata sielewi anayoyazungumza ni akili yake au ya kuazima, kama kweli ametukana awe makini radio si sehemu ya kuropoka tu mawazo binafsi kama huwezi kuongea mambo ya msingi si lazima uongee mimi mmoja wa walioacha kuckilza jahazi kwa sababu ya upuuzi wake ni hayo tu ya kwangu.
 
↲Burudani si matusi au kizazi chenu burudani ni matusi?
bisekosonj80 karibu sana janvini.
Rudia kusoma post yangu tena na tena uone wapi imeandikwa kibonde katukana na ndio burudani yenyewe
kisha tafakari kizazi chako
 
kibonde mpumbavu alitukana wanafunzi wa UDSM kuwa ni malaya,walevi eti wanakesha baa,hivi huyu kibonde huwa analewa bia ngapi? Hivi kwa sh.5000,unaweza ukakesha baa.huyu bwabwa anakera sana,anatafuta sifa,sijui anaisi watawala watampa ubunge wa viti maalumu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…