Governor of Bettors-GB
JF-Expert Member
- Jul 14, 2013
- 10,897
- 10,127
Massai nakubaliana na wewe,hili neno ni Tusi na tatizo nikwamba walioponda hapo juu walifikiria kwamba maana yake hujui mpaka wengine eti kujifanya kuanisha sijui What`sup Facebook na Twitter.Wakati hilo linafahamika na kila mtu hadi watoto.Lkn inabaki pale kwamba hilo neno ni tusi, na watengenezaji sio kweli hawalijui hilo
Hapo ndio huwa tunalalamika wakenya kuja kuchukua ajira zetu kwa uzembe huu.
Kwa wale ambao ni kizazi cha kabla ya facebook wakati wa chatting rooms za kimarekani haya mamaneo hutumika sana,na wengi walikuwa wakitumia kwa ufupi huo pale ukiwazingua.
Sasa mie naelewa watu wa Marketing hii ni taaluma yao,na ni miongoni mwa vitu wanatakiwa kuvikwepa sana,mie nina kiji Certificate cha mambo hayo.Labda hao wenye ma Degree ndio waliona haina shida.
Ila hilo neno ni tatizo,labda wakaweke matangazo hayo vijijini,ila mjini kwa wale ambao walikuwa wakichat kwenye sites za nje miaka kumi iliyopita basi wanajua nini maana ya ufupisho huo.Maana siku hizi watu wamezama kwenye Mitandao hiyo ya kawaida inayojulikana.
We usihadaike na nembo zile za ufupisho wa maneno,pale mtu anaweza hata kuchora gari na ikawa na mueleweko mwingine.
Kwanini asiyageuze maneno mfano(TWF),hapo tatizo ni abreviations zake ndio zimepelekea kuwa tusi.
Natoa angalizo,kwa wale ambao wamechat zamani miaka kumi iliyopita basi wanajua maana yake ila hawa ambao miaka kumi ya facebook wameingia basi wao wanaona sawa tu.
Jamaa wabadilishe tangazo lao,yaani hadi kichefuchefu kulitizama,na mbaya zaidi ukizingati dole gumba la mwisho wa heru ndio kabisaaaa.
Na Model mwenyewe na hivi ni mkaa uchi kwnye kipindi chake maziwa nje,ndio inapoteza kila kitu.
In Gneral tangazo linakera hata kutizama.
Halafu unaweza kukuta Board kubwa likawekwa Airport,duhh,kazi kweli.Nchi ya vituko hii.