Matunda matatu yasiyopatikana kiholela mjini

Matunda matatu yasiyopatikana kiholela mjini

Haya namba 3 watu huyaita matunda damu. Haya hupatikana kwa wingi sana huko Dar kipindi cha msimu wake.
Hayo ya katikati ni mafyulisi (Peach) hayo utayala sana ukiwa Tukutu na Mbeya. Mjini kuinekana ni kwa darubini sana. Ni matunda mazuri mno. Kuna kipindi kulikuwa na zile juice za maboksi kutoka Afrique du Sud, zilikuwa zinatengenezwa na hayo matunda...zile juice waa next level. Sijui kama bado mnaletewa.

Hayo mengine ya kwanza hapo juu yanapatikana sana maprini huko Tukuyu, nilijaribu kuyaelewa nikashindwa. Nashanga ukienda Ndarisalama yamefanywa ni ya kishua
Matunda damu yanauzwa mpaka jero jero yakiwa kwenye kimfumo tena yanakuwa 6
 
Haya matunda ukiwa mjini unaweza usiyale miaka kadhaa.
View attachment 3409272View attachment 3409273View attachment 3409274

Strawberry zinapatikana haswa kwenye supermarkets au Kisutu (Dar), Arusha pia nishawahi ona mahal8 zimejiotea tu...

Peaches zipo sana Mbeya, Iringa, Njombe hadi watu wanasaza, nadhani hata Lushoto zitakuwepo ingawa sidhani kama zinazidi nyanda za juu...

Hayo matunda mekundu (wengine huita matunda damu) yapo kwa wingi Lushoto, Mombo, Iringa...

Mikoa ya nyanda za juu kusini, Arusha, Lushoto nadhani hizi ndio makao makuu ya matunda ya kizungu Tanzania kwa sababu ya hali ya hewa...
 
Alafu kuna tunda makamasi hili lipo tabora na magongoti ni machachu kuliko chumvi
 
Ni watu wachache wanaenda kununua matunda Kariakoo
hakuna anaenda kununua MATUNDA kkoo ukipita hiyo mitaa unakutana na vitorori zina hizo bidhaa unasimama unanunua kwenda kuvila
ni matunda ya hamu ukiyaona ndio unapata hamu hapohapo sio ile ufunge safari toka bunju uje kkoo ununue hizo shelisheli
 
Back
Top Bottom