Mahesabu
JF-Expert Member
- Jan 27, 2008
- 6,015
- 3,946
Mbwana Matumla Adundwa kwa Knockout Philippines
Sunday, May 17, 2009 4:30 AM
Mbwana Matumla 'Golden Boy' usiku wa kuamkia leo ameshindwa kuwika nchini Philippines mbele ya bondia wao AJ 'Bazooka' Banal baada ya kupewa makonde mazito yaliyomfanya aliage pambano hilo kwa Knockout katika raundi ya pili. Kabla ya pambano hilo Matumla alikuwa gumzo nchini philipines kutokana na historia yake nzuri katika ndondi akionekana ni tishio kubwa kwa bondia huyo wa Philipines.
Katika pambano hilo lililofanyika kwenye mji wa Cebu nchini Philippines, AJ Banal au maarufu kama "Bazooka" alilitawala pambano hilo akimpa makonde Matumla kuanzia dakika ya kwanza ya mpambano huo.
Matumla ambaye alionekana dhahiri kuelemewa na mfilipino huyo katika raundi ya pili, ilimbidi aliage pambano hilo katika raundi hiyo baada ya kupewa makonde mawili mazito yaliyomdondosha chari kwa nyuma.
Matumla alijaribu kuamka bila mafanikio na refa wa pambano hilo alilimaliza pambano hilo katika raundi ya pili dakika ya 2:59.
Banal kwa ushindi wake dhidi ya Matumla, amefanikiwa kupata nafasi ya kuzipiga kwenye usiku wa mpambano wa kukata na shoka kati ya Mmarekani Floyd Mayweather na Juan Manuel Marquez julai 18 jijini Las Vegas.
Katika mpambano mwingine wa leo mkenya Morris "Virus" Chule alitandikwa kwa pointi na mfilipino mwingine Czar Amonsot.
source nifahamishe.com